Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wajukuu wanamtaka Babu hilo unasemajeHaikubaliki
Miaka 43 no please sio miaka ya kugombea cha mzazi anatakiwa awe alishapata chake kwa kuhangaikia maisha kivyake
Umri unakataa hata aende mahakamani
Hata mahakama itamshangaa
Lina miaka 43 bado toto hilo? Liende huko lisisumbue Mzee Kakobe tena likome
Angekuwa basi hata anampigia simu.Wana umri gani kuna umri mtoto hatakiwi nyumbani
Makabila kibao mfano kwa wakurya miaka kumi na tano tu lazima mtoto wa kiume ajitegemee na awe kwake
Sio hao tu yako mengi tu mtoto wa kiume zaidi ya miaka 18 hatakiwi kula hata nyumbani kwa mzazi anakuwa na kashamba kake na kajumba kake ka majani
Jitu zima miaka 43 linataka kuonana na baba yake na kwenda nyumbani kuhitaji msaada no please
Kakobe kazaliwa vijijini yuko sahihi
Mtoto miaka 43 hapana
Baba akisema usije kwangu baki tu kuwasiliana naye kwa simu tu usikanyage ofisini kwake wala nyumbani kwake kama hataki
Una agenda gani kukomaa kuwa lazima muonane uso kwa uso wakati simu zipo na namba unazo ? Si ukororofi huo
[emoji28][emoji28]Je inawezekana mtoto akamzidi umri Mzazi?
pale karibu na rainbowKakobe ana kaa Mbezi Beach
Kwenye nyumba kubwa
Kama sikosei mtaa wa Tembo
Hata akifika hapo majirani watamwonyesha
Miaka 43????Katika pitapita zangu mitandaoni, nimekutana na makala hii inayohusu mahojiano aliyoyafanya huyu jamaa anaitwa Frank ambaye anasema ni mtoto wa Mchungaji Zachary Kakobe, nimeona si vibaya nikishea hapa inawezekana kama ni kweli basi ujumbe umfikie kwa urahisi mtumishi kwa kuwa najua JF ni platform kubwa na inafika mbali.
@@@@
Naitwa Frank Zachary Kakobe, mimi ni mzaliwa wa Tuliani, Wilayani Mvomelu Mkoani Morogoro, nilisoma Elimu ya Msingi Mwenge Mwaka 1986 hadi 1993 baada ya hapo nikaenda Real High School ipo Thiker Nchini Kenya
Baada ya hapo nikasomea masuala ya kompyuta nikapata Diploma katika chuo cha Techno Brain, sijui sasa hivi kinaitwaje.
Nina umri wa miaka 43, nina Watoto watatu na baada ya kuhitimu masomo yangu nilifanya kazi kadhaa za kiufundi.
Nia yangu ya kujitokeza kuzungumza hapa ni baba yangu apate taarifa juu ya uwepo wangu, tangu nilipoachana naye miaka 17 hadi 20 iliyopita, nimejaribu mara kadhaa kumtafuta kwa njia nyingi kupata mawasiliano naye lakini imekuwa ngumu.
Nimewahi kukaa pale Kanisani zaidi ya wiki sijaonana naye, nilipowaona viongozi wa Kanisa lake wakaniambia niandike barua ndio nitafanikiwa kumuona, nikafanya hivyo kwa kuandika barua za zaidi ya 300 lakini sijafanikiwa.
Nimetuma SMS za simu nyingi tu lakini hakuna mafanikio, ninachokumbuka nimewahi kukutana naye mara kadhaa akiwa anaingia kwenye gari nikawa naishia kumsalimia “Shikamoo Baba”, basi baada ya hapo inaishi hivyohivyo.
Nimeshaenda nyumbani Mbezi Beach lakini sijafanikiwa kuonana naye, hata wiki mbili zilizopita nilienda nikakutana na mlinzi ambaye akaniambia niandike barua.
Nikawa najiuliza niandike barua tena? Akaniambia ndio utaratibu, nikajiuliza niandike barua kuingia nyumbani!
View attachment 2546433
Nakiri kuwa hali ya mazingira kama hayo ikanifanya niwe mlevi, mara kadhaa nikawa nalewa licha ya kuwa mimi sipendi pombe.
Kuna muda nilikuwa nalewa kisha naenda Kanisani kumtafuta baba yangu kutokana na mawazo, nilikuwa nalala hapohapo Kanisani lakini hakuna mafanikio.
