Hakuna academic privacy duniani kote? Sasa mtu kama wewe jamani huna hata a smidgen of exposure ya dunia inavyokwenda, tutajadili nini na wewe?
Total waste of time.
Kwa hiyo kubandika matokeo ukutani kumekomesha wizi wa vyeti?
Ni utafiti gani umeonyesha kwamba watoto wa zamani walikuwa wanafaulu zaidi kwa sababu matokeo yalikuwa made public?
Halafu unawaita watoto mburura. Hivi mtu mwenye akili unaweza kumuita mtoto mburura kwa sababu kapata division IV? Such an unbridled moral decay in the nation.
Unaficha matokeo ili iweje?
Matokeo ni bora akapewa mtu mwenyewe na wazazi wake kwa sababu unapomzodoa mtoto kwa kumtangazia matokeo mabaya unaweza kumuachia trauma ambayo itafanya achukie shule moja kwa moja na asijaribu tena.
Na pia unapomtangaza kwamba alifeli shule, na ukamuita kilaza hadharani, kama mheshimiwa Rais alivyofanya kwa wananchi wake vijana, huyu mtu husaidii kumuachia confidence ya kujaribu mambo mengine nje ya taaluma kwa sababu umesham label kwamba ni failure, kilaza, maishani. It is not very constructive by any stretch.
But more than anything, sio kila aliyefaulu shuleni amekuja kuwa model citizen maishani, kama ambavyo si wote waliofeli shule wanaishia kuwa hohehahe mbeleni. Raia mmoja wa nchi hii ambae alianza kama mpiga shoe shine hakuwa na elimu ya kutisha wakati akiijenga Azam, lakini kwa sasa anamiliki the biggest business conglomerate in the country na anaajiri wasomi wetu wa kila aina. Kama taifa tusidharau makundi ya watu ambao hawakufanya vizuri shuleni, hawajapoteza nafasi ya kuwa hazina kwa taifa.
Nimefeli shule, ndio, lakini sioni kama hilo linadhoofisha hoja yangu kwamba kubandika matokeo ya watoto na kuwaita vilaza kwenye hotuba za Rais haijengi. Kama ni mikopo na nafasi za vyuo ni wao wenyewe wamewapa, kwa nini Rais awatukane?
Unapotaka kutatua tatizo la uduni wa elimu nchini haisaidii kujikita kwenye kulizodoa kundi la ambao hawakufanya vizuri.