Mtoto wa mkeo asipokupenda unafanyaje?

Mtoto wa mkeo asipokupenda unafanyaje?

Unasubiri nini kumfungia nje? Mwambie asikuletee kiburi sababu utamnyoa kwa kigae tena umwambie mbele ya mama yake usiku huku ukimvuta nje wakati mvua inanyesha. Uone kama hasemi nisamehe baba. Kisha mwambie futa machozi haraka sana na nisikie kelele.

Then akinyamaza unampa adhabu ya kuamka mapema apanguse viatu vyako kabla ya shule.

Uone kama atajaribu kuuliza tena huyu ni nani. Avae kanga ya mama yako ndo baba yako mwambie.
 
Mapenzi hayalazimishwi!!

Tatizo mnamlazimisha huyo mtoto kukupenda badala ya kumpa nafasi ya yeye kukupenda mwenyewe naturally. Sijui kwanini ila nahisi kama wewe (or who ever that is) mlikuwa na haraka sana ya kutambulishana kwa mtoto. Mlipaswa kuacha mahuasiano yenu kuwa yenu kwanza, wakati unaanzisha urafiki na mtoto bila pressure yoyote mpaka hapo baadae.

Kama mko serious na mahusiano yenu kweli, cha msingi acheni kum-force huyo mtoto kukupenda/kukukubali mara moja. Na wala usijipendekeze nae sana. Just be there as a friend & a father figure. Akionyesha kukuhitaji kwa lolote sawa, asipoonyesha pia sawa....mwishowe atakuzoea na bond itaanzia hapo. Huyo mtoto bado mdogo sana....angekuwa mkubwa ndio ingekuwa changamoto.

Swali la kizushi.....
Usikute una nia mbaya nao na mtoto can sense that alafu unatuchosha na ushauri? 😬😬
uko sahihi, waliwahi kudandiana na kumilikisha mahaba.....walisahau kwamba walipaswa kuwa na muda wa kutosha ili huyo mtoto aanze kumzoea anko kwa style ya come visit and go.......ili huyo mtoto akupende slowly slowly,,,, na mama mtoto awe akiongea nae bila jazba wala ulazima, but kama mama......kwa kifupi wameharakisha habari.........hapo kazi unayo blaza..
 
Upo na mama yake mwaka wa 2 sasa maana ulimchukua akiwa na mwaka 1, tazoeaje mfano

Kama alikuwa na mwaka mmoja kayajuaje hayo! Jibu ni ANAFUNDISHWA.

Usilazimishe kupendwa, ilimradi mama’ke anajua tatizo sio wewe hawezi kukulaumu (make hofu yako ni sharti kumkubali mtoto).... basi usitumie nguvu fanya mambo yako atajileta akitaka.

Watoto (watu wengi) wana kawaida ya kuchukua faida kwa kile wakiona ni kama udhaifu kwako.

Halafu mbona umeishia tu kusema mama hana wazazi, gusia kuhusu baba wa mtoto... ndo option sahihi ikifikia hatua ya kumwondoa hapo huyo mtoto.
 
tafuta michezo wanayopenda watoto na unaohisi ataupenda alafu ufanye peke ako akiwa anakuona bila kumuita.... Kama ni cartoon unaangalia cartoon huku unafurahia baada ya mda atakuja toys nyingine unazitumia wewe mwenyewe kwa kuimagine kama unaongea and the likes....pia kumpeleka sehem zaivhezo ya watoto will help

Aisee mna kazi, yote hayo ili tu kumrubuni mtoto wa watu!!
 
Imetokea na huwa inatokea mtoto wa mkeo hakupendi. Umeamua kuishi au kuoa mke ambaye hana kazi ana mtoto mmoja wa kike au wa kiume mwenye umri wa miaka 4 sasa mkeo anajaribu kumwambia mtoto kuwa wewe ndiye baba yake au baba wa kambo mtoto hataki na ukijaribu kuwa karibu na yeye hakubali, unamletea juice, pipi, biscuit mara kwa mara kama zawadi hataki, siku moja mkiwa wawili wewe na mkeo mama anamuuliza mbele yako huyu nani anasema hajui.

