Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Siasa za ndani ya CCM zimegawanyika kwenye makundi manne. Kundi la kwanza ni la koo zinazomiliki chama hicho. Hizo koo ambazo si nyingi, ndizo huamua muelekeo wa CCM.
Kundi la pili ni kundi la pangu pakavu tia mchuzi, kundi la wanasiasa wajuzi ama kwa bahati wanaofanikiwa kufika ngazi za juu za madaraka kwenye CCM. Kundi hili ni kundi linalotumiwa na zile koo zinazomiliki CCM kutengeneza picha kuwa CCM kila mtu anaweza kuwa kiongozi.
Kundi la tatu ni kundi wezeshi ambalo ndani ya kundi hili wapo watu ambao hutumiwa na kundi la Koo za wenye CCM kuonesha kuwa CCM ni chama cha umma.
Kundi la nne ni kundi la wanachama wa kawaida ambao wapo CCM kwa mazoea tu, woga, kujikomba, ujinga, umaskini, na hata ushirikina.
Leo nimemsikiliza mtoto wa Marehemu John Komba (toka kundi wezeshi) akimnasihi mtoto wa Marehemu Job Ndugai toka kundi (Pangu pakavu tia mchuzi) juu ya maisha yao watoto wa Ndugai yatakavyokuwa baada ya baba yao kufariki
Kumbe watoto wa Komba baada ya baba yao kufariki walitelekezwa na CCM😳