Mtoto aliyefariki mwaka 2017 adaiwa kufufuka

Mtoto aliyefariki mwaka 2017 adaiwa kufufuka

Sasa hii migomba inayotumika kwenye hizi shughuli ni mingi sana,swali langu hao wenye mashamba ya migomba huwa hawalalamiki wakiona mingi imevunwa.
Mkuu, wachawi wana mashamba yao, yani wachawi wengine ni wakulima hawa hawa tunaishi nao mitaani so anachukua vitendea kazi shambani kwake au anaiba kwako mmoja na hutojua kamwe
mchawi anaweza kukuibia wewe nguo zako na usijue, anakupumbaza unazisahau
 
Kwa mfano hilo eneo linalosemekana mdio Gambosh hakuna Mgomba unaoweza kuota ni sehemu kavu sana swali langu huwa wanaitoa wapi?
 
UCHAWI UPO SIO BURE ILA SERIKALI HAIAMINI KATIKA UCHAWI
Kitu ambacho watu wengi wanachanganya ni hii ishu ya serikali na imani ya kishirikiba.

Ukweli ni kwamba Serikali inatambia uwepo wa uchawi kupitia sheria ya uchawi. Hii sheria ipo Tanzania tangu enzi ya muingereza na ndie aliyeileta miaka ya 1920s hadi leo inatumika.

Ni kwamba unaweza kumshitaki mtu kwa kufanya vitendo vya kishirikina/kichawi ila lazima upate ruhusa ya Mwendesha mashtaka wa serikali DPP.

Changamoto kubwa ya hii sheria ipo kwenyr muingiliano wa vitendo vilivyotajwa na hii sheria kama vitendo vya kishirikina/kichaei na vile vilivyotajwa kama vitendo vya tiba asilia na tiba mbadala, vilivyotajwa kwenye sheria ya tiba asili na mbadala. Yaani ni ngumu kumtenga mchawi na mganga kwa hii sheria, na kesi zipo moja ambayo ni 'landmark case' ni ya jamaa anaitwa Masamaki ilitokea huko usukumani Jaji alitaja vifaa vilivyoonekana kama vya kichawi kuwa ni vifaa vya mganga kama ilivyo daktari wa kisasa kuwa na vifaa kama sindano basi nao wana vifaa kama matunguri.

Sasa kwa kutokufahamu sheria za nchi watu wengi wanadhani na kufikiri kuwa serikali haitambui) kuamini uwepo wa uchawi.
 
Sasa hii migomba inayotumika kwenye hizi shughuli ni mingi sana,swali langu hao wenye mashamba ya migomba huwa hawalalamiki wakiona mingi imevunwa.
Rate ya kukua ni kubwa pia sio migomba tu hata nguo matambara, majani nk uweka
 
Yani wanalazimisha mambo ya uzushi, hamna mtu atakayekuja hadharani kufanya uchawi . Ni habari za kusimuliana kama mambo ya gharika kuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] viumbe wote walikufa sasa samaki walikuwaje
Mambo ya gharika ni kituko kingine, ni mjinga gani anaweza kuamini kua hakukuwa na watu wanao miliki boti ambazo wangetumia kujinusuru kipindi cha gharika?

Zaidi wakajaribu kutuhamisha fikra tusifikirie huko bali tufokasi kuangalia uzembe wa hao watu na jitihada zao za kujinusuru kwa kukwea miti mirefu

Ukisoma Genesis 7:19-24 inasema mungu alishusha mvua iliyodumu siku 40 ikinyesha usiku na mchana iliyosababisha mafuriko makubwa kiasi cha kuificha milima mirefu

If the highest mountains on earth was covered in water kwa siku 150, maji hayo yamepotelea wapi?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwanza dunia ingeganda maana carbon dioxide nyingi ingekuwa absord na maji[emoji1787][emoji1787][emoji1787]sasa wangeishine wakati temeprature ingedrop saba[emoji1787][emoji1787][emoji1787] habari zao hawa watu haziwezekani.. mimi naamini mambo ya wachawi yanatokana na story za dini zaidi kuliko hata uhalisia wa uchawi wenyewe
 
Rate ya kukua ni kubwa pia sio migomba tu hata nguo matambara, majani nk uweka
Lakini hadithi nyingi nilizosoma kuhusu Watu kufanywa Mazombie huwa na wanasema ni Migomba.
 
MTOTO MIAKA 11 AFUFUKA MKOANI GEITA.

Mtoto Leonard Morisha Mwenye umri wa Miaka 11 Mkazi wa kijiji na kata ya Ngemo wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita aliyefariki June 27 ,2017 katika hospitali ya Geita amefufuka baada ya kuzikwa kwa kipindi cha miaka 5 mpaka kufufuka kwake huku ikidaiwa kukatwa ulimi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo alionekana usiku katika kijiji cha Segese kata ya Msalala wilaya ya kahama akiwa anaranda randa katika Maduka.

Kamanda amesema mtoto huyo baada ya kuonekana katika Maduka hayo alikuwepo mlinzi katika Maduka hayo aitwae Emmanuel Busiga alimchukua na kumpeleka kwao badae alifikisha taarifa katika uongozi wa kijiji.

"Mtoto huyo ana afya njema lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi katika kituo cha afya cha Masumbwe alibainika kukatwa ulimi kwa kiwango kikubwa mishipa ya ulimi wake na kusababisha ashindwe kuongea, " Mwaibambe.

Mwaibambe amesema baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la polisi lilipata kibali kutoka katika Mahakama kwa ajili kufukuwa kaburi lake ambalo mtoto huyo alikuwa kazikwa na kukuta kaptura pamoja na suruali ya Baba mzazi wake aliyefariki mwaka 2019.

#KitengeUpdatesView attachment 2047442
Kama MTU anaamini kuna Mungu lakini haamini kuna ushirikina mwache tu aende zake usimbughudhi..atakurudia tu na ushuhuda wa kushangaza
 
Kwa mfano hilo eneo linalosemekana mdio Gambosh hakuna Mgomba unaoweza kuota ni sehemu kavu sana swali langu huwa wanaitoa wapi?
Mkuu,nimekuelewa, huwa wanaweza kuletewa kutoka sehemu nyingine ,ikumbukwe wachawi hawaishi gamboshi,ile ni kama office tu asubuh hurudi kwao na kuwaacha baadhi wakisimamia
hivo wale wanaorudi kwao ndio huja na migomba,alafu sio kwamba kila siku wanaua mtu so ni migomba michache sana hutumika
 
Kwahiyo hata Mchawi wa Mtwara ofisi yake ni Gambosh?
 
Kwahiyo hata Mchawi wa Mtwara ofisi yake ni Gambosh?
Gamboshi ni jina tu tunatumia sisi ambao sio wachawi ila ki uhalisia zipo Gamboshi nyingi nchi nzima so wa mtwara nao wana ofisi zao huko
 
Gamboshi ni jina tu tunatumia sisi ambao sio wachawi ila ki uhalisia zipo Gamboshi nyingi nchi nzima so wa mtwara nao wana ofisi zao huko
Gambosh ni Kijiji nadhani kiko Maswa au Bariadi kama sikosei.

Kinaaminika kwenye Stori za Wasukuma kuwa ni Kijiji cha Wachawi sijasikia kwenye Stori za Makabila mengine kwamba wana Vijiji vyao vya Wachawi.
 
uzi uliletwa humu na videos zipo youtube za hiko kijiji hivo upo sahihi, lakini kwakuwa hicho kijiji ndicho maarufu kwa uchawi na inasemekana kambi ipo huko kubwa basi watu huamini huko tu ndio kuna kambi ya uchawi
ukisoma comment ya story niliyosimulia humu asubuhi kwa mujibu wa jamaa aliyekumbwa na tukio yeye hakupelekwa nje ya mkoa wa mara kwa maana wakati wanalima aliona watu wa kawaida na pia wakati anarudishwa kutoka kwa wachawi ilikua within a day akafika kijijini kwao
 
Back
Top Bottom