Mtoto wa Zachary Kakobe: Mfikishieni salamu baba yangu namtafuta, sijaonana naye kwa Miaka 20, nikienda Kanisani sipati nafasi ya kumuona

Miaka 43 mbona amekomaa hivyo Kama ana miaka 60! Inaonekana anateseka sana wakati baba yake ni bilionea! Kakobe aache kunyanyasa watoto kwa kujifanya Mungu mtu.. yaani mtoto wako mwenyewe akija nyumbani hawezi kuingia mpaka aandike barua! Hatari sana
 
Hapa kuna mambo ya kujifunza passively:

Kulingana na yatokanayo.

1: Watoto kulelewa na wazazi/jamiii kwa kadri ya maadili mema.

2: Watoto kufuata maadili kwa kadri ya maelekezo ya wazazi na jamii.

3: Watoto wanapoamua kukisanua na kufuata yao, wahakikishe wanamaanisha. Usisuburi baadae huruma ya jamii na maandiko.

Maana kuna wakati ujuaji wa mtoto unaweza kumpa uchizi mpaka kifo mzazi/wazazi au watoto kuifanya safari ya mwisho ya mzazi.

NB: Yaliyoko kati yao wayajua wenyewe na baba yao wa sirini. Kama yaweza kusameheka au la ni jukumu lao. Usiubebe mzigo unaokuzalishia zambi zaidi.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa hata wewe umekaza pumb* ukaachana na bababyako?

Kama baba yupo hai, kwa nini asimtafute?

Hataki kulelewa maana amesema alishalelewa naye bali anataka kuzungumza naye. Hofu yenu ni kuwa atadai mali
Mm sio kukaza pumbu tu hadi dushe that's why sitegemei mtu chini ya jua zaidi ya Mungu pekee ili kuweza kuishi.
Mm ni mstaafu sasa nakula pensheni tu + stahiki zangu.
Huyo anamtafuta baba yake ili aweze kuishi imagine kama angekuwa anamtafuta baba yake just kumsalimia tu na amehangaika mara zaidi ya mamia kwanini asiachane naye?
Huyo anataka Kitonga toka kwa baba yake trust me..))))
 
Hesabu zinagoma! Miaka 43 ina maana kazaliwa 1980, kaanza standard One akiwa na Miaka sita? Kwa miaka ile ilikua ngumu
 
Wako wengi aende Same atawakuta ndugu zake
 
Kumbe Ni wa kwakwe

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama una maisha yako na hakutaki kwanini umtafute?

Pili yaani baba yako na mama yako akukatae? Labda ni mtoto wa nnje mama kakobe anakaza

Apambane na maisha tu amuombe Mungu amsaidie apate fedha aache mambo ya kujikomba
 
Kwa nini unasema hivyo? Inawezekana matatizo tu ndio yanamfanya mtoto aonekane mzee zaidi
Nadhani Pombe ndo zimeleta athari lakini I hope atasaidiwa na mzee wake Pombe sio nzuri Sana kwa wanaume.
 
Miaka 43 anamwonyesha njia gani jitu zima hilo

Limtafute mzee kwa adabu tena za hali juu likiwa limeacha tabia zote mbovu lisije mdhuru Mzee Kakobe


Liandike tu linaishi wapi Mzee Kakobe atakuja kulifuata huko siku akijisikia lakini sio kwenda kumsumbua Kanisani au nyumbani na kwenda vyombo vya habari

Hana adabu
 
Njia anayotumia si sahihi anamnyanyapaa baba yake Mzee Kakobe
 
Usipotoshe maandiko kwa Issue ya mtoto wa Kakobe

Mwana mpotevu alienda kwa baba yake nyumbani tena akiwa na akili timamu huyo anasema amekuwa akienda hadi kanisani akiwa kalewa njwiii kutaka kuonana na baba yake kanisani anataka nini? Kwenda kalewa kanisani ambako baba yake anahudumu ? Kumwaibisha au kumharibu kisaikolojia apate presha are madhabahuni aanze ugomvi wa mirathi au nini? Lengo la kwenda kalewa kanisani kama sio kuharibu huduma ya baba yake mzazi ni nini?

Kwa hili nadimama na Kakobe mtoto alichofanya school na sio mtoto ana miaka 43 na ana watoto na kasema uchumi wake umeyumba kwa hiyo anataka Mzee Kakobe ampe sadaka za kanisani kwa nguvu na shinikizo?

Anachofanya ni kitendo cha unyasasaji wazee next time akifika akamatwe apelekwe polisi Mzazi akigoma kukuona ukiwa na miaka 43 sio kesi hutakiwi ku.force uhusiano

Baba kasema sikutaki to hell kila mtu aendelee na maisha yake


Wanasheria kanisani akija hapo.kanisani mpelekeni polisi awekwe ndani na mburuzeni mahakamani kwa kufanya fujo kanisani na kunyanyasa mzazi wake

Hata kama Mzee Kakobe hataki mpelekeni Polisi na mahakamani
 
Pombe ni nzuri ila ni mbaya kama ukiinywa ili ikuondolee mawazo .

Frank ni kijana wake kakobe hii ni kwa mujibu wa maneno yake yeye tulipokuwa tunakunywa gambe bukoba miaka ya tisini na kitu .

Ilikuwa ni ziara ya mzee wake huko kagera kulifungua kanisa la Full gospel lililopo pale Hamugembe miaka hiyo ndiyo nikiwa bar fulani nikapata kujuana na kijana na kunieleza kuwa ni mtoto wa Kakobe na pia amekuja kwenye uzinduzi wa hilo kanisa kipindi iko mimi nikiwa kwenye shughuli zangu .

Tukapoteana na kijana nikaja kumuona tena Dodoma mwaka 2014 akiwa ni mtangazaji katika kituo cha redio fulani .

Tukapata wasaa wa kunywa kama kawaida ila hakuwa kachoka kama nionavyo leo, ila baada ya pale sijaonana naye tena wala sikuwa na mawasiliano naye sababu sikuwa na kazi wala bond na yeye kwa lolote zaidi ya kulewa .

Ni hapo nilijua kuwa kweli kuwa mtoto wa mtumishi sio kuwa mtakatifu .

Ila kwa kawaida nahisi ni mwanaye kweli japo watakuwa walitibuana na mzee wake .

Kakobe mpokee mwanao wenzako wanatafuta watoto hawapati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…