Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Kuna namna wazazi huwaona watoto kama hivi hawana hisia au wanaweza kuachilia vitu kirahisi kiasi kwamba anaweza kumfanyia kitu ambacho kitamuumiza na yeye atakibrush tu na kuendelea na maisha yake kama kawaida au hata kama akikubali kosa inakuwa ni ile ya ilimradi.
Unakuta umekula mkong'oto wa maana kwa kitu ambacho hujafanya au umesingiziwa, akijua ukweli anakwambia kwanini hukusema sasa? Au mi nisingekubali kuchapwa wakati sijafanya, au ila kuna wakati ulifanya kama hivi! Yaani hakuna kukiri kuwa ulikosea na unahitaji kurekebisha kwa kukiri kuwa kweli ulichofanya si kitendo cha uungwana.
Mwisho mzazi anashangaa kwanini mtoto wake hana ukaribu nae, na anajitahidi kujitenga kila nafasi anayoipata tena, kwanini hamwambii tena shida zake au hawapigi tena story kama zamani.
Maumivu yale huwa ni makubwa sana kwa mtoto, anayabeba yote kwenye moyo na kuhusanisha na upendo wa mzazi kwake hasa inapokuwa kuna mtoto anapendwa zaidi yake na hata afanye nini huwa hapati adhabu kama yeye.
Nilikutana na post moja Insta mzazi anasema kama nilikukosea njoo tuongee LAKINI UJE KWA HESHIMA! Like umeniacha na maumivu miaka yote hiyo na bado unakuwa na udacity ya kuweka masharti? Yaani mazungumzo yafanyike lakini kwa your own terms, hapo unakuwa unaomba msamaha au bado una impose mabavu yako kwake. Kwamba kwakua wewe ni mzazi you should always have an upper hand?
Ukifuatilia watu wazima wengi ambao mahusiano yao na wazazi yao sio ya kuonana jicho kwa jicho (yana ukakasi) utakuta tu kuna mambo mzazi alifanya, yakakua na kujijenga kufikia hatua mtoto akasema basi, wacha niendelee na yangu.
Na ukitaka kujua kuwa watu wana maumivu, unakuta mtu ana miaka 25, 30+ au 40 anakumbuka kosa alilofanyiwa akiwa na miaka 9, au 12, yaani anakuelezea kama vile jambo lile lilitokea jana!
Waombeni watoto wenu msamaha mnapowakosea, kama ambayo unachkmwa mtu akikukosea, ni zaidi kwa mtoto hasa hisia zake zinapopuuzwa. Na mkianza mazunguzo hayo usiende na masharti, acha mtoto afunguke atoe uchungu wake na hasira yake. Only then ndipo mtaweza kurudisha that bond mlitengeza.
Kama unaona humuwezi kufanya hilo wenyewe, unaweza kutumia usaidizi wa therapist au mtu mwingine ambaye mtoto wako atajihisi kusikilizwa bila kudogodeshwa au kuwa judged kufungua hisia zake.
Tusikuze watoto na uchungu, trauma, inaumiza sana.... na wewe ambae umekuwa na maumivu hayo jitahidi upone (heal) ili usije kurudia jambo hilo kwa mtoto/watoto wako.
Wewe una experience gani? Mzazi alikuomba msamaha alipokukosea au bado unajifunza namna ya kuachilia maumivu hayo wewe mwenyewe?