Wenye uzoefu na haya mambo unafanyaje, kwanza mama hajisikii vizuri mtoto kutokuwa karibu na wewe na hataki kukusogelea ukizingatia kuwa mkeo alikwambia kuishi na mimi lazima umkubali mwanaye. Zingatia kwamba mkeo hana tena wazazi kwamba angempeleka mtoto kwa bibi yake.

Tunafanyaje kwa mfano huu.
Hilo ndio tatizo sugu kwenye aina hiyo ya mahusiano,ni vizuri mama kama ana akili amtengenezee mtoto mazingira ili akukubali lakini kwa kutumia vijuice na soda hivyo mkuu utaliwa sana hela zako na hakuna utakachofanikiwa,shida hapo ni huyo mwanamke sio mtoto...
 
Mzee au ulitaka kumfanya vibaya... sio rahisi saja mtoto kukuchukia mazima..

Jipe muda,, then mtaelewana sana na mtakuwa na bond nzuri mnoooo..

In every reaction there is an.....
 
Achana nae endelea na yako,akiamua atakupenda Kama hataki mpoyezee tu
 
NI UTOTO UNAMSUMBUA ataacha akikua.........endelea kum care. ...ingawa anaonekana ana kiburi cha kichaw......

Anyway

MWANAMKE WA KUOLEWA AWE.....BIKRA TU ...
Huyo bikra utamuumba mwenyewe?
 
Mama kumuelekeza mtoto akuamkie sio kosa na sio ku force, mama kumwambia mtoto huyo ndio baba yako ili akitaka kufanya kitu ajue huyo ndiye baba sio kosa, mwanaume hata muda wa kutaka kuongea na mtoto ila kama mtoto wake akitoka kazini au sehem anakuja na zawadi bado mtoto hataki hizo zawadi. Nia mbaya kwa huyo mtoto ni kama ipi mfano maana hakuna mpango wa kumuumiza au kumfanyia mtoto kitu kibaya.
Kwanini mama anamwambia mtoto kuwa wewe ni baba yake wakati siyo?!

Mtoto ana akili huyo......anajua baba yake halisi ni yupi
 
Acha ufala, nilishasema mechi lazima ianze moja moja au hom iwin sasa wewe umekengeuka.
 
Mkuu funguka kutoka moyoni mwako,inaonesha una upendo wa kinafiki kwa mtoto,asiporuhu moyo wako kumpenda huyo mtoto na kumchukulia kama mwanao kutoka sakafu ya moyo wako kamwe mtoto hatakupenda hata kidogo,watoto ni wepesi sana wa kusoma hisia za watu .

Mfano Mimi juzi nilisafiri kwenda kwa jamaa Yangu ,nilipofika kwa mwenyeji wangu nikiwa na dreva wa bodaboda nilikuta familia ile ina watoto wa kati ya miaka mitatu hadi mitano wako kama watano,baada ya kufika na kupewa viti ,watoto wale walikuja kutulaki ,kutokana na kuchoka na jinsi walivyochafuka sikutaka watoto wale wanisogelee,hizi hisia zilitoka moyoni(nilichukizwa na kitendo cha watoto kutaka kuja kuning'inia miguuni pangu),na kweli watoto hawakunisogelea japo sikuonesha hisia zozote usoni pangu Bali moyoni,watoto wale walienda kwa dereva wa bodaboda na kuanza kumuomba pipi na kuninginia miguuni pake huku Mimi wakiniogopa,maana tayari nilikuwa nimeonesha chuki/kutokutaka kusogelewa na watoto wale.

So, ninachokiona kwako mkuu unaupendo wa kuigiza kwa huyo mtoto na ndio maana umeanza kumuwazia mambo mabaya mtoto wa miaka minne kuwa hakupendi,lakini ukweli ni kuwa wewe ndo haumpendi,jaribu kuondoa kinyongo ndani ya moyo wako hakika huyo mtoto atakupenda na kukuthamini.

Tambua kuwa kuna baadhi ya watoto wamejaliwa uwezo wa kusoma hisia zetu na hicho kinachokukuta ni kutoka na na tabia yako ya kuonesha upendo wa uongo.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Ni bora huyo anayeonesha makucha yake mapema kuliko yule mtoto nasibu nyange.... loh aiseeee
 
Back
Top Bottom