Mtoto wa miaka 15 auawa na Jeshi la Police Mkoani Mwanza

Mtoto wa miaka 15 auawa na Jeshi la Police Mkoani Mwanza

Huyo mtoto chanzo kufuatwa na mitutu?
Polisi wameua wakamatwe
Yawezekana dogo kuna siri kubwa au tukio kubwa alishuhudia kwa macho wakifanya police au kiongozi fulani mkubwa,so ili kuua soo ni kumzimisha dogo kabla hajaropoka,yangu ni hayo.RIP dogo langu

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Tujiulize Huyu mtoto alikosa nini? Asije akawa panya road wanaochoma watu visu bila huruma!

Nina Dada mmoja licha ya kutoa hela na simu bado alichezea mapanga. Ni bora ukutane na jambazi Jombi kuliko hivi vitoto, ni mapanga na visu lazima wakukate
 
Haya mambo ndo tunataka tuone Rais na viongozi wenzake wanayafanyia maamuzi ya haraka na jamii ikapata majibu.....Hii nchi ina viongozi wa ajabu...vitu kama hivi huwezi ukaviskia viongozi wanaviongelea kwa uzito.....watu wako bizy na tozo tu..Mama aanze kutumbua tu
 
Duh mtiririko wa habari haueleweki- lkn Sasa kwa haya mauaji ya polisi yalivyokithiri ni vyema kuwepo na kitengo cha internal affairs ambacho kitadeal na askari wakiukaji wa maadili na wavunja Sheria.

Hawa Division O wamezidi kujichukulia hatua mikononi kinyume cha sheria
Mkuu hoja yako ni nzuri, isipokuwa umeiharibu ulipoiwekea wigo na ubaguzi.

Uozo nchi hii ni mpana kuliko unavyodhania wewe!

Manyanyaso ya Mapolisi kwa raia, yana tofauti gani na manyanyaso yanayofanywa na mahakimu na wanasheria kupindisha na kupoka haki za watu mahakamani?

Div 0 ya mapolisi vihiyo si sababu toshelezi ya kutenda dhambi ya uadilifu hapa nchini bhana!

Kuna viongozi wangapi ambao hawakusoma ama kupata elimu ya juu, lakini waliongoza kwa uadilifu wa kutukuka?

Haujasikia Phd holders na maprofesa walioaminiwa na umma walivyogawana mabilioni kwenye viroba vya sandarusi kwa pesa za Iptl na kina profesa Anna kuziita hela ya mboga, tayari umekwisha kusahau?

Haujawasikia kina "joka la makengeza" kutohoa mikataba ya Trl na fedha chafu walizohodhi ughaibuni zilizopatikana kwa skendali hilo kuziita vijisenti?

Umesahau au hautaki kukumbuka kina Basil Mramba enzi zao waliyoyafanya?

Nimekupa "causion" hiyo ndogo katika trillion za uozo uliotamalaki katika jamii yetu ili ubongo wako usiuwekee wigo katika kutafakari.

Kungelikuwa na viongozi na serikali inayofuata sheria na haki, hao wahalifu waliomo ndani ya magamba ya nyadhifa na vyeo mbali mbali serikalini, wasingelithubutu kufanya wanayoyafanya hivi sasa kwa raia maskini!

Tushikamane kama Taifa bila kubaguana kielimu, kikanda, haiba ya mtu nk nk, maana kila eneo linaloitwa Taifa ama Nchi, lazima liwe na watu "kamchanganyikeni" , wenye elimu na wasio na elimu, wenye nacho na wasiokuwa nacho nk nk, lakini linapokuja suala la haki, basi matabaka yote ni kitu kimoja na hakuna lililopo juu ya sheria ama bora kuliko jingine.
 
View attachment 2354967Kijana Yahaya Aboubakar mwenye umri wa miaka 15 anadaiwa kukamatwa na askari polisi nyumbani kwa bibi yake mtaa wa Juhudi, Kata ya Mabatini wilaya ya Nyamagana Septemba 2, 2022, akiwa mzima, kisha polisi hao waliondoka nae na kumfungia ndani bibi yake Yahaya ambapo baada ya kufanikiwa kutoka ndani alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake katika vituo vya polisi na kumkosa.

