Mtu anayejenga gorofa bila kusimamisha nguzo za zege (columns), ni imara kweli?

Acha kucomplicatisha maisha, unahitaji detailed structural analysis umetoa hela??
Mtu kauliza amejibiwa shida iko wapi??

Anyways, Hakuna shida, mimi ni engineer tena structural na nina muhuri kabisa wa ERB.

Nasema hivi, INAWEZEKANA TENA BILA SHIDA YEYOTE KUJENGA JENGO HATA LA GHOROFA TATU BILA KUTUMIA COLUMNS.

Ukiwa na tofari za kuchoma itakuwa nzuri zaidi kuliko hizi za block za mtaani.

Maana tofari za kuchoma constantly zina bearing capacity kubwa ukilinganisha na za block ambazo nyingi