Mtu anapoomba maji baada ya ajali na ukampatia, ni nini kitamtokea?

Vipi kuhusu water break ile ya uwanjani mkipiga mtanange ,inashauriwaje au kwakua ni mpira sio mazoezi ya viungo?
 
Mhasiriwa? Ndio nini? Au ilikusudiwa muathirik(w)a?
 
Hataree sana. Sasa miezi mate si kondoo wa BWANA wangemweka kwenye kitubio.
 
Vipi kuhusu water break ile ya uwanjani mkipiga mtanange ,inashauriwaje au kwakua ni mpira sio mazoezi ya viungo?
Hapa unakuta wachezaji wamechemka balaa halafu na hapo hapo wanakunywa maji na hamna kinachotokea
 
sikia mtu akiomba maji mpe ila asinywe bali mlambishe ktk lipa anywe matone matone utamsave sana sana kuliko kumpa aingie utamuua
 
Kiu kali kwa muhanga wa ajali ni kutokana na kupoteza maji mengi na damu nyingi!!ikumbukwe tumboni kuna mishipa mingi ya damu kwa ajili ya kufyonza maji na chakula!!sasa kama damu imepungua mwilini ujue maji utakayompa mhanga hayatafyonzwa na mwili tena bali yatamtia ganzi tumboni na mwili kwa ujumla yataenda kupoza neva na mishipa na kutia ganzi mwili mzima!hicho ndicho chanzo vifo hivi tuvionavyo!!njia pekee ni kutundikiwa dripu ya maji ambayo yataingia kwenye mfumo moja kwa moja kabisa bila madhara!!!!!GANZI KWENYE TUMBO INAYOTOKANA NA UBARIDI WA TUMBO NDIO HUMUUA ANAPOPEWA MAJI BARIDI AKIWA HANA DAMU YA KUTOSHA!!!
 
[emoji122][emoji122]
 
Asante sana mkuu!! Ila ungeiandika kwa lugha yetu ya kizaramo hii ulikuwa umemaliza kabisa yani. [emoji120][emoji120] by the way..
 
2020 Mwezi May, somewhere Kanda ya kati,nilipata ajali mbaya sana, nilikua pekeyangu... Bahat nzuri eneo hilo kulikua na watu. Nilikua ktk hali mbaya sana,nilijihisi kuzimia na kuishiwa nguv. Niliweza kujitoa nje ya gari... ILINIJIA KIU KUBWA SANA NIKATAKA KUOMBA MAJI. ILA NAFSI YANGU IKANIKATAZA NISIOMBE MAJI, NA NIKAKUMBUKA KTK HALI HIYO KUOMBA MAJI NI SAWA NA KUOMBA UMAUTI... Sikutamka kuomba maji... Ktk yote hadi leo sijui niliponaje ktk ile ajali maana kilamtu alikua anajua nitakufa anytime. MUNGU NI YEYE YULE JANA LEO HATA MILELE NITAMUABUDU POPOTE
 
Pole Sana mkuu
 
Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…