Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Mtoto wa Magufuli (Jesca) sijui alifikaje Chuo Kikuu?

Kama unadhani kauli zako wewe na wenzako hamdhalilishi Rais basi poleni sana...there is a big problem...nadhani hamuelewi mtendalo, na hili ni tatizo kubwa....
tumemdhalilisha kwa lipi?
 
Swala ni Jessica amedahiliwa vipi chuo kikuu...and lemme remind you tunatokea katika background tofauti tofauti na kutokana na kasi ya ukuaji ya utandawazi kila kitu kipo wazi...mzazi anaheshimiwa na sio kuabudiwa...kama mzazi amekosea unamrekebisha lakini katika njia sahihi...hakuna aliyemdhalilisha huyo baba yako ila tunajadili mtoto wake amefika vipi chuo kikuu within two years only??? Usichoropoke nje ya mada hatutaki mada ndani ya mada


Nadhani wewe ndiyo kwanza unagfungua uzi huu, na ni wazi hujasoma comments nyingine humu kuhusu issue hii, na kama umesoma comments zote katika uzi huu na ukaona sawa, basi pole...NO RESEARCH NO RIGHT TO COMMENT
 
Nadhani wewe ndiyo kwanza unagfungua uzi huu, na ni wazi hujasoma comments nyingine humu kuhusu issue hii, na kama umesoma comments zote katika uzi huu na ukaona sawa, basi pole...NO RESEARCH NO RIGHT TO COMMENT
Hahahahahha unanichekesha sababu wewe ndiye hujafanya research maana ungefanya research basi ungebaini nipo tangu mwanzo wa Uzi mpaka unakaribia number 2,000 na mpaka hapo hakuna jibu la kafika vipi degree ndani ya miaka miwili mtu aliyetandika four la 30...nikupe pole tena once again
 
Unajaribu kumtoa nje ya mada husika...iwe laana, mashetani, majini and whatever the issue is Jessica amefika vipi degree chuo kikuu ndani ya miaka miwili kwa mwanafunzi aliyefeli (kilaza) form four???? Mambo ya kauli and other issues ain't our issue hommie
 
Pitia comments zote kuhusu suala hili na halafu ufanye tathmin yako....
Kama kuna sehemu amedhalilishwa huu uzi ungefutwa na Mods kwavile amna ndio maana una huone uko mpaka sasa hivi.
 
Unajifanya hujaelewa????Baba yako mzazi unaweza ukamdhalilisha hivyo kama unavyomdhalilisha Rais?

kama huropoki ebu lete hata neno moja nililomzalilisha rais, usipoleta basi wewe ni mropokaji
 
Chuo gani hicho nimpeleke mtoto wangu asiyeende form 5? Hicho chuo kinasoma mfululizo bila kupumzika wala kwenda field hizo ndizo elimu ambazo hatuzitaki na kama ni kwanini muafukuze watoto wanaosoma diploma miaka 3.?
Wenzio wanazitaka waache wasome msiwaonee wivu. Kwani mazoezi kazini unahitaji mwaka mzima?
 
kama huropoki ebu lete hata neno moja nililomzalilisha rais, usipoleta basi wewe ni mropokaji

Nimeshindwa kuendelea na wewe katika mjadala huu kwa kuwa ni wazi nahisi upeo wako wa kujadilili hoja ni wa kiwango cha chini...Hii inajidhihirisha na namna unavyoandika maneno mbalimbali:

