Mtoto kugomea shule akiwa kidato cha Nne

Mtoto kugomea shule akiwa kidato cha Nne

Wewe tulia hujui uchungu wa ada wala nauli jumlisha mahitaji yake mengine.

Wewe unadhani kwa maisha ya sasa hataki shule kajiingiza kwenye mahusiano ni sahihi kwako.
Anaomba mvua wakati wa masika huyu!
 
Nipo hapa Dodoma eneo la Kisasa karibu na block F, Block F ni eneo ambalo wanakaa watu wengi wa kipato cha chini. Kuna binti alibahatika kufaulu hadi kufika kidato cha nne2023! Sasa cha ajabu alitoroka na kurudi, lakini hataki tena kuendelea na shule hadi wazazi wake wamempeleka polisi na polisi kuamuru akapimwe General hospital kama alivyotoroka hajarudi na mimba!

Ila cha ajabu Dr wa kuthibitisha hayupo toka jana! Je huyu mtoto haoni maisha ya chini ya wazazi wake? Kichwani amejiandaa kufanya kazi gani na wapi? Hizi ni changamoto za kujitakia.

Nasikitika sana
Karogwa huyo!!
 
Kwa hio akasome Archimedes principl
Una watoto? Kama wapo omba yasikukute. Sisi wazazi tunakasirika sana mtoto akikataa shule kwakua maisha bila elimu mambo mengi yatakupita na kwenye makuzi yapo mambo mengi ya kurekebisha mtoto mimi sio mfuasi wa kupiga ila ikatokea binti yangu kagoma kwenda shule atanisamehe tu lazima nimchape kutoa ujinga kichwani.
Na law of friction , quadratic equation afeli ? Upoteze ada
 
Kwa hio akasome Archimedes principl

Na law of friction , quadratic equation afeli ? Upoteze ada
Hakuna ada inayopotea elimu ni haki ya msingi kwa mtoto umaskini wetu ndio unafanya tuhesabu hela ya ada of which ni hela ambayo usingetakiwa hata kuiwazia kama unavyonunua dawa kichwa kikiuma ukajitibia huwezi anza fikiria 600 ya kidonge ulichonunua
 
Huyo siyi jeuri inawezekana ndo ile stage yake ya makuzi. Na ktk kipindi hicho wanaona dunia yote ipo mikononi wanaweza fanya kitu chochote.

Msitumie nguvu wala kuwapeleka polisi. Jenga urafiki naye mwambie mjenge kisaikolojia. Lkn pia mchukue mpeleke maeneo yenye watoto wenye uhitaji mfano kwenye makao ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu,,watoto wa mitaani.


Lkn changamoto kubwa tuliyonayo wazazi wa leo tunalea watoto wetu kuwa wasipate shida ambazo sisi tulipitia na hivyo mtoto na yeye anaishi humu kwa kuamini mzazi hata kama nisiposoma basi sitapata shida mbeleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora huyo kidato cha nne juzi nimetoka kumpiga mtoto wa dada yangu nusu niuwe yupo kidato cha kwanza hataki shule ila sijamshindwa bado [emoji51]

Muulize vizuri kwanin anakataa je atapenda kwenda shule nyingine?huwezi jua labda hapendi ongea nae taratibu tu muulize anapenda nin?kisha mshaurii vizuri kuhusu elimu
 
Back
Top Bottom