Mtoto atolewa Shanga kwenye Mapafu bila upasuaji Muhimbili Hospitali

Mtoto atolewa Shanga kwenye Mapafu bila upasuaji Muhimbili Hospitali

Ndugu Zungu watanzania,

Tunaposema humu jukwaani kila siku kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu,imara na madhubuti wa Rais Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nuru ya wanyonge na nyota ya matumaini kuwa amefanya uwekezaji mkubwa katika Secta ya Afya tutaanza kueleweka vyema kwa sasa.

Hii ni baada ya jopo la madaktari bingwa wa kitanzania kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanya jambo la kishujaa na kupongezwa kabisa la kumtoa shanga katika pafu aliyokuwa ameimeza mtoto wa miaka mitano mwezi mmoja uliopita. Ambapo mtoto huyo aliimeza shanga hiyo kwa bahati mbaya baada ya kupaliwa wakati akiichezea mdomoni.

Shanga hiyo imetolewa kihodari na kitaalamu sana na kwa teknolojia ya hali ya juu sana mpaka unaweza fikiri kuwa zoezi hilo limefanyika kule Washington DC marekani kumbe ni hapa hapa katika ardhi ya Rais Mama Samia kipenzi cha watanzania wote wenye akili Timamu na wanaojitambua.

Ambapo madaktari hao wameeleza kuwa kama kusingefanyika utaalamu huo na kwa teknolojia hiyo ya hali ya juu ambapo waliingiza kifaa chenye camera na chenye uwezo wa kuinasa shanga hiyo basi ingelazimika kumfanyia upasuaji mkubwa ambao ungepelekea mambo mengine kama vile kutoa pafu au sehemu ya pafu na hivyo kuleta pancha kwa mtoto.

Madaktari hao jasiri na wenye mioyo ya kizalendo na wito wa kazi na wenye kuipenda kwa dhati kazi yao wametoa Rai kwa jamii kuwachunga vyema watoto hasa wanapokuwa wanacheza wenyewe au wanachezea vitu ,ili wasipeleke mdomoni na kumeza kwa bahati mbaya vitu wanavyochezea.

Haya yanafanyika huku Rais Samia akiwa tayari amewekeza na kutiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya afya kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya hospitali pamoja na kununua vifaa tiba,kusomesha wataalumu kama vile madaktari bingwa,kununua madawa na mambo mengine mengi sana. Ingekuwa zamani huko ungeshangaa mtoto huyu anaombewa michango kupitia vyombo vya habari kwa ajili ya kupelekwa Apollo India Lakini kwa sasa ni kama Apollo imehamia Muhimbili kwa kuwa huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini.ndio maana tunaona hata majirani zetu wanakimbilia Muhimbili na hospitali zingine zilizopo hapa nchini kupata matibabu .ambapo kwa mwaka jana zaidi ya mamia ya wagonjwa kutoka nje ya nchi walitibiwa hapa nchini .

Hongera sana madaktari wetu kwa kazi nzuri na ya kizalendo mnayoendelea kuifanya kuokoa maisha ya watanzania.chapeni kazi kwa moyo wenu wote na Mungu atawalipa kwa kazi yenu hiyo njema kabisa kwa watanzania. tunawapenda sana madaktari wetu na tunawaheshimuni sana. Mungu awe nanyi na awabariki sana.najuwa changamoto kama za kimaslahi huwa hazikosekani lakini muwe na subira na uvumilivu kwa kuwa Rais wenu na wetu Mh Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan ni mama wa upendo na huruma na anatambua kazi kubwa mnayoendelea kuifanya katika kujenga Taifa la watu wenye afya njema na nguvu,na hivyo ataendelea kuwaboresheeni marupurupu na maslahi yenu kwa kadri hali ya uchumi inavyoruhusu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Vp kuhusu wajawazito wanao fia hospitalini,,,iv akili huwa mnaziacha wap?
 
Ili ikusaidie nini kilaza wewe!
Jibu hoja

Kuna investment ya technology inafanywa na serikali ambayo wewe na ukoo wako wote cannot even contribute asilimia 0.01

Kengebluuzz
 
Jibu hoja

Kuna investment ya technology inafanywa na serikali ambayo wewe na ukoo wako wote cannot even contribute asilimia 0.01

Kengebluuzz
Pumbavu mkubwa wa lumumba wewe' ni wapi serikali inaweza kufanya jambo lolote la kimaendeleo bila kutumia kodi ya mwananchi kenge wewe?

Hiyo investment na technology inatokea tu bila kutumia fedha za walipa kodi?

Hivi lumumba pakoje? Mbona imejikusanyia vijana vilaza kiasi hiki?

Au ubongo huwa mnatupa wapi mkifika lumumba?
 
Pumbavu mkubwa wa lumumba wewe' ni wapi serikali inaweza kufanya jambo lolote la kimaendeleo bila kutumia kodi ya mwananchi kenge wewe?

Hiyo investment na technology inatokea tu bila kutumia fedha za walipa kodi?

Hivi lumumba pakoje? Mbona imejikusanyia vijana vilaza kiasi hiki?

Au ubongo huwa mnatupa wapi mkifika lumumba?
You have contributed nothing

Never you will

Continue typing
 
Back
Top Bottom