✓Julius Nyerere alisoma Arts akawa Mwalimu kabla hajaja kutuongoza kwa miaka 24
✓Ali Hassan Mwinyi, alikuwa Mwalimu wa Arts kabla hajaja kutuongoza kwa miaka 10
✓Benjamin Mkapa - alikuwa mwandishi wa habari (kama sijakosea) akisomea Arts kabla hajatuongoza kwa miaka 10 ya kuwa Rais wa Nchi
✓Jakaya Kikwete, alisoma Uchumi (Arts) kabla hajatuongoza kwa miaka 10
✓John Pombe Magufuli, alikuwa Mwalimu wa Kemia (Sayansi) kabla hajatuongoza kwa miaka 6 ya Rais wa Nchi
✓Samia Suluhu Hassan, alisomea Arts (Masuala ya Usekretari, Utawala) kabala hajakaa Magogoni miaka 6 sasa ya Rais wa Nchi
Sisi tumesoma Sayansi lakini tumeishia kuwa washika mikoba na waimba mapambio ya hao wa juu 🙌
Mwache asome anachopenda yeye, lakini usiache kumpa ushauri kuhusu uelekeo wa Dunia
Wakati unawazia kufanya biashara, usijilinganishe na Bill Gates, Elon Musk (au pengine Rais wa Nchi); Jilinganishe na watu mnao endana endana ndio utafanikiwa...tofauti na hapo utabakia kuwa motivation speaker tu.....
Niliwahi kumwambia mtu, bei ya petrol Marekani ikiuzwa shs 10,000 kwa lita; Nirahisi sana ukilinganisha na shs 4000 kwa Tanzania. ILA motivation speaker wa bongo wanalinganisha bei, ya Marekani sijui Ujerumani na Tanzania..