Mtoto aliyejeruhiwa na ndugu zake 6 kuuawa kikatili Mkoani Kigoma naye afariki

Mtoto aliyejeruhiwa na ndugu zake 6 kuuawa kikatili Mkoani Kigoma naye afariki

naongra
Ndege zetu zinazoenda Kigoma (Bombardier) hazina stretcher, haziwezi kubeba mgonjwa asiyeweza kukaa na au anayehitaji uangalizi maalumu, labda wangekodi ndege binafsi which is way ezpensive
unaongea kama upo Baa unakunywa wanzuki!
kwa hiyo kubebwa na gari inayoruka ruka spidi 160 siku 2 njiani ni sawa ee! si ndio maana wamemuua pumbafu na wewe
 
Mtu yuko Kigoma anasafirishwa kwa gari kuja Dar? Kwani gharama za mafuta ya gari kwenda na kurudi na wahudumu wote si zingefidiwa na tiketi ya ndege
Mkuu nimewaza exactly kama wewe. Watakuwa wamemuua wao,MTU yuko ICU unamsafirisha kwa gari na Barbara zetu hizi. Viongozi wetu hawa akili hazimo kabisa. Kutwa kucha wako kwenye kampeni za pedi kwa mtoto wa kike huku suala kama hili LA kuokoa maisha wanafanya masihara.
 
ILISHINDIKANA TIKETI KWELI YA KIGOMA KUJA DAR SERIKALI YA MKOA SIO WATU
 
Wako radhi wazuie hedhi kwa wasichana sio kuzuia kifo. Hahaha.....shamba LA wanyama.
 
Hawa Viongozi Sijui Vp, Ndege Zinakwenda Kigoma Kila Siku Walishindwa Nini?
Mtu yuko Kigoma anasafirishwa kwa gari kuja Dar? Kwani gharama za mafuta ya gari kwenda na kurudi na wahudumu wote si zingefidiwa na tiketi ya ndege

Wako radhi wazuie hedhi kwa wasichana sio kuzuia kifo. Hahaha.....shamba LA wanyama.
Labda hajatangaza kuomba msaada kwa wasamaria wema
Si unajua mambo mengine lazima uhojiwa na millard,lazima wangetokea wachangiaji wangesaidia kisifa
Mwisho wa siku mtoto angekodishiwa hata chopa

Ova
 
So sad kwa nn binadamu tunakuwa na roho za kikatili hivi?
 
Ndege zetu zinazoenda Kigoma (Bombardier) hazina stretcher, haziwezi kubeba mgonjwa asiyeweza kukaa na au anayehitaji uangalizi maalumu, labda wangekodi ndege binafsi which is way more expensive.
Wangechukua siti tatu za pamoja na mtoto alazwe hapo.
Kama mabasi yanabeba wagonjwa mahututi kwa nini ndege ishindwe?
 
naongra
Ndege zetu zinazoenda Kigoma (Bombardier) hazina stretcher, haziwezi kubeba mgonjwa asiyeweza kukaa na au anayehitaji uangalizi maalumu, labda wangekodi ndege binafsi which is way ezpensive
unaongea kama upo Baa unakunywa wanzuki!
kwa hiyo kubebwa na gari inayoruka ruka spidi 160 siku 2 njiani ni sawa ee! si ndio maana wamemuua pumbafu na wewe pia
 
Mtu yuko Kigoma anasafirishwa kwa gari kuja Dar? Kwani gharama za mafuta ya gari kwenda na kurudi na wahudumu wote si zingefidiwa na tiketi ya ndege
Posho
Hawakujali uhai wa mtoto
 
Ndege zetu zinazoenda Kigoma (Bombardier) hazina stretcher, haziwezi kubeba mgonjwa asiyeweza kukaa na au anayehitaji uangalizi maalumu, labda wangekodi ndege binafsi which is way more expensive.
Expensive kuliko maisha ya mtoto.mdogo kama huyo ambaye future iko gizani
 
Kigoma to dar kwa gari, mgonjwa yuko mahtuti.

Hivi kweli mbona hali imekuwa hivi, kigoma hakuna ndege ?
 
Mtoto James Januari (4) aliyejeruhiwa katika tukio la mauaji ya watu sita wa familia moja yaliyotokea kwenye Kijiji cha Kiganza, Halmashauri ya Wilaya Kigoma amefariki usiku wa kuamkia leo Julai 5, 2022.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni, Dkt. Stanley Binagi amethibitisha kifo cha mtoto huyo kilichotokea kwenye Hospitali ya Mkoa Morogoro akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Dkt. Binagi alisema awali Marehemu James alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uangalizi zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye tukio hilo.

Mganga huyo Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa alisema kuwa marehemu alikuwa ameathirika mgongoni na kwenye fuvu la kichwa na kufanya sehemu ya mwili wake kutokuwa na mawasiliano.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya Kigoma, Ester Mahawe alisema kuwa walifanikiwa kumpa rufaa mtoto huyo kwenda Muhimbili na aliondoka Kigoma, Jumatatu jioni kwa gari akiwa na ndugu na wahudumu wa afya lakini alipofika Morogoro hali yake ilibadilika na kupelekwa Hospitali ya Mkoa Morogoro kwa msaada ambapo alifariki baadaye.

Kufuatia kifo hicho Mkuu huyo wa Wilaya alisema amewasiliana na viongozi wa kata na Kijiji cha Kiganza kutoa taarifa kwa familia ya mtoto huyo na kuandaa taratibu za mazishi ambapo mazishi yanaweza kufanyika kesho baada ya mwili kutarajiwa kufika leo jioni.

Kifo cha mtoto Januari kinafanya idadi ya watu waliokufa kwenye tukio hilo kufikia saba ambapo mtoto mwenye umri wa miezi mitatu alinusurika akiwa hajadhurika na kwa sasa amehifadhiwa kwa ajili ya matunzo na usalama wake.

Jeshi la Polisi chini ya usimamizi wa Kamishna wa operesheni na mafunzo, Liberatus Sabas limeanza uchunguzi wa tukio hilo huku Kamishna huyo wa polisi akiahidi kuwatia mbaroni wahusika katika kipindi kifupi kijacho.

Chanzo: Malunde

Pia soma
- Kigoma: Watu 6 wa familia moja wauawa kikatili usiku wa kuamkia Julai 3
Kwanini wasinge mpeleka Benjamin mkapa Dodoma then specialist kutoka Muhimbili wangemkuta hapo maana kama vifaa vipo
 
Ukute kuna Mbunge huko , wala hakutoa neno kusaidia huyo mtoto aweze kusafiri kwa Ndege.

Kulingana na hali yake ilivyokuwa kutumia usafiri wa gari haikuwa busara.

Poleni sana wafiwa , wauaji wasakwe ili wafikishwe mbele ya sheria.
 
Mtu yuko Kigoma anasafirishwa kwa gari kuja Dar? Kwani gharama za mafuta ya gari kwenda na kurudi na wahudumu wote si zingefidiwa na tiketi ya ndege
Hii sekta ya afya inahitaji maboresho makubwa na uwekezaji mkubwa ili huduma muhimu zipatikane huku huku mikoani kuliko kutegemea sehemu moja pekee.
 
Back
Top Bottom