Mtoto wa Zachary Kakobe: Mfikishieni salamu baba yangu namtafuta, sijaonana naye kwa Miaka 20, nikienda Kanisani sipati nafasi ya kumuona

Mtoto wa Zachary Kakobe: Mfikishieni salamu baba yangu namtafuta, sijaonana naye kwa Miaka 20, nikienda Kanisani sipati nafasi ya kumuona

Miaka 43 ndio unakuwa hivyo? Mbona anaonekana ana miaka 80 huko
 
Haikubaliki

Miaka 43 no please sio miaka ya kugombea cha mzazi anatakiwa awe alishapata chake kwa kuhangaikia maisha kivyake

Umri unakataa hata aende mahakamani

Hata mahakama itamshangaa
Wajukuu wanamtaka Babu hilo unasemaje
 
Nadhani ni kwa tabia mbaya alizokuwa nazo huyu kijana ndiyo maana baba yake alimtelekeza! Huyu kama sikusahau ni mmoja wa watoto ambao Bishop alizaa nje ya ndoa kabla hajaitwa kuwa Mtumishi wa Mungu.Huyu kijana angekuwa mtulivu angekula vinono! Kwa mfano ukiangalia watoto wa mke wa ndoa wa Bishop wako vizuri sana kimaisha na wana Kampuni yao ya biashara iinayowaingizia pesa nzuri tu.Sasa inawezekana huyu kijana akiona watoto wengine wa Bishop wako vizuri anajaribu kutafuta mlango wa kumwona baba yake akifikiri labda anaweza kumwangalizia fursa.
Nadhani kwa umri aliofikia huyu kijana angeendelea na mishe zake za kusaka maisha kuliko atafute fursa ya kuonana na baba yake ambaye yuko bize na majukumu ya Kanisa!
 
Lina miaka 43 bado toto hilo? Liende huko lisisumbue Mzee Kakobe tena likome


Ukisoma michango mingi ya wadau humu utagundua ni kiasi gani sisi waTanzania tu wabinafsi na wenye roho mbaya mpaka inatisha.

Fikra za kimaskini zimetawala bongo zetu kiasi kwamba utu wetu umemezwa na tamaa ya mali!

Giza la roho nyeusi limeyapofua macho yetu hatuoni uhalisia Bali matamanio yetu!

Tumepofushwa na matokeo mabaya ya kuuzoea umaskini mpaka tumeshupaza mishipa kumkatalia Jamaa haki yake ya kuwa mtoto wa Mzee Kakobe!! As if we can!!!

Tumeamua kuwa jamii isiyotambua na kuamini ya kwamba msingi sahihi na muhimu katika kuijenga jamii na kisha Taifa, ni familia imara yenye mshikamano mfano wa kamba ya Chuma.

Familia imara yenye mshikamano wa pamoja pasipo ubaguzi, umimi na mawazo ovu muda wote ndio nguzo pekee inayosimama kizazi na kizazi.

Si ajabu wengi wetu hatujui hata babu kizaa baba yake na babu ni nani!

Inaumiza sana kufikiria miaka 10 ijayo hali itakuwaje kijamii!!
 
Wana umri gani kuna umri mtoto hatakiwi nyumbani

Makabila kibao mfano kwa wakurya miaka kumi na tano tu lazima mtoto wa kiume ajitegemee na awe kwake

Sio hao tu yako mengi tu mtoto wa kiume zaidi ya miaka 18 hatakiwi kula hata nyumbani kwa mzazi anakuwa na kashamba kake na kajumba kake ka majani

Jitu zima miaka 43 linataka kuonana na baba yake na kwenda nyumbani kuhitaji msaada no please

Kakobe kazaliwa vijijini yuko sahihi

Mtoto miaka 43 hapana

Baba akisema usije kwangu baki tu kuwasiliana naye kwa simu tu usikanyage ofisini kwake wala nyumbani kwake kama hataki

Una agenda gani kukomaa kuwa lazima muonane uso kwa uso wakati simu zipo na namba unazo ? Si ukororofi huo
Angekuwa basi hata anampigia simu.
Angekuwa basi hata anasema nikietewe wajukuu zangu wanisalimie
Angekuwa basi anasema awasiliane na mkwewe.

Lakini hao watoto wengine kuwajengea majumba na kuwaanzishia biashara kunakuuma sana kuona huyu ambaye katupwa jalalani anataka tu kuzungumza na baba yake ili hata wasipoonana wawe wameagana salama unaona nongwa sana.

