Mtoto wa Rais Samia (Wanu): Sitamani Kuonekana Mtoto wa Rais Nikiingia Mahali/Naumia Mzazi Akitukanwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Kuna mahali naingia nafanya kazi zangu naondoka bila Watu kujua kama nilikuwa pale, lakini unapokwenda kwenye shughuli za kijamii hasa harusi kuna Watu lazima wanitambulishe kama mtoto wa Rais, ile huwa inanifanya nisiwe huru katika mazingira yale" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge na Mwenyekiti wa MIF

“Inaumiza kama mtoto kuona mzazi anarushiwa maneno mitandaoni na katika kipindi ambacho muda wake wote amewekeza kwa Taifa, muda mwingi anakuwa mbali na familia, lakini ni Mtu imara sana namfahamu hajawahi kutetereka kwenye hilo” - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge na Mwenyekiti wa MIF

"Moja kati ya changamoto kubwa ninayokutana nayo katika uongozi wangu ni wananchi wangu pamoja na Watu wengine kuhisi naweza kufanya kila kitu kwa kigezo kwamba ni mtoto wa Rais, sio kweli kwamba naweza kufanya kila kitu na kuna wakati nazidiwa" - Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Mbunge na Mwenyekiti wa MIF

 
bado hajasema, matusi ya kuanzia november 2024 hadi november 2025 atajinyonga kabisa. Amwambie mama yake atangaze mapema kuwa hana nia kugombea urais 2025 hapo atasalimika kiasi fulani, tofauti na hapo watamtambua kama mama yake ana tamaa sana...kapewa akaimu miaka 4 tu tayari amenogewa anataka na anaona anaweza kumbe embe la kupewa si sawa na la kununua.
 
imagine yeye ni mbunge na licheo lingine na bado mama yake ndio slave masta wetu halafu analialia, ila kuna watu hawana mbele wala nyuma na wazaz wao wanahamishwa kinguvu na polis wenye marungu na mabunduki kutoka kwenye makaz ya asili anadhan watamsifia bimdashi wake aache utoto
 
Mjulishe mam !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…