nilizomzalilisha>>>>>>>>>NILIVYOMDHALILISHA

ebu>>>>>>>>>>>>>>>HEBU
 
Kumbe mnajua hayo yapo mbona mnataka kujitoa akili
Hapana mi sijajitoa akili ila nadhani we hukunielewa ama hatuki kunielewa, nimekufafanulia nini maana foundation course na hatua mpaka mtu adahiliwe kuwa kwenye foundation course.
. Muda kati ya 2011 na oktoba 2014, unakitosha chuo kinachohitaji wanafunzi wa shahada, kuandaa wanafunzi wa kidato cha nne kufikia sifa ya kudahiliwa. Kipindi hiki kinazaidi ya miezi 30 ambayo inatosha kuwafanya wanafunzi hawa kusoma
Hapana sio ukweli na hiyo sio foundation course jinsi ilivyo kwa mifumo ya elimu ya tanzania jinsi ilivyo, na hakuna chuo tanzania kinachotoa foundation course kuanzia mwanafunzi wa form 4. hii kwa nchi yetu hakipo kitu kama hiko, foundation course huwa zinatolewa ndani ya miezi kama mitata au minne kabla ya chuo kufunguliwa ni kwa wanafunzi walioshindwa kufikisha minimum requirements, ngoja nikueleweshe hapa chini,
Ili mtu aweze kujiunga na chuo kikuu kwa ajili ya masomo ya shahada anatakiwa awe ni vitu vifuatavyo kwa mahitaji ya TCU.
1. AWE AMEMALIZA KIDATO CHA SITA
2. AWE NA ELIMU YA DIPLOMA
3. AWE na principal passes 2 ambazo ni sawa na point 2 kwa diploma basi AWE NA GPA 2.0
sasa kwa sababu chuo ni taasisi zinazojitegemea huwa wanaseti minimum requirements zao wenyewe kwa kutumia TCU kama standard kwa mfano SUA ilikuwa ni 3.5~4 UDSM kwa baadhi ya courses ilikuwa 5, Sasa kuna wanafunzi wamekuwa wametimiza standard ya TCU kujiunga na vyuo lakini hawajatimiza point zinazotakiwa na chuo husika, sasa hapa chuo husika ndo kinaanza kutoa kile kinachoitwa foundation course kwa miezi kadhaa ili ukidhi viwango vya kujiunga na chuo chao.

astashahada miezi 9 na stashahada miezi 18 kwa mihula minne ya miezi minne ya masomo ambayo inatosha kubeba module za stashahada.
kwa aliyemaliza mwaka 2011 haiwezekani awe amemaliza diploma 2014, mkuu hili haliwezekaniki hata siku moja, nakufafanulia hapa chini.
mtihani mwezi wa kumi 2011 majibu ya mtihani kimakadilio ni mwezi wa 3/2012 hivyo basi mtiririko ni kama ifuatavyo
10/2012-7/2013===Certificate(cheti).
10/2013-7/2014===Diploma mwaka wa kwanza
10/2014-7/2015===Diploma mwaka wa pili.
10/2015-7/2016===Degree mwaka wa kwanza.
Nimekuelezea hapo juu maana ya foundation course kwa vyuo vya tanzania sasa tuambie kama ni kweli yupo mwaka wa pili amefikaje? na amepitia foundation course kama inavyotakiwa kama ni hivyo amefikaje mwala wa pili?

Nafikiri nimeongeza nyama kwa kile ulichokuwa nacho kutoka saut. Kila chuo kinaweza kuja na muundo waka ili iweze kuvutia wanafunzi.
Hakuna kitu kama hicho Tanzania kwa chuo kutoa foundation course kwa mwanafunzi wa form four tofauti na ile special diploma.
Nimekuelezea hapo juu maana ya foundation course kwa vyuo vya tanzania sasa tuambie kama ni kweli yupo mwaka wa pili amefikaje? na amepitia foundation course kama inavyotakiwa kama ni hivyo amefikaje mwala wa pili?
 
kwiiii kwi kwiii, kapiga mbizi, du!!!!
kuanzia mwakani watatoa matokeo kwa namba za mitihani, mambo ya majina yanatuaibisha, wanaoafiki waseme siyo,
siyoooo, wanaopinga waseme ndio,
ndiyooooooooooooooooooooooooo!
Obrigado
Hata wakitoa kwa namba watu waliokuwa wizarani bado wana uwezo wa kuvujisha hizo namba kwa umma
 
Usituchanganye bhana! Huyu ni mtahiniwa wa mwaka 2011 na kwahiyo matokeo yake yalitoka 2012!

Any study program, ingeanza anywhere from July 2012 to September 2012 na kwa hesabu zako ingeisha anywhere from May 2014 to July 2014.

Haya piga hesabu sasa kutoka July 2012 hadi July 2014 halafu utuambie hiyo miezi ZAIDI ya 30 inatoka wapi!
Anayewakataza kuanza mwezi wa tatu baada ya matokeo kutoka ni nani ili kufikia malengo.
Ndio tatizo la kulishwa ujinga. Sasa aliyewafuga anafurahi kuwaona mkiangaikia humu jamvini.
 
Back
Top Bottom