Mtoto wa miaka 15 auawa na Jeshi la Police Mkoani Mwanza

Kwa hivyo Mahakama imetoa hukumu kuwa wakikamatwa wapelekwe kwa wananchi wakawaue?

Acha ujinga. Mtuhumiwa amekamatwa mzima, sasa alipelekwa kwa wananchi kwa minajili gani?
Huna unachojua. Tulia usidiwe
 
Inasikitisha
Sanaaaaa.. Yaani hili jeshi kama hakutakuwa na chombo cha kuliwajibisha tabu iko pale pale... Lazima kuwe na chombo cha kuhakiki utendaji kazi wake kwa kweli.
 
RCO anajibu kirahisi tuu km aliyekufa ni mbwa hana nidhamu mxiiiu zake.
Kwa sababu hakuna popote pale anaweza kuwa answerable labda itokee imeundwa tume au mamlaka ya nchi iingilie kati kama wale polisi wa kule Mtwara..
 
Hii stori Ina uongo Tena kutoka kwa mama mtu, RCO hawezi toa Hilo jibu hata Kama polisi wamemuua huyo mtoto
Poleni sana familia. Uchunguzi ufanyike ikiwa mtoto alichukuliwa mzima kifo lazma polisi wawajibike
Unless uwe unaujua ukweli otherwise unaanzia wapi kuhitimisha kwamba ni uongo? Huyo RCO hawezi kutoa jibu hilo kwa sababu gani?? Tumeona kwenye kesi ya Mbowe walivyokuwa wanatoa majibu ya ajabu hata kushinda hilo..
 
mbona mapolisi walimchukua nyumbani akiwa mzima? akaniambia kwamba baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa eneo la mashiri na kupigwa na wananchi ndipo akafariki,"
Kazi ya polisi ni kuwapelekea wananchi mtu apigwe!! Hii mpya
 
Ipo siku raia watamchoka
 
Mbowe atasema ni magufuli kaua
 
Kwa sababu hakuna popote pale anaweza kuwa answerable labda itokee imeundwa tume au mamlaka ya nchi iingilie kati kama wale polisi wa kule Mtwara..
Kwa waziri hawawe
Kwa sababu hakuna popote pale anaweza kuwa answerable labda itokee imeundwa tume au mamlaka ya nchi iingilie kati kama wale polisi wa kule Mtwara..
Mmh kwa IGP, kwa waziri, kwa rais, hawa woote ni wakubwa zake ujue
 
Ndio shida ya kuchukua failures, div 0 kuongoza taasisi nyeti na kubwa kiasi hiki.
 
Haki ya huyo mtoto haiwezi kupatikana kamwe, ikiwa ile kesi ya kule mtwara ipo kimya sembuse hii?

Unaposema haki haiwezi kupatikana inategemea unamtegemea nani au nini kuipata
Ila tambua haki ya uhai wa mtu kamwe haidhulumiki
 
Ingekua Nchi wanazojitambua huyo aliejibu kuwa wakamchukue motuary angekua ndani muda huu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…