Mtoto kugomea shule akiwa kidato cha Nne

Mtoto kugomea shule akiwa kidato cha Nne

Awashirikishe pia viongozi wa dini, huwezi jua tatizo. Kabakiza mkia tu
 
Wazazi hebu tujifunze kuwasikiliza watoto wetu na wakati tunawaskiza tukumbuke hao ni watoto wetu ambao ni watu wazima wajao watakaotegemewa kufanya maamuzi mepesi na magumu kwenye jamii kwa ajili yetu na Yao pia.

Wakati huo huo tukumbuke kila mwanaAdamu ameumbwa tofauti kwa asilimia 100.

Tusikariri aina ya makuzi tuliyopata sisi tukidhani ndio misingi sahihi na haina makosa ndani yake.

Wengi wetu bado ni wazazi wachanga tusiojua hata miongo miwili ya malezi ikoje, nasi pia tuendelee kujifunza namna bora zaidi ya kuwalea na kuwakuza watoto wetu kuwa miongoni mwa viumbe wawajibikaji.

Wote ni binaadam lakini tuna tofauti katika maumbile na karama tulizopewa.

Kila mmoja wetu anachokipawa chake na hata watoto wetu pia.

Mtoto kupenda kuwa “dancer” sio kosa, mtafutie msingi sahihi wa kufikia ndoto zake bila kuharibu utaratibu (kukataa shule). Kama hakuna sehemu sahihi basi ni fursa nyingine kwa familia na jamii kutengeneza mazingira kwa ajili yao. Shule za muziki, shule za matumizi ya vyombo vya muziki, shule za kufundisha uchezaji wa muziki. Etcetera

Na kwa watoto wale waliofikia balehe basi tuvivae viatu vyao, tukumbuke tulipotoka, tuyakumbuke na kuzingatia yale mabadiriko ya kimaumbile yaliyotupata katika ukuaji wetu yaliyoandamana na mabadiliko ya kisaikolojia tuliyokumbana nayo. Ule mkanganyiko wa kihisia na moto uliowaka ndani yetu.

Tuliweza kuchomoka salama? Tuliwezaje? Tuliharibu wapi? Tulifanikiwa kiasi gani na kwa mbinu gani?

Tuwasaidie kwa kujitumia sisi wenyewe Kama sehemu ya mifano hai inayotakiwa kuwapo katika siku zote za maisha yao.

Tusimame nao sambamba, shida zao tuzifanye za kwetu, wasiwasi wao uwe wa kwetu huku tukijitoa kwao Kama ngao na nguzo zao wakati wote wa mahitaji na maisha yao.
 
Hasira mkuu ila sitakuja mpiga tena maana alizima kwa masaa sitamgusa nisije enda jela.

Kaa nae ongea mwambie huyo kijana anaweza kumtunza wakaish kama familia au baadae ndio akizaa arudi nyumbani. ?
 
Mimi siku hizi nikiona mtoto wa mtu ameharibika au hafanyi vizuri kwa lolote, sina cha kujudge zaidi ya kumuombea kheri.

Kuna watoto wanaharibika sababu hawajalelewa, wamejilea... Ila kuna mtoto anaharibika hadi unajiuliza nini shida?

Utaongea nae kirafiki, utapiga, utamueleza dunia ilivyo na mabalaa yake, utasali na kufunga na kujitesa ili maombi yako yafike lakini wapi, kuna siku nguvu za kuomba zinaisha kabisa unaishia kusema "Mwenyezi Mungu mimi nimechoka nakuachia wewe"

Kidemokrasia, utamuacha achague anachokitaka, na akichangua ukampa support hicho alichokichagua utashangaa kinamshinda pia. Utampa second chance ataharibu, utampa chances na chances you will end up being disappointed.

Jana nimeingia google kusoma, kuna baadhi ya watoto personality zao zinawafanya wawe wepesi sana kuchagua mambo ya hovyo, ukimuwekea vitu viwili kizuri na kibaya atachagua kibaya, ukimuwekea vitu viwili vizuri hatachagua chochote sababu kitu kizuri kwake ni boring na kibaya ndio kinaichangamsha akili yake.

Ni shida aiseee, usiombe kama mzazi/mlezi yakukute inauma sana unaweza tembea barabarani unaongea pekeyako. Kuna muda unaacha kila kitu unakaa kusubiri divine interventions, kama ni Mungu au mizimu ya kwao basi ifanye jambo.

Speaking as a sister/mlezi wa wadogo zangu wa3, wakiume ninayefuata nae wa amenidissapont zaidi ya mara 10, nimenyoosha mikono sasa. Hata hivyo namshukuru Mungu kwa ajili ya mabinti wawili njia yao imenyooka sana.
 
Hata mie nilikataaga shule form 5 Ila baadae sana nikasoma, niliulizwa unataka shule au ndoa, nikawajibu ndoa, wakanisusa Ila baadae wakanikubali tu baada ya kusomeshwa na aliyenizuzua[emoji38][emoji38]
Namshukuru Mungu nimefanikiwa kimaisha
Na sisi tunamshukuru Mungu wewe kufanikiwa, kwa wenzio inaweza isitokee hivyo.
 
Back
Top Bottom