Mtoto wa miaka 15 auawa na Jeshi la Police Mkoani Mwanza

Kwamba Polisi walimchukua wakampeleka mahali alikopigwa na wananchi akafa[emoji119][emoji119][emoji119]
Hatari na nusu, japo hawajaeleza alichukuliwa kwa tuhuma gani. Lakini all in all mtuhumiwa hatakiwi kuuwawa mikononi mwa polis
 
Yaani RCO aseme tuu mtoto wenu yuko mochwari!? Yaani kirahisi hivyo!?
Kuna kitu hakijakamilika kwenye hii habari

Haki ya uhai wa huyu mtoto itapatikana tuu

Lala salama mtoto, pole kwa familia na wote walioguswa na msiba
Haki ya huyo mtoto haiwezi kupatikana kamwe, ikiwa ile kesi ya kule mtwara ipo kimya sembuse hii?
 
Mama hapendi hayo mambo, akisikia hiyo atasikitika sana! Mama ni mpenda haki, mama anahuruma!
Naamini hili akilisikia atalifanyia kazi.
 
akasema mtoto wako yupo Bugando Mochwari nikamuuliza mochwari amefuata nini? mbona mapolisi walimchukua nyumbani akiwa mzima? akaniambia kwamba baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa eneo la mashiri na kupigwa na wananchi ndipo akafariki," ameeleza mama wa marehemu.[emoji3064]
 
Hata ukiomba uchunguzi ufanyike, kwa Afrika ni jambo lisilo na uhakika wa majibu yatayoondoa shaka...
 
View attachment 2354967Kijana Yahaya Aboubakar mwenye umri wa miaka 15 anadaiwa kukamatwa na askari polisi nyumbani kwa bibi yake mtaa wa Juhudi, Kata ya Mabatini wilaya ya Nyamagana Septemba 2, 2022, akiwa mzima, kisha polisi hao waliondoka nae na kumfungia ndani bibi yake Yahaya ambapo baada ya kufanikiwa kutoka ndani alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake katika vituo vya polisi na kumkosa.

"Wakasema wewe mama fungua nikawauliza nyie kina nani? mna kibali cha kuingia humu wakasema wao ni maaskari mbona hakuna mwenyekiti wala balozi wakasema ukigoma kufungua tunapiga mawe, baadae saa kumi na mbli marehemu akafika mjukuu wangu akawekewa mtutu huku na huku akaambiwa fungua mlango akafungua mlango wakamshika wakamuweka chini marehemu akalalamika akasema msinipige mimi sijabisha mnipeleke tu kama ni kituoni mimi nikamwambia mtoto huyo ni mgonjwa msimpige mpelekeni tu tutamfuatilia" ameeleza Bibi wa marehemu.

Mama mzazi wa Yahaya, Rehema Simba, amesema baada ya kuzunguka vituo vyote vya polisi kikiwemo kituo kikuu cha Nyamagana na kumkosa kijana wake ndipo akakutana na mkuu wa upelelezi akamwambia aende kwa RCO ili amueleze mtoto wake alipo.

"Baada ya kufika kwa RCO akasema shida nini nikamuelezea kwamba tumekuja ofisini kwako kuna kijana wangu amekamatwa tumeshazunguka vituo vyote vya polisi hatujampata akasema mtoto wako yupo Bugando Mochwari nikamuuliza mochwari amefuata nini? mbona mapolisi walimchukua nyumbani akiwa mzima? akaniambia kwamba baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa eneo la mashiri na kupigwa na wananchi ndipo akafariki," ameeleza mama wa marehemu.

Ramadhan Ng’anzi ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, amesema bado uchunguzi unafanyika wa tukio hilo na atakayebainika kuhusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo:- East Africa Radio
Ukisoma ilivyoandikwa unaweza ukawahurumia. Ila kama umeishi mwanza utawaelewa polisi. Huto tu Toto ni zaidi ya panya wa dar. AF hao mabibi na wazazi ndio wanufaika. Yaani huyo dogo ni kama walimchelewesha.
 
RCO anyooshe maelezo...
 
Jeshi Hili Lichunguzwe Matukio Yamezidi Sana
 
Ukisoma ilivyoandikwa unaweza ukawahurumia. Ila kama umeishi mwanza utawaelewa polisi. Huto tu Toto ni zaidi ya panya wa dar. AF hao mabibi na wazazi ndio wanufaika. Yaani huyo dogo ni kama walimchelewesha.
Kwa hivyo Mahakama imetoa hukumu kuwa wakikamatwa wapelekwe kwa wananchi wakawaue?

Acha ujinga. Mtuhumiwa amekamatwa mzima, sasa alipelekwa kwa wananchi kwa minajili gani?
 
Haya yalitokea awamu ya IGP aliyepita,tuone IGP mpya atalichukuliaje suala hili,akikaa kimya basi tujue tu kuwa huu ndo utamaduni wa jeshi la polisi kwa raia.
 
Shida sio division 0.viongozi wao wanawalinda,na kulindana
Duh mtiririko wa habari haueleweki- lkn Sasa kwa haya mauaji ya polisi yalivyokithiri ni vyema kuwepo na kitengo cha internal affairs ambacho kitadeal na askari wakiukaji wa maadili na wavunja Sheria.

Hawa Division O wamezidi kujichukulia hatua mikononi kinyume cha sheria
 
Ukisoma ilivyoandikwa unaweza ukawahurumia. Ila kama umeishi mwanza utawaelewa polisi. Huto tu Toto ni zaidi ya panya wa dar. AF hao mabibi na wazazi ndio wanufaika. Yaani huyo dogo ni kama walimchelewesha.
Kweli! Ungelidadavua kidogo ututoe tongotongo machoni mkuu!
 
Hata Kama ndio wamuue? Eti mtu asikamatwe hadi upelelezi ukamilike Polisi Mungu anawaona, shame
Nchi zilizoendelea ndiyo huwa wanafanya hivyo. Kama hawana ushahidi wa kutosha wa kukutia hatiani wakienda mahakamani watakuchunguza na kutafuta evidence hata kama itachukua miaka miwili. Hakuna kuwekana tu mahabusu bila kupelekwa mahakamani na bila kuwa na ushahidi wa kutosha.
 
Back
Top Bottom