Mtoto wa miaka 15 auawa na Jeshi la Police Mkoani Mwanza

Mtoto wa miaka 15 auawa na Jeshi la Police Mkoani Mwanza

Yawezekana dogo kuna siri kubwa au tukio kubwa alishuhudia kwa macho wakifanya police au kiongozi fulani mkubwa,so ili kuua soo ni kumzimisha dogo kabla hajaropoka,yangu ni hayo.RIP dogo langu

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app

Kuua ni kosa kisheria Ila ulichoeleza hakiwezi kuwa kweli/kuwa na mantiki.

Huyo Dogo lazima kuna kosa kafanya, au ni mhuni Fulani Kama panya road.
Ukitaka kuona Hilo angalia habari haijaeleza nini kilichopelekea Polisi wakaruka Nyumba elfu wakaenda kwenye Nyumba ya huyo Bibi kumkamata dogo wa miaka 15.

Habari imeacha maswali mengi Mno.

Hata hivyo waliofanya mauaji wachukuliwe hatua.
Ila Kama dogo ni Wale wa tabia za Panya road basi hiyo ndio dawa yao
 
Yani polisi walimchukua wakampeleka kwa wananchi, Na huyo mtoto alikua na kosa gani mbona maelezo hayajitoshelezi
 
Hii habari mi naona imeandikwa kishabiki ili kuwachafua police kwa sababu.
1.soma hapo marehemu akaja sa12 asubuhi akasema atafungua mlango huku kawekewa mitutu ya bunduki??????? Hapo kuna kitu.
2. Rco... hawezi kuwq namajibu ya hivyo , kalishwa maneno
3.kapelekwa mashiri kupigwa mawe na wananchi.
4.Bibi hataki kufungua mlango asikali hawezi sema tutapiga mrango mawe. Bola aseme tutavunja .

Saivi kuna kundi la panyq rod wanakimbilia mkoa nawengine wanaanzisha hayo makundi mikoani , nahuyo inaonekana kuanzia bibi na mjukuu niwazoefu , kwani si rahisi mwizi na mzazi wa mwizi kuomba apelekwe police , hawa walijua ushahidi haupo wakumfunga mtt.
Maoni yangu
 
View attachment 2354967Kijana Yahaya Aboubakar mwenye umri wa miaka 15 anadaiwa kukamatwa na askari polisi nyumbani kwa bibi yake mtaa wa Juhudi, Kata ya Mabatini wilaya ya Nyamagana Septemba 2, 2022, akiwa mzima, kisha polisi hao waliondoka nae na kumfungia ndani bibi yake Yahaya ambapo baada ya kufanikiwa kutoka ndani alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake katika vituo vya polisi na kumkosa.

"Wakasema wewe mama fungua nikawauliza nyie kina nani? mna kibali cha kuingia humu wakasema wao ni maaskari mbona hakuna mwenyekiti wala balozi wakasema ukigoma kufungua tunapiga mawe, baadae saa kumi na mbli marehemu akafika mjukuu wangu akawekewa mtutu huku na huku akaambiwa fungua mlango akafungua mlango wakamshika wakamuweka chini marehemu akalalamika akasema msinipige mimi sijabisha mnipeleke tu kama ni kituoni mimi nikamwambia mtoto huyo ni mgonjwa msimpige mpelekeni tu tutamfuatilia" ameeleza Bibi wa marehemu.

Mama mzazi wa Yahaya, Rehema Simba, amesema baada ya kuzunguka vituo vyote vya polisi kikiwemo kituo kikuu cha Nyamagana na kumkosa kijana wake ndipo akakutana na mkuu wa upelelezi akamwambia aende kwa RCO ili amueleze mtoto wake alipo.

"Baada ya kufika kwa RCO akasema shida nini nikamuelezea kwamba tumekuja ofisini kwako kuna kijana wangu amekamatwa tumeshazunguka vituo vyote vya polisi hatujampata akasema mtoto wako yupo Bugando Mochwari nikamuuliza mochwari amefuata nini? mbona mapolisi walimchukua nyumbani akiwa mzima? akaniambia kwamba baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa eneo la mashiri na kupigwa na wananchi ndipo akafariki," ameeleza mama wa marehemu.

Ramadhan Ng’anzi ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, amesema bado uchunguzi unafanyika wa tukio hilo na atakayebainika kuhusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo:- East Africa Radio
Hawa PT ni tatizo kubwa kwenye jamii
 
Ivi ukienda course ya polisi binadamu wenzako unawaona mbwa?
Ni bahati mbaya za kazini wakuu. Hata ungeenda wewe yamkini dogo kizazi jeuri akajibu hovyo . japo sisapoti kifo cha mtu yeyote ila tusubiri uchunguzi
 
Inawezekana kuna shida kwa huyo dogo hakuwa mtu wa kawaida police hadi wakutolee mitutu wew n dangerous kwanza had waje wote na mitutu n hatar
 
Huyo dogo hadi polisi wanamwendea na mitutu ujue hakuwa mtu wa kawaida

Polisi hawawezi kwenda hivyo kwa mtu wa kawaida

Huyo dogo alikuwa mtu hatari
Inaelekea pia raia walikuwa na hasira naye

Ova
 
Hii habari mi naona imeandikwa kishabiki ili kuwachafua police kwa sababu.
1.soma hapo marehemu akaja sa12 asubuhi akasema atafungua mlango huku kawekewa mitutu ya bunduki??????? Hapo kuna kitu.
2. Rco... hawezi kuwq namajibu ya hivyo , kalishwa maneno
3.kapelekwa mashiri kupigwa mawe na wananchi.
4.Bibi hataki kufungua mlango asikali hawezi sema tutapiga mrango mawe. Bola aseme tutavunja .

Saivi kuna kundi la panyq rod wanakimbilia mkoa nawengine wanaanzisha hayo makundi mikoani , nahuyo inaonekana kuanzia bibi na mjukuu niwazoefu , kwani si rahisi mwizi na mzazi wa mwizi kuomba apelekwe police , hawa walijua ushahidi haupo wakumfunga mtt.
Maoni yangu
nimekuelewa
 
Juzi juzi hapo kuna polisi alijinyonga nilifurahi sana
Ingependeza angenyongwa,

Jirani yetu ni polisi mume na mkewe wote,

Wanaishi na kijana wao ni lijizi yaani kitaata anaogopwa,alienda kuiba mtaa wa pili raia wakamkamata kumpeleka kituoni usiku,asubuhi ndugu zake wakamtoa eti kesi haina kithibitisho[emoji23]

Sasa sipiti picha huyu kijana angekuwa wa mtaani tu sijui kama angekuwa hai hadi leo.
 
Ataingia tu kwenye 18 za watu mitaa mingine

Ova
 
Huyo dogo hadi polisi wanamwendea na mitutu ujue hakuwa mtu wa kawaida

Polisi hawawezi kwenda hivyo kwa mtu wa kawaida

Huyo dogo alikuwa mtu hatari
Police gani? Hawa wetu hawa ambao ata ulinunua simu ya wizi wanakuja kwa mitutu!
 
Back
Top Bottom