Sijui kuna ukuta upi uliotokea kati yangu na baba hadi anifanyie yote hayo, nakumbuka mara ya mwisho kupata mrejesho ilikuwa wakati nahitaji vyeti vya Watoto, nilituma SMS zaidi ya 80, ndipo nikajibiwa kuwa nifike getini nikachukue hivyo vyeti.
Nilienda na nikasaini kisha baada ya hapo sijawahi kupata mrejesho wowote.
Nilikuwa kimya muda mrefu, lakini nimeamua kufunguka na kumtafuta, mimi sina madai yoyote kuhusu baba, kwamba ndani ya miaka yoye hiyo ambayo sijamuona nadai kitu fulani, Hapana.
Unajua yeye ndiye kanilea kuanzia nikiwa mdogo nina miaka mitatu.
Kuhusu ukaribu wa wadogo zangu na mimi haupo, sijui wanapokaa wala wao hawajui ninapokaa na wala sijawahi kukaribishwa wala kushirikishwa kama familia licha ya kuwa mimi ndio nilikuwa ninawalea kwa kuwa walinikuta kaka yao.
Naamini barua ambazo nimekuwa nikituma inawezekana zinamfikia au hazimfikii, hivyo nimeamua kutumia nafasi hii kuweka wazi ili kama kuna ukuta upo kati yetu uweze kubomoka.
Matatizo katika familia yapo na ni kawaida kutokea, sijajua tatizo lililopo kati yangu mimi na yeye (Kakobe), kiasi kwamba kumekuwa na ukuta huo mkubwa.
Mfano mimi sinywi pombe kwa starehe, lakini imetokana na mawazo na kuathirika kisaikolojia, pia kwa kuwa nimeathirika kimaendeleo basi hata familia yangu pia imeathirika kwa njia moja au nyingine.
Baba yangu ni mtumishi na ninajua ana upendo sana, naamini haya mambo anaweza kuyatatua watu wakasameheana kama kulikuwa na shida.
Pia nina dada yangu anaitwa Mage ambaye naye hajaonana na baba kwa muda mrefu inawezekana zaidi hata ya ilivyo kwangu.
Chanzo: OnTV
Huyo jamaa anajulikana na juna wengi wanamjua akiwa hata chalii kanisan kwa kakobe miaka hiyo.Sasa kama una maisha yako na hakutaki kwanini umtafute?
Pili yaani baba yako na mama yako akukatae? Labda ni mtoto wa nnje mama kakobe anakaza
Apambane na maisha tu amuombe Mungu amsaidie apate fedha aache mambo ya kujikomba
Kihistoria kakobe amembeba sana huyu mtoto mpaka ikafikia wakati ni shida kwa kanisa...Hakuna watu wabaya zaidi ya hao wanaojiita watumishi wa Bwana.
Hapo wanaofia mali, mke kashika bango akisema mwana wa mjakazi hataridhi mali
Waambieni waache roho mbaya, mali zenyewe ni sadaka kutoka mifuko ya watu,
Ndugu mbona unanena maneno makali dhidi ya mwanadamu mwenzako kana kwamba sisi sote ni wakamilifu.....!!?Mtoto mpotevu alifuja mali za baba yake
Kakobe alimsomesha vizuri na akawa na maisha aliondoka kwake na akili timamu anamrudia akili zimeharibika aweza ua mzazi aenda kalewa kanisani hujui kavuta bangi au nini Halafu jitu zima miaka 43 huyo sio mtoto yule wa kisheria ambapo sheria hutaka mzazi awajibike yaani wa umri wa shule ya msingi au sekondari jitu zima hilo linasumbua baba yake kwa lipi? Liendelee na maisha yake kama baba yake halitaki si ni jitu zima
Anaeza akaamua kuzitumbua tu... Dogo kashiakua mtu mzima... Dingi hana tena majukumu ya lazima juu yake..Hata akidai/akiomba mali ni haki yake! Mali zote hizo Kakobe ataenda nazo wapi?
Kama kweli ni mtoto wake basi baba ana Siri kubwa. Ili mambo yake yaende inabidi mtoto awe hivyo.
Mmeanza aiseeKama kweli ni mtoto wake basi baba ana Siri kubwa. Ili mambo yake yaende inabidi mtoto awe hivyo.