Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia mtoto wa miaka 13 mkazi wa kijiji cha Minyembe halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka miwili.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema tukio hilo lilitokea Septemba 30, 2022.
Amesema mtuhumiwa anashikiliwa na polisi akisubiri uchunguzi ukamilike ili afikishwe mahakamani.
“Jeshi hilo lnakemea ukatili wa aina hiyo dhidi ya watoto, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote wanaoendelea kufanya ukatili kama huo,” amesema Katembo.
Sabina Samweli, mkazi wa kijiji cha Minyembe amesema muda tukio linatokea watu wengi walikuwa mashambani na watoto hao ni ndugu.
"Watu walikuwa mashambani huyo mtoto aliitwa na kaka yake wakaingia ndani, ila alipolia kwa sauti yule mdogo, watoto waliokuwa wakicheza jirani na eneo hilo walikimbilia ndani kufika wakakuta tukio limeshafanyika yaani huyu kijana asingekuwa ndugu yake nafikiri mimi ndio ningeenda jela haiwezekani umfanyie mdogo wako unyama kama ule."
"Nimejisikia vibaya huyu mtoto ni mdogo sana kufanyiwa kitendo hiki kibaya sana yaani ameumizwa sana yaani amemuingilia kinyume cha maumbile hii sio sawa," amesema Samwel