Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Mtoto niliyemkataa miaka 4 iliyopita, anafanana na mimi. Sasa ameletwa karibu na ninapoishi

Wanajamvi aisee nilimkataa mtoto miaka kama minne imepita.

Sasa ubaya leo kaja na mama yake sehemu ambayo karibu na kwangu, mtoto anafanana na mimi mpaka nimeona aibu nikaangalia pembeni.

Sasa ubaya mama yake sijui kafanya makusudi kahamia huu mtaa aisee yaani dogo bora asingefanana na mimi, ni noma.

Inapoelekea ndoa yangu itaharibika maana dogo anachezacheza na wenzake karibu na kwangu ubaya akija kuanza mazoea na wanangu naona kama nitaumbuka.

Nishaurini nifanyaje wadau.
Mwanaume usikose la kusema. Kama mkeo atakuja kuhisi kitu kuhusu kufanana kwa mtoto huyo na wewe.
1. Mwambie tatizo ni wewe mwaka ule ulipokuwa unaninyima unyumba kwa visingizio mbalimbali kwa kweli mke wangu nilichepuka ikawa hivyo unavyoona. Kuhamia huku imetokea kama bahati mbaya mume wake kahamia huku mara walipooana hivi karibuni, hata hajui kama niko huku. Tatizo ni wewe kamwe halingekuwepo hili.
 
Unakataaje damu yako?
Sasa kama unamkubali shida ipo wapi? Mwambie mkeo una mtoto, hakuna jipya kwenye haya maisha mwisho ni kifo kinakusubiri.
 
Mwanaume usikose la kusema. Kama mkeo atakuja kuhisi kitu kuhusu kufanana kwa mtoto huyo na wewe.
1. Mwambie tatizo ni wewe mwaka ule ulipokuwa unaninyima unyumba kwa visingizio mbalimbali kwa kweli mke wangu nilichepuka ikawa hivyo unavyoona. Kuhamia huku imetokea kama bahati mbaya mume wake kahamia huku mara walipooana hivi karibuni, hata hajui kama niko huku. Tatizo ni wewe kamwe halingekuwepo hili.
Sawa mkuu
 
Dah mbona mnaniponda naongea uhalisia au mlitaka nisisime ukweli
Kwa hiyo unakili mtoto ni wako si Ndio?, kama Ndio lea, swali kati ya mkeo na huyo mtoto ni yupi alianza kuwa sehemu yako? Kama mwanamke aliingia kwenye ndoa mtoto akiwa amezaliwa, akubali yote, Amie ila mpange, kama ulizaa nje ukiwa na ndoa wewe Ndio mzinguzi tuliza chovyachovya
 
Na akikuambia kuwa sio mtoto wako? Kuwa baba yake yupo na ndie anayemlea!

Amandla...
 
Kabisa. Sasa ona, mamaake mtoto kafyatua kopi utadhani mbaba alitumbukizwa kwenye mashine ya kutolea kopi, kumbe mbususu..!!
Hahahahaah na mara nyingi huwa hivyo mimba zenye mashaka..au mimba zenye kukataliwa Mungu huwa anawanyoosha wababa...
 
Back
Top Bottom