Mtoto wa ndugu yangu kakoswa koswa kutekwa na watekaji wa watoto

Mtoto wa ndugu yangu kakoswa koswa kutekwa na watekaji wa watoto

Hapa tunajadili utekaji sio malezi, hayo malezi hayahusiani na utekaji.!!
Kutekwa hata mtu mzima anatekwa.
Ni kweli kabisa tena wengi tu
Tuwatahadharishe tu
Yaani huyo mtoto jamaa aliesema aliitwa kwa pipi bila kukataa angetekwa nae

Ndio nikasema watoto wanafundishwa kutokuongea na strangers
Ni onyo tu kwa watoto
Hawatekwi kama wakubwa bali wanawarubuni hata kwa hela
Nimekuelewa na tuombe tu sana maana yanatokea siku hizi
 
2025 inakaribia

Kuweni makini na haya mambo
Watoto
Wazee wako (vikongwe)
Jiepushe na kunywa Sana pombe

Siasa sio kitu kizuri
 
Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa njiro Arusha, ktk ki grocery njee kuliwa na vitoto vya kike vinacheza pembeni yupo mlevi hawa wa banana

mara kutoka nje naona kapakata katoto kadogo umri wa miaka 4-5 mkono ndani ya chupi ya mtoto daaaah...
Nilichukua hatua..
Hili tukio silisahaugi
Duh inamana uyo muhuni alikuwa anapima oil kwa katoto kadogo pia isitoshe nia yake alitaka kukabaka kama sikosei aisee sio powa ukatili wa kingono upo sana kwa watoto
 
Mkuu hamuoni watu wasio waswahili watoto wao hawaonekani wakicheza hovyo nje?
Tunasema ni wabaguzi kumbe wao ndio wako sahihi kila wakati
Wangewaacha mngeona damu changanyikeni kila mahali

Tuwafunze maadili watoto la sivyo mtaendelea kuona mtoto wa miaka 12 yuko na jamaa gesti
Kabisa mkuu kuna jambo la kujifunza hapa, muda mwingine tunasema watoto wa mageti kali wanaringa sana kumbe wapo sahihi, mitoto ya uswazi yani ni kujichanganya tu mwisho wa siku ustawi wa mtoto kimaadili ni ziro kabisa
 
Back
Top Bottom