Mimi siku hizi nikiona mtoto wa mtu ameharibika au hafanyi vizuri kwa lolote, sina cha kujudge zaidi ya kumuombea kheri.
Kuna watoto wanaharibika sababu hawajalelewa, wamejilea... Ila kuna mtoto anaharibika hadi unajiuliza nini shida?
Utaongea nae kirafiki, utapiga, utamueleza dunia ilivyo na mabalaa yake, utasali na kufunga na kujitesa ili maombi yako yafike lakini wapi, kuna siku nguvu za kuomba zinaisha kabisa unaishia kusema "Mwenyezi Mungu mimi nimechoka nakuachia wewe"
Kidemokrasia, utamuacha achague anachokitaka, na akichangua ukampa support hicho alichokichagua utashangaa kinamshinda pia. Utampa second chance ataharibu, utampa chances na chances you will end up being disappointed.
Jana nimeingia google kusoma, kuna baadhi ya watoto personality zao zinawafanya wawe wepesi sana kuchagua mambo ya hovyo, ukimuwekea vitu viwili kizuri na kibaya atachagua kibaya, ukimuwekea vitu viwili vizuri hatachagua chochote sababu kitu kizuri kwake ni boring na kibaya ndio kinaichangamsha akili yake.
Ni shida aiseee, usiombe kama mzazi/mlezi yakukute inauma sana unaweza tembea barabarani unaongea pekeyako. Kuna muda unaacha kila kitu unakaa kusubiri divine interventions, kama ni Mungu au mizimu ya kwao basi ifanye jambo.
Speaking as a sister/mlezi wa wadogo zangu wa3, wakiume ninayefuata nae wa amenidissapont zaidi ya mara 10, nimenyoosha mikono sasa. Hata hivyo namshukuru Mungu kwa ajili ya mabinti wawili njia yao imenyooka sana.