Ndugu wa forum mie pia nimeguswa na huu upotoshwaji unaoenea kwenye hii thread, kwa data nilizonazo kutoka kwenye reliable source ni hivi.
Ili kufika kusoma degree kwa nchi yetu kuna njia mbili watu wanapitia
1. Kutokea A level
2. Kutokea Diploma na si vinginevyo na kwa yule mwenye diploma kwa taratibu za NACTE ni lazima awe amepitia mafunzo ya miaka mitatu yaani NTA Level 4 (Basic Technician Certificate) mwaka mmoja, then NTA Level 5 (Technician Certificate) kwa mwaka mmoja na NTA Level 6 (Ordinary Diploma) kwa mwaka mmoja. Na utaratibu huo Huwezi kuvuka level moja kwenda nyingine kama huja qualify kwa GPA ya 2.0 yaani Pass au zaid kutokana na vigezo vitavyoelekezwa na chuo but isipungue hapo kutoka kwenye level ya chini.
Pia ili kusoma NTA level 4 yaani entry level qualification za NACTE ni Pass 4 Olevel kwenye masomo yasiyo ya dini na tukiangalia huyu anaye zungumziwa hapa anavyo na kilicho mpeleaka chuo kikuu ni diploma ambayo kutokana na taarifa nilizo nazo huyu anazo na alifaauli vizuri diploma ya HR pale Public service Institute Na kupitia mfumo wa udahili wa pamoja kati ya TCU na NACTE akachaguliwa Chuo kikuu dodoma kama inavyoonyweshwa kwenye kozi ambayo alisomea diploma yake.
Huu utaratibu upo sehemu mbalimbali duniani walio na mifumo ya Technical Education Fuatilieni mjue ukweli an sio kupayuka tu bila kufanya reaserch
Nawakilisha