Kwenye video yake ameweka namba yake. Mpigie umpe marufuku yako asimhangaishe askofu wako


Lakini hao ndugu
 
Kakobe ana kaa Mbezi Beach
Kwenye nyumba kubwa
Kama sikosei mtaa wa Tembo
Hata akifika hapo majirani watamwonyesha
 
Katika pitapita zangu mitandaoni, nimekutana na makala hii inayohusu mahojiano aliyoyafanya huyu jamaa anaitwa Frank ambaye anasema ni mtoto wa Mchungaji Zachary Kakobe, nimeona si vibaya nikishea hapa inawezekana kama ni kweli basi ujumbe umfikie kwa urahisi mtumishi kwa kuwa najua JF ni platform kubwa na inafika mbali.

@@@@

Naitwa Frank Zachary Kakobe, mimi ni mzaliwa wa Tuliani, Wilayani Mvomelu Mkoani Morogoro, nilisoma Elimu ya Msingi Mwenge Mwaka 1986 hadi 1993 baada ya hapo nikaenda Real High School ipo Thiker Nchini Kenya

Baada ya hapo nikasomea masuala ya kompyuta nikapata Diploma katika chuo cha Techno Brain, sijui sasa hivi kinaitwaje.

Nina umri wa miaka 43, nina Watoto watatu na baada ya kuhitimu masomo yangu nilifanya kazi kadhaa za kiufundi.

Nia yangu ya kujitokeza kuzungumza hapa ni baba yangu apate taarifa juu ya uwepo wangu, tangu nilipoachana naye miaka 17 hadi 20 iliyopita, nimejaribu mara kadhaa kumtafuta kwa njia nyingi kupata mawasiliano naye lakini imekuwa ngumu.

Nimewahi kukaa pale Kanisani zaidi ya wiki sijaonana naye, nilipowaona viongozi wa Kanisa lake wakaniambia niandike barua ndio nitafanikiwa kumuona, nikafanya hivyo kwa kuandika barua za zaidi ya 300 lakini sijafanikiwa.

Nimetuma SMS za simu nyingi tu lakini hakuna mafanikio, ninachokumbuka nimewahi kukutana naye mara kadhaa akiwa anaingia kwenye gari nikawa naishia kumsalimia “Shikamoo Baba”, basi baada ya hapo inaishi hivyohivyo.

Nimeshaenda nyumbani Mbezi Beach lakini sijafanikiwa kuonana naye, hata wiki mbili zilizopita nilienda nikakutana na mlinzi ambaye akaniambia niandike barua.

Nikawa najiuliza niandike barua tena? Akaniambia ndio utaratibu, nikajiuliza niandike barua kuingia nyumbani!
View attachment 2546433
Nakiri kuwa hali ya mazingira kama hayo ikanifanya niwe mlevi, mara kadhaa nikawa nalewa licha ya kuwa mimi sipendi pombe.

Kuna muda nilikuwa nalewa kisha naenda Kanisani kumtafuta baba yangu kutokana na mawazo, nilikuwa nalala hapohapo Kanisani lakini hakuna mafanikio.

Sijui kuna ukuta upi uliotokea kati yangu na baba hadi anifanyie yote hayo, nakumbuka mara ya mwisho kupata mrejesho ilikuwa wakati nahitaji vyeti vya Watoto, nilituma SMS zaidi ya 80, ndipo nikajibiwa kuwa nifike getini nikachukue hivyo vyeti.

Nilienda na nikasaini kisha baada ya hapo sijawahi kupata mrejesho wowote.

Nilikuwa kimya muda mrefu, lakini nimeamua kufunguka na kumtafuta, mimi sina madai yoyote kuhusu baba, kwamba ndani ya miaka yoye hiyo ambayo sijamuona nadai kitu fulani, Hapana.

Unajua yeye ndiye kanilea kuanzia nikiwa mdogo nina miaka mitatu.

Kuhusu ukaribu wa wadogo zangu na mimi haupo, sijui wanapokaa wala wao hawajui ninapokaa na wala sijawahi kukaribishwa wala kushirikishwa kama familia licha ya kuwa mimi ndio nilikuwa ninawalea kwa kuwa walinikuta kaka yao.

Naamini barua ambazo nimekuwa nikituma inawezekana zinamfikia au hazimfikii, hivyo nimeamua kutumia nafasi hii kuweka wazi ili kama kuna ukuta upo kati yetu uweze kubomoka.

