Nina mtoto wa kiume umri miaka 2.5, huyu kijana wangu akiwa na hasira anatabia ya kujibonda chini au sehem yoyote kwa nguvu sana na pia anang'ata sana, kufinya, angali akiwa toka mdogo nikajua labd akikuwa ataacha.
Saiv imekuw 2much anaeza fanya kitu ukamtoa au ukamnyang'anya basi ni ugomvi mzito katoka nundu chin ya jicho jana tu saiv napata taarifa kavimba kichwa washavirugana na mama ake kiukwel hii hali inanipa wasiwasi sijui huyu mtoto anatatizo gn alaf anakuwa anahasira kali sana muda mwingin anataka mpk mpigane km mkitibuana anakukwida
Pole sana , tafuta mtaalam wa mahusiano ya watoto na mlezi au mwanasaikolojia wa watoto. Ila kipindi unapanga kukutana na mtaalam fanya yafuatayo kupunguza mtoto asijiumize:
1.usimnyanganye kitu au kumkataza kitu Kwakumkaripia, ongea nae Kwa utulivu pale unapohitaji kumhasa asifanye kitu. Akianza kulia au kupiga kelele nyamaza person, Tulia, usishtuke.
2.ukiona anataka kujibamiza mchukue Kwa utulivu na mkumbatie ili akiwa anataka kubamiza kichwa uwe umemdhibiti ajikute anaishia kukutana na Bega au kifua huku mkono umemshika kichwa asijirusherushe Bali atulie. Ukifanya hivi uwe kwenye hali ya utulivu, I nyamaza usiseme kitu labda uwe unambembeleza Kwa kutembea au kuyumba ukiwa umembeba na kumkumbatia kama tunavyofanya ukiwa unataka kumtoa mtoto gesi baada ya kula. Usiongee, usimkaripie, I usimkandamize Kwa nguvu. Baada ya muda mwili wake utarelax na hasira zitapungua. Akitulia anza kuongea nae Kwa pole. Ongea nae Kwa utashi kama ambavyo ungongea na mtu mzima aliyetoka kuhuzunika au kasirika. Mpe pole Kwa Ile hali, I muulize kama bado ana hasira au la, I na kama anahitaji muda zaidi au yuko tayari kuongelea kwanini hawezi kupata anachotaka Kwa muda Huo.
3.kamwe usimkimbie au kuondoka bila kumuaga, kama Kuna mzazi au mlezi anafanya hivyo Basi asitishe kufanya hivyo. Mkitoka mumuage, I hata kama Natalia na mwambie utarudi lini na sa ngapi. Ukirudi mtaarifu kuwa Umerudi.
4.asichapwe wala kupewa adjabu ya kumpa maumivu ya mwili pale mnapomuadhibu. Tafuta adhabu mbadala kama kutokuangalia kipindi anachopenda au kutokwenda kucheza Kwenye mtoko wa familia n. k.
5.kama Kuna mtu mwenye kukasirika
haraka na kukaripia hapo nyumbani apunguze au atafute mbinu na msaada wa kuweza kupunguza hasira. Kwenye kutokuelewana watu wa hiyo nyumba wa Jaribu kuongea Kwa sauti za chini sio kupayuka na kusiwe na hali ya kuumizana Mbele ya mtoto. Hii ni Kwa wote hata watoto wenzake au ndugu wanaoidhi hapa wasitumie person njia za kikatili kwenye mawasiliano.
6.hakikisha Ana ratiba yenye kupunguza hasira mfano kalale masaa nane usiku, acheze vya kutosha mchana, asile vyakula yenye sukari sana au ngano, asitumie vyombo vya screen zaidi ya ule unaoshauriwa Kwa umri wake n.k.
Haya yatasaidia wakati unapanga kumuona mtaalam. Atakua Sawa, ni changamoto kwenye mawasiliano na hisia.Utatuzi wa haraka na kitaslam utasaidia kusiwe na hatari ya kutumia Kwa Sasa na uwezekano wa changamoto Nyingine huko Mbeleni.