Mtoto anakohoa sana na wakati wa usiku hadi anatapika

Karibu
 
Muco-Asthalin
Prednisolone
Loratadine
Amox DT

Vyote apewe.kulingana na uzito wake
 
Hapo
Yeah ni kweli 100% nakubaliana na wewe as per my post # 16
Sasa hapo kuna masharti ya vyakula mpaka uwaza mtoto huyu atakula nn kwa mfano wangu wangu hatumii samaki,
Mayai,
dagaa,
karanga,
korosho,
maziwa ya ng'ombe..
Maharage ya soya
Pia mama take asitumie hivyo vyakula kama mtoto ananyonya
Pafume na mafuta yenye harufu msitumie mkiwa na mtoto.
 
Tatizo wengi wakiwapeleka watoto hosipitali wanahudumiwa na madakitari wa watu wazima badala ya madakitari wa watoto, hili nalo ni tatizo, jaribu kusisitiza uonane na dakitari wa watoto.
 
Kuhusu Masharti ya chakula Ni bora kwanza apime ili kupata majibu kila mtu anakuwa exposed na allergens tofauti
 
Kwani hako kanyama kameota?

Chunguza atakuwa anaanza kukohoa saa sita usiku mpaka saa nane usiku. Hii ni kwa sababu kunakuwa na mabadiliko ya hali ya hewa kutoka siku moja kwenda siku nyingine.

Kama kanyama hakajaota na kwenye familia hakuna athma, basi mtoto wako atakuwa ana aleji na mchanganyiko ufuatao unaweza kumsaidia.

1. Asali mbichi
2. Tangawizi
3. Vitunguu swaumu
4. Limao
5. Mayai ya kienyeji.

Pia, mchanganyiko huu uwe katika kimiminika ambapo utaweka maji kiasi kupunguza ukali wa limao na vitunguu swaumu.

Mchanganyiko huu hauna shida na atakuwa anakunywa tu kama chakula akijisikia.

NB. Hapo vya kusagwa visagwe.
 
Ndugu nikupe pole kwa kuuguliwa na mtoto,
Nakusihi nenda hospital kubwa zenye vipimo vya kuangalia mapafu ya mtoto, like Aga Khan maana hao wako mikoa mingi. Huenda mtoto wako ana Pneumonia na ndio maana anakohoa kwa stahili hiyo.

Wao watamuanzishia dose (mara nyingi za sindano [aina ya dawa sikuweza kunote]) na ile mitambo yao ya kumlainisha mucous mtoto ili aweze kupumua kwa nafuu. Ni tiba ya almost 24 hours.

Utafurahi pamoja na mwanao, fanya hivyo.
 

Approach nzuri kwa syndromic treatment. Ni kweli vikohozi vingi vinavyozidi usiku ni kwa mfumo wa allergy na visababishi vinakuwa kwenye mfumo wa maisha


Ingawa mzazi/mlezi wa mtoto huyu anastahili kusikilizwa zaidi:

1: Historia ya allery kwenye familia.

2: Kugatilia uongezekaji wa uzito wa mtoto.

3: Kusikiliza kifua.

4: Dawa, itategemea hapo juu.

5: Mabadiliko kwenye mwenendo wa maisha:

A: Jitahizi kuzuia vyakula vyenye rangi (artificial) kama: juisi za viwandani, ubuyu, popcorn za rangi, barafu/ice cream, yoghurt zenye rangi nk.

B: Kutokulaza watoto wakipulizwa na feni yenye kasi kubwa.

C: Kwa wale wanaowapa uji kuna shida ya unga wa uji ukichanganywa na karanga au mbegu za maboga.

D: Kuna watoto pia husumbuliwa na maziwa ya ng'ombe na blue band. Ni vitu vinahitaji ufatiliaji wa karibu, unaweza kuviondoa na kuweka kioja baada ya kingine.
 
Mcheki minyoo kwnza.

Then mpeleke kwa specialist wa watoto.
 
Nenda Tabata Segerea shuka muulize bodaboda yeyote kwa Dr Kundy ukifika Hospital hakikisha unaonana na Dr Kundy baada ya wiki leta mrejesho
 
Kama upo dar hebu jaribu ekenywa hospital waangalie tatizo ni hospital ya private
Huu ushauri ufate,mara nyingi tonsil husababisha kikohoz km unachokiongelea especially usiku
 
Daaah mkuu kwahiyo unakubali kabisa siku inaanza saa6 usiku?
 
Daaah mkuu kwahiyo unakubali kabisa siku inaanza saa6 usiku?
Sijajua ni kwa nini inakuwa hivyo. Ila kwa nilichojifunza kutoka kwa mtoto wangu, binafsi naweza kuamini kwa mkoa niliopo siku mpya hubadilika na hali yake ya hewa hubadilika kuanzia saa sita mpaka saba usiku.

Ukiangalia comment yangu ya kwanza nimeelezea tu kuhusu tiba lishe ila kiukweli sikutaka kueleza kwa undani ni kwa namna gani nime-experience hiyo hali kwa mtoto wangu.

Mtoto wangu alikuwa mchana kutwa anacheza vizuri tu, ikifika saa sita mpaka saa saba usiku ndio anaanza kukohoa mfululizo mpaka mpaka saa kumi na moja asubuhi ndio analala. Yeye hakua na kalimi. Mwanzoni nilihisi uchawi mana kila ilipokuwa inafika saa sita na dakika kadhaa mtoto anaanza kukohoa mfululizo mpaka huruma.

Nikamuuliza dokta mmoja hivi ndio akaniambia kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kuhamia siku nyingine. Pamoja na tiba lishe, ila akanishauri niwe nampa salbutamo usiku ili mwili uendane na mabadiliko ya hali ya hewa hiyo usiku.

Na kama hana kalimi au athma, hali hiyo huisha taratibu mtoto anapokua.
 
Hapana kacheck nimonia
 
Nashukuru sana wote mliojali tatizo la mwanangu. Ninajitahidi kufanyia kazi ushauri wenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…