Matatizo katika familia yapo na ni kawaida kutokea, sijajua tatizo lililopo kati yangu mimi na yeye (Kakobe), kiasi kwamba kumekuwa na ukuta huo mkubwa.

Mfano mimi sinywi pombe kwa starehe, lakini imetokana na mawazo na kuathirika kisaikolojia, pia kwa kuwa nimeathirika kimaendeleo basi hata familia yangu pia imeathirika kwa njia moja au nyingine.

Baba yangu ni mtumishi na ninajua ana upendo sana, naamini haya mambo anaweza kuyatatua watu wakasameheana kama kulikuwa na shida.

Pia nina dada yangu anaitwa Mage ambaye naye hajaonana na baba kwa muda mrefu inawezekana zaidi hata ya ilivyo kwangu.

Chanzo: OnTV
Miaka 43????
 
Sasa kama una maisha yako na hakutaki kwanini umtafute?

Pili yaani baba yako na mama yako akukatae? Labda ni mtoto wa nnje mama kakobe anakaza

Apambane na maisha tu amuombe Mungu amsaidie apate fedha aache mambo ya kujikomba
Huyo jamaa anajulikana na juna wengi wanamjua akiwa hata chalii kanisan kwa kakobe miaka hiyo.
Sio kwamba kakobe hajawahi kuishi naye...
Pale kanisan alikuwa anagombanisha mabinti na akaanza ulevi.ilikuwa changamoto sana kwa kanisa vibinti vinatobolewa na huyu mwamba.
Kakobe akamwonya, akamwonya tena, na kumuonya ila jamaa akawa hasikii.Ikawa kakobe achague kanisa au mmtoto. Kwa hekima akachagua kanisa
 
Hakuna watu wabaya zaidi ya hao wanaojiita watumishi wa Bwana.

Hapo wanaofia mali, mke kashika bango akisema mwana wa mjakazi hataridhi mali

Waambieni waache roho mbaya, mali zenyewe ni sadaka kutoka mifuko ya watu,
Kihistoria kakobe amembeba sana huyu mtoto mpaka ikafikia wakati ni shida kwa kanisa...
Mabinti kanisani anawazoa...baaadae ulevi . Kakobe akaona asiwe taabu...
Majirani zake kakobe wanamjua vizuri akiwa chalii anaishi kwa kakobe
 
Mtoto mpotevu alifuja mali za baba yake
Kakobe alimsomesha vizuri na akawa na maisha aliondoka kwake na akili timamu anamrudia akili zimeharibika aweza ua mzazi aenda kalewa kanisani hujui kavuta bangi au nini Halafu jitu zima miaka 43 huyo sio mtoto yule wa kisheria ambapo sheria hutaka mzazi awajibike yaani wa umri wa shule ya msingi au sekondari jitu zima hilo linasumbua baba yake kwa lipi? Liendelee na maisha yake kama baba yake halitaki si ni jitu zima
Ndugu mbona unanena maneno makali dhidi ya mwanadamu mwenzako kana kwamba sisi sote ni wakamilifu.....!!?

Inawezekana kijana akawa amemkosea mzee wake kutokana na harakati na pirika pirika za kiulimwengu kama tunavyoelwa mambo ya ujana.........

Pamoja na yote lakini bado anasthili msamaha kwani yeye ni mzazi wake......mzee Kakobe ameze mate ya uchungu na amsamehe kijana kama ambavyo anahubiri KANISANI kwake nguvu ya msamaha.........

Amini nakwambia ya kuwa ijapokuwa inaonekana hajali kwa sababu ya kibuli na kumbu kumbu mbaya lakini nafsini mwake inamtesa kwani damu ni nzito kuliko maji...............

Haijalishi ametumia njia Gani lakini tujikitie kwenye hoja na ya msingi ya kijana........

Hata sisi kwenye maisha haya nyakati fulani huwakwaza na kuwakosea watu na huomba misamaha na kusamehewa..........

Kuhifadhi mafundo ya chuki dhidi ya wanadamu wenzako ni ushetani bali kuachiilia msamaha ni upendo.........
 
Kama kweli ni mtoto wake basi baba ana Siri kubwa. Ili mambo yake yaende inabidi mtoto awe hivyo.
 
Mambo gani? Hujawahi kuona mtoto wa tajiri yupo yupo tu na hasaidiwi? Mwingine anakunywa mpaka anapoteza fahamu! Tajiri atashindwa kumsaidia?
 
Back
Top Bottom