Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Huo mnaoueneza ni uongo ,DV 4 kwa mtu mwenye D 3 na C moja unakwenda chuo kikuu bila kupingwa ,unafuata hatua zifuatazo unakwenda certificate mwaka mmoj Then unaingia diploma miaka miwili,ukitoka unakwenda kusoma degree,Au option nyingine unaweza kwenda ualimu grade one,then unakwenda diploma,then degree...Tatizo kabla hamjatoa hoja chambua kwanza ndugu
Hatukatai hayo lakini huyu binti alimaliza form 4 mwaka 2011 matokeo yakatoka 2012 ilitakiwa aanze cheti mwezi wa 9 2012 mpaka mwezi 7 2013 aanze diploma mwezi wa 9,2013 mpaka mwezi wa 7,2015 lakini huyu tayari yupo mwaka wa pili UDOM Alidahiriwa mwaka 2014.
 
Naona panzi wameanza kutunishiana misuli, sisi mwewe tuko tunaruka ruka karibu na eneo la tukio kufaidi matokeo.
 
Mtu akiwa na D 4 anaruhusiwa kufanya professional course then asome foundation course kama atafaulu anaweza kuomba chuo kikuu na akakubaliwa.
So kwa nchi hii kama mtu akimaliza form 4 anaweza kuwa chuo kikuu baada ya miaka 2 bila kuchakachua popote.
Na kama ataenda kwa mtindo wakawaida kama alivyokua anasema rais ataanza na cheti mwaka 1, then diploma mwaka 1 halafu degree ni sahihi.
Ila hawezi kutoka form four tukamkuta chuo kikuuu
Diploma huwa miaka 2 lakini kama ni hivyo kwanini rais aseme haiwezekani mtu aliyemaliza form 4 asiende chuo kikuu kulikuwa na haja gani kuwafukuza wanafunzi wa udom wanaosoma diploma kwa miaka 3.
 
Tunamuomba mh Ndalichako atolee tamko juu ya haya matokeo ya huyo mtwanafunzi
 
Kama form 5 na 6 kafanya vizuri anaweza kuchuguliwa kwenda chuo kikuu.
Inakua tatizo kama hajapitia high level au certificate au diploma.

Lakini yeye baba kama anajua kuwa Div 4 ya 30 ambayo inachungulia shimo la Div.0 ni ukilaza ilikuwaje akamsomesha tena.

Na ni High leveel ipi wanachukua shimo la Div 0?????

LUNYA ANYE BATA AKINYA KUKU ATAAMBIWA KAHARISHA!!!!!!!!!!!!!!

Bajeti.jpg


Bora Ukimwi kuliko CCM.jpg


Abiria Tanzania.jpg

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
ahahaahahaha MKUU njoo huku nimekutafta nikutag sijakuona, eti wadau wanasema mbona First Daughter ni KILAZA ila mi simo.
Kwani First daughter alipata div ngapi vile....
ahahahaahaha
 
Kama elimu ya wanawe imemshinda hii ya nchi ataiweza? Kama huyu binti kaingia kwa magumashi mbona yeye kama mzazi hakumzuia?
 
Ila hii nchi bwana watoto wa viongozi wakubwa serikalini asilimia kubwa ni VILAZA ushahidi mnao wenyewe kuanzia uongozi wa awamu ya kwanza mnawajua VILAZA wa mwalimu sitaki niwataje niishie jela mie mpaka Sasa hivi ingawa hapo kati kuna ukakasi kwani kuna mmoja sijawahi kusikia mtoto wake sijui hana au ndio wapo nje ya nchi tangu wanazaliwa...

Asilimia kubwa ya VICHWA nchi hii wametokea kwa mkulima...hakuna namna mtoto wa kiongozi akaongoza school...hata yule aliyejiita mwanasheria na elimu yake ya kubahatisha kama dingi..... akaaaa simo nimesema tu nisije ishia pabaya mie
 
Akili za wa Tanzania bana wameacha kujadili matukio, wameanza kumtafuta mtoto wa Magufuli. Kwa hiyo kama mtoto wa Magufuli ni 'kilaza' mlitaka na hawa vilaza wengine waendelee kukumbatiwa?
 
Back
Top Bottom