"Wakasema wewe mama fungua nikawauliza nyie kina nani? mna kibali cha kuingia humu wakasema wao ni maaskari mbona hakuna mwenyekiti wala balozi wakasema ukigoma kufungua tunapiga mawe, baadae saa kumi na mbli marehemu akafika mjukuu wangu akawekewa mtutu huku na huku akaambiwa fungua mlango akafungua mlango wakamshika wakamuweka chini marehemu akalalamika akasema msinipige mimi sijabisha mnipeleke tu kama ni kituoni mimi nikamwambia mtoto huyo ni mgonjwa msimpige mpelekeni tu tutamfuatilia" ameeleza Bibi wa marehemu.

Mama mzazi wa Yahaya, Rehema Simba, amesema baada ya kuzunguka vituo vyote vya polisi kikiwemo kituo kikuu cha Nyamagana na kumkosa kijana wake ndipo akakutana na mkuu wa upelelezi akamwambia aende kwa RCO ili amueleze mtoto wake alipo.

"Baada ya kufika kwa RCO akasema shida nini nikamuelezea kwamba tumekuja ofisini kwako kuna kijana wangu amekamatwa tumeshazunguka vituo vyote vya polisi hatujampata akasema mtoto wako yupo Bugando Mochwari nikamuuliza mochwari amefuata nini? mbona mapolisi walimchukua nyumbani akiwa mzima? akaniambia kwamba baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa eneo la mashiri na kupigwa na wananchi ndipo akafariki," ameeleza mama wa marehemu.

Ramadhan Ng’anzi ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, amesema bado uchunguzi unafanyika wa tukio hilo na atakayebainika kuhusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo:- East Africa Radio
Nilwahi kusema kuwa hakuna cha Sirro Wala Cammilius Wambura Polisi ni walewale ambao kwao maisha ya binadamu asiyekuwa na undugu na mzito yeyote Serikalini hayana thamani yoyote kwa aliyebahatika kuishi jirani na kituo cha polisi anajua ninachosema vipigo vya kule ni afadhali kambi za mateso za Hitler lakini je haya mambo mwisho wake ni lini? Hadi wafe wangapi?
 
Mkuu hoja yako ni nzuri, isipokuwa umeiharibu ulipoiwekea wigo na ubaguzi.

Wigo wa uozo nchi hii ni mpana kuliko unavyodhania wewe!

Manyanyaso ya Mapolisi kwa raia, yana tofauti gani na manyanyaso yanayofanywa na mahakimu na wanasheria kupindisha na kupoka haki za watu mahakamani?

Div 0 ya mapolisi vihiyo si sababu toshekezi ya kutenda dhambi ya uadilifu hapa nchini bhana!

Kuna viongozi wangapi ambao hawakusoma ama kupata elimu ya juu, lakini waliongoza kwa uadilifu na kutukuka?

Haujasikia Phd holders na maprofesa walioaminiwa na umma walivyogawana mabilioni kwenye viroba vya sandarusi kwa pesa za Iptl na kina profesa Anna kuziita hela ya mboga, tayari umekwisha kusahau?

Haujawasikia kina joka la makengeza kutohoa mikataba ya Trl na fedha chafu walizohodhi ughaibuni kwa skendali hilo kuziita vijisenti?

Umesahau au hautaki kukumbuka kina Basil Mramba enzi zao waliyoyafanya?

Nimekupa "causion" hiyo ndogo katika trillion za uozo uliotanalaki katika jamii yetu ili ubongo wako usiuwekee wigo katika kutafakari.

Kungelikuwa na viongozi na serikali inayofuata sheria na haki, hao wahalifu waliomo ndani ya magamba ya nyadhifa na vyeo mbali mbali, wasingelithubutu kufanya wanayoyafanya hivi sasa kwa raia maskini!

Tushikamane kama Taifa bila kubaguana kielimu, kikanda, haiba ya mtu nk nk, maana kila eneo linaloitwa Taifa ama Nchi, lazima liwe na watu "kamchanganyikeni" , wenye elimu na wasio na elimu, wenye nacho na wasiokuwa nacho nk nk, lakini linapokuja suala la haki, basi matabaka yote ni kitu kimoja na hakuna lililopo juu ya sheria.
Nakuunga mkono asilimia mia moja
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu. Mungu Ibariki Tanzania 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Attachments

  • VID-20220912-WA0081.mp4
    8.4 MB
Hii stori Ina uongo Tena kutoka kwa mama mtu, RCO hawezi toa Hilo jibu hata Kama polisi wamemuua huyo mtoto
Poleni sana familia. Uchunguzi ufanyike ikiwa mtoto alichukuliwa mzima kifo lazma polisi wawajibike
 
Back
Top Bottom