Mtoto wa mkubwa yupi anaendesha bodaboda? CCM acheni hadaa

Mtoto wa mkubwa yupi anaendesha bodaboda? CCM acheni hadaa

Mimi kwa hili natofautiana na Lema aisee.
Mkuu huyu LEMA ni form 4 failure ,usafri wa boda boda upo dunia nzima haswa nchi zinazoendelea ,leo anakuja kulisha tongo pori wanachi wanaojitafutia riziki halali
 
Nina wasiwasi na akili za wana - CDM yaani mnataka kazi na maisha ya mtoto wa mkubwa yafanane na haya yetu?

Acheni utani basi
Hiki chama kimefanikiwa saana kuandaa vijana wajinga aisee hadi wanatia huruma ,ukimuuliza LEMA hawa vijana waliojiajiri anaweza kuwapa ajira sidhani kama anaweza kuwa na jibu
 
Viongozi wa CCM acheni kuwadanganya vijana wetu kuwa kuendesha bodaboda ni kazi kama kazi nyingine.

Mbona watoto wenu haweendeshi bodaboda?

Kiongozi yupi ambaye mwanaye ni dereva bodaboda?

Kama hakuna basi mfahamu kuwa hiyo siyo kazi ya heshima. Ni laana.
Embu tuanzia kwa watoto wa Lissu,Mbowe na Lema mwenyewe na utuletee majibu hapa
 
Kiongozi wa hivyo hatakuwa na exposure, hivyo atajiendeshea nchi kama fulani mwisho wa siku tutapata tabu tu na mateso.

Haitakiwi kamwe mtu wa hivyo kutawala taifa.
Tangu tupate uhuru inchi inaendeshwa na watoto wa wakulima, wachunga n'gombe, wakimbizi nk , ndio iwe bodaboda?
 
Uimbaji na uigizaji Kolimba na mwanae kotide, Vick nk, je udereva wa nini maana hata boda ni udereva ola kama ni kuendesha ma v 8 wapo wengi na viongozi wenyewe ni madereva.
Udereva kama wa uber au kuwaendesha viongozi.
 
Kwa nini ajali hizi nyingi ziwe kwao bodaboda tu na siyo aina nyingine za udereva? Ok ngoja nilipe sababu maana wewe unakwepa kujichoma kisu labda ni sehemu ya tatizo,


Bodaboda walio wengi hawana mafunzo ya kuendesha bodaboda na hata wengi hawana leseni.
Sasa hapo ndio useme wenyewe hawaipendi hiyo kazi kwa sababu hawana mafunzo ya kuendesha pikipiki hivyo wanapata ajali? Ndio maana nikakwambia kuwa hizo ajali asilimia kubwa husababishwa na wao wenyewe kutokana na aina ya uendeshaji wao.
 
Ni fujo na vurugu tu. Hawafuati sheria wala kanuni za barabarani. Wanaendesha kushoto kulia kati kati na hata hawaheshimu mataa. Polisi trafiki wanawaangalia tu hata wakipakia mishikaki na wasipovaa kofia ngumu hawajali
 
Namlaum Sana vikali caliyeruhusu bodaboda
Mwakyembe akiwa waziri wa uchukuzi 2010 ndiyo alipeleka muswada bungeni wa kuhalalisha bodaboda kuwa chombo cha usafiri wa umma.
 
ukimuuliza LEMA hawa vijana waliojiajiri anaweza kuwapa ajira sidhani kama anaweza kuwa na jibu
Kwahiyo kazi ya bodaboda unaichukulia kama ndiyo mafanikio ya ccm ktk kutoa ajira kwa vijana?

Uwezo wako wa kufikiri mdogo Sana kama uduvi.
 
Embu tuanzia kwa watoto wa Lissu,Mbowe na Lema mwenyewe na utuletee majibu hapa
Hawa hawawezi kuwaruhusu watoto wao wawe bodaboda kwasbb washakuambia kuwa hiyo ni laana.

Lkn ninyi mnawahadaa watoto wa walalahoi kwamba bodaboda ni kazi
 
Hadi sasa hakuna aliyeweza kueleza akaeleweka kwanini bodaboda iwe laana? Kila mmoja anaeleza lake tu.
 
Kwahiyo ukahaba na wizi ni kazi ila bodaboda ndio sio kazi?
Wewe ndiye hauelewi, hizo ni kazi ila zina laana ndani yake kutokana na madhara kwa jamii yatokanayo na kazi hiyo. Ndiyo maana umeambiwa kama ni riziki tu hata hizo kazi zina riziki nzuri tu ndani yake iko laana kama tumavyoona madhara ya bodaboda.
 
Wewe ndiye hauelewi, hizo ni kazi ila zina laana ndani yake kutokana na madhara kwa jamii yatokanayo na kazi hiyo. Ndiyo maana umeambiwa kama ni riziki tu hata hizo kazi zina riziki nzuri tu ndani yake iko laana kama tumavyoona madhara ya bodaboda.
Ndio maana nasema hamueleweki, wengine mnasema bodaboda si kazi ni kitu ambacho watu hufanya kujishikiza tu baada ya kukosa kazi ndio maana hakuna mtoto wa kiongozi ambaye ni bodaboda.

wengine mnaona bodaboda ni kazi ila isiyo na heshima na yenye mapato kiduchu.

Wewe unasema bodaboda ni kazi ila ina laana kutokana na madhara yake kwenye jamii na kuifananisha na ujambazi na umalaya.
 
Tunazungumzia maisha bora mkuu kuajiriwa na kadhalika, nini sustainability ya Bodaboda, ukiambia elezea miaka 30 ijauo boda boda hao watakuwaje utaelezea vipi?
Wengi wao hawakatizi miaka 10
 
Boda boda ndiyo ajira ambayo imeua watu wengi
Imesababisha vilema vingi
 
Back
Top Bottom