Mtoto aliyejeruhiwa na ndugu zake 6 kuuawa kikatili Mkoani Kigoma naye afariki

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mtoto James Januari (4) aliyejeruhiwa katika tukio la mauaji ya watu sita wa familia moja yaliyotokea kwenye Kijiji cha Kiganza, Halmashauri ya Wilaya Kigoma amefariki usiku wa kuamkia leo Julai 5, 2022.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni, Dkt. Stanley Binagi amethibitisha kifo cha mtoto huyo kilichotokea kwenye Hospitali ya Mkoa Morogoro akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Dkt. Binagi alisema awali Marehemu James alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uangalizi zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye tukio hilo.

Mganga huyo Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa alisema kuwa marehemu alikuwa ameathirika mgongoni na kwenye fuvu la kichwa na kufanya sehemu ya mwili wake kutokuwa na mawasiliano.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya Kigoma, Ester Mahawe alisema kuwa walifanikiwa kumpa rufaa mtoto huyo kwenda Muhimbili na aliondoka Kigoma, Jumatatu jioni kwa gari akiwa na ndugu na wahudumu wa afya lakini alipofika Morogoro hali yake ilibadilika na kupelekwa Hospitali ya Mkoa Morogoro kwa msaada ambapo alifariki baadaye.

Kufuatia kifo hicho Mkuu huyo wa Wilaya alisema amewasiliana na viongozi wa kata na Kijiji cha Kiganza kutoa taarifa kwa familia ya mtoto huyo na kuandaa taratibu za mazishi ambapo mazishi yanaweza kufanyika kesho baada ya mwili kutarajiwa kufika leo jioni.

Kifo cha mtoto Januari kinafanya idadi ya watu waliokufa kwenye tukio hilo kufikia saba ambapo mtoto mwenye umri wa miezi mitatu alinusurika akiwa hajadhurika na kwa sasa amehifadhiwa kwa ajili ya matunzo na usalama wake.

Jeshi la Polisi chini ya usimamizi wa Kamishna wa operesheni na mafunzo, Liberatus Sabas limeanza uchunguzi wa tukio hilo huku Kamishna huyo wa polisi akiahidi kuwatia mbaroni wahusika katika kipindi kifupi kijacho.

Chanzo: Malunde

Pia soma
- Kigoma: Watu 6 wa familia moja wauawa kikatili usiku wa kuamkia Julai 3
 
Ila tunachekesha sana, yaani Kigoma Hadi Dar kwa gari na mgonjwa mahututi? Kama Mkoa Haina pesa si wangesema tukachangia ikakodishwa ndege? Hapa Kuna Manesi walishapiga hesabu za perdiem Mpya za 240,000 times 7days hahahaah
 
Mtoto James Januari (4) aliyejeruhiwa katika tukio la mauaji ya watu sita wa familia moja yaliyotokea kwenye Kijiji cha Kiganza, Halmashauri ya Wilaya Kigoma amefariki usiku wa kuamkia leo Julai 5, 2022.
Hili suala hadi mkuu wa mkoa awajibike kwa upumbafu huu! kweli hali ya mtoto.mbaya hivyo mnambeba kwenye gari zaidi ya kilometa 1400 kweli? huu ni unyama wa ajabu kabisa! kwa uchungu wa tukio lenyewe na bado mmeendelea kuleta masihara kwenye ishu za kitaifa kama hivi kweli? Mungu anawaona na soon KARMA will do the right thing!
 
Hili suala hadi mkuu wa mjoa awajibike kwa upumbafu huu! kweli hali ya mtoto.mbaya hivyo mnambeba kwenye gari zaidi ya kilometa 1400 kweli? huu ni unyama wa ajabu kabisa! kwa uchungu wa tukio lenyewe na bado mmeendelea kuleta masihara kwenye ishu za kitaifa kama hivi kweli? Mungu anawaona na soon KARMA will do the right thing!
Kabisa, noma sana.
 
Mtoto James Januari (4) aliyejeruhiwa katika tukio la mauaji ya watu sita wa familia moja yaliyotokea kwenye Kijiji cha Kiganza, Halmashauri ya Wilaya Kigoma amefariki usiku wa kuamkia leo Julai 5, 2022.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni, Dkt. Stanley Binagi amethibitisha kifo cha mtoto huyo kilichotokea kwenye Hospitali ya Mkoa Morogoro akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Dkt. Binagi alisema awali Marehemu James alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uangalizi zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye tukio hilo.

Mganga huyo Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa alisema kuwa marehemu alikuwa ameathirika mgongoni na kwenye fuvu la kichwa na kufanya sehemu ya mwili wake kutokuwa na mawasiliano.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya Kigoma, Ester Mahawe alisema kuwa walifanikiwa kumpa rufaa mtoto huyo kwenda Muhimbili na aliondoka Kigoma, Jumatatu jioni kwa gari akiwa na ndugu na wahudumu wa afya lakini alipofika Morogoro hali yake ilibadilika na kupelekwa Hospitali ya Mkoa Morogoro kwa msaada ambapo alifariki baadaye.

Kufuatia kifo hicho Mkuu huyo wa Wilaya alisema amewasiliana na viongozi wa kata na Kijiji cha Kiganza kutoa taarifa kwa familia ya mtoto huyo na kuandaa taratibu za mazishi ambapo mazishi yanaweza kufanyika kesho baada ya mwili kutarajiwa kufika leo jioni.

Kifo cha mtoto Januari kinafanya idadi ya watu waliokufa kwenye tukio hilo kufikia saba ambapo mtoto mwenye umri wa miezi mitatu alinusurika akiwa hajadhurika na kwa sasa amehifadhiwa kwa ajili ya matunzo na usalama wake.

Jeshi la Polisi chini ya usimamizi wa Kamishna wa operesheni na mafunzo, Liberatus Sabas limeanza uchunguzi wa tukio hilo huku Kamishna huyo wa polisi akiahidi kuwatia mbaroni wahusika katika kipindi kifupi kijacho.

Chanzo: Malunde

Namtamania sana uyo mtoto, ni direct peponi 🙂

Allaah atujaalie mwisho mwema.
 
Poleni sana wafiwa, Mungu awape wepesi
 
Mtu yuko Kigoma anasafirishwa kwa gari kuja Dar? Kwani gharama za mafuta ya gari kwenda na kurudi na wahudumu wote si zingefidiwa na tiketi ya ndege
Ndege zetu zinazoenda Kigoma (Bombardier) hazina stretcher, haziwezi kubeba mgonjwa asiyeweza kukaa na au anayehitaji uangalizi maalumu, labda wangekodi ndege binafsi which is way more expensive.
 
Back
Top Bottom