Mtoto wa mkeo asipokupenda unafanyaje?

tafuta michezo wanayopenda watoto na unaohisi ataupenda alafu ufanye peke ako akiwa anakuona bila kumuita.... Kama ni cartoon unaangalia cartoon huku unafurahia baada ya mda atakuja toys nyingine unazitumia wewe mwenyewe kwa kuimagine kama unaongea and the likes....pia kumpeleka sehem zaivhezo ya watoto will help
 
Inaonekana baba yake mzazi alikuwa anamjali sana na kumlea vizuri
Sasa anaona wewe unalazimisha kuingia sehemu ya baba yake
Kumbuka miaka 4 anaelewa vizuri kinachoendelea
Kuwa mpole na usimuite baba kwani anajua baba ni nani
Ni vizuri kama baba yake yupo ungemshawishi mkeo jamaa awe anakuja kumchukua mara moja moja

Kama hajulikani ni tatizo lingine
Ila kama yupo na uliamua kuoa single mother basi itabidi uvumilie mengi
 
Nilijaribu kumuuliza mwanamke kuhusu malezi ya baba yake akasema ya kawaida sana, jamaa aje amchukue si ndio maana yake akae naye tu maana ndiye anaye mtambua na mama yake hataki mtoto wake aende kwa yule baba.
 
Hii maneno ya masingo maza tulishakubaliana kwamba hakuna kuoa. Sasa huyu apambane na hali yake. Sisi tupo bize kuvaa barakoa maana hii corona mpya upimaji wake hatuupendi kabisa. 😂😂😂
Kusema ukweli kuoa ma single mother kuna changamoto yeye anataka umpende mwanaye mwanaye hakupendi mama anajaribu kulazimisha ili asimtie aibu maana alimtetea kuja kukaa na ww lakini mtoto hana mood kabisa. ngumu sana
 
Duh! Basi mtoto atakuwa ameisoma HATARI KUBWA SANA huko mbeleni magunia mawili ya mkaa n.k, ujue watoto wadogo ni kama malaika. Mkuu, wewe utakuwa ni mtu hatari sana.
 
upo na mama yake mwaka wa 2 sasa maana ulimchukua akiwa na mwaka 1, tazoeaje mfano

Kama usemacho hapa ni ukweli, basi shida ipo sana upande wako na au mkeo na Wala siyo mtoto.

Jichunguze na ujirekebishe.

Haswa ukaribu wako na familia ninahisi haupo vizuri.

Ukute unaamka akiwa kalala, na unarudi unakuta kalala kila siku.

Hapo lazima yatokee hayo unayoyalalamikia
 
Duh! Basi mtoto atakuwa ameisoma HATARI KUBWA SANA huko mbeleni magunia mawili ya mkaa n.k, ujue watoto wadogo ni kama malaika. Mkuu, wewe utakuwa ni mtu hatari sana.
😂😂
 

Na siku akija home kumchukua mtoto akikuta haupo awe anakumbushia kula tunda.
 
Wewe sepa zako,jifanye nawe ndgu wa nyange
 
Sio hadi mama akutengenezee connection.
Unaweza kungeneza mwenyewe na kila kitu kikakaa sawa.

Next level: ni kutumia hekima na akili za Mungu kuweka mambo level.
 
Nilijaribu kumuuliza mwanamke kuhusu malezi ya baba yake akasema ya kawaida sana, jamaa aje amchukue si ndio maana yake akae naye tu maana ndiye anaye mtambua na mama yake hataki mtoto wake aende kwa yule baba.

Mtoto lazima amuone baba yake msimnyime haki yake maana atakuja kukuchukia kama yule msanii
Jenga urafiki na ex wake man to man ili umsaidie mtoto kuliko kumuacha aumie hivyo
Ubaya utakurudia na bado una nafasi kama mlezi
Chukua maamuzi ya kiume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…