Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mtoto wa Rais Faustin-Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Evariste Touadera amezusha gumzo kubwa baada ya video inayomuonesha akiwazaba makofi wazungu kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.Inaelezwa kwamba tukio hilo limetokea katika Mji wa Kislovodsk, Kusini mwa Urusi ambako alipelekwa kwa ajili ya matibabu ya uraibu wa dawa za kulevya.
Evariste alipelekwa nchini Urusi kwa matibabu, baada ya athari za madawa ya kulevya kuonesha kumvuruga akili yake, kiasi cha kuwa anafanya matukio mengi ya ajabu.
Hata hivyo, akiwa nchini Urusi, alijaribu kutoroka akidai anakosa uhuru wa 'kula bata' na marafiki zake, katika harakati za kumtafuta ndipo alipokutwa na mabegi yake kisha akaanzisha ugomvi.
Imeelezwa kwamba, miongoni mwa waliopigwa, ni daktari wa saikolojia, Zarina ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakimhudumia.
Licha ya songombingo hilo, Evariste alisafirishwa salama mpaka jijini Moscow, Urusi na kukabidhiwa kwenye ubalozi wa nchi yake jijini humo.
Waliopigwa katika sakata hilo, inaelezwa kwamba hawana nia ya kumfungulia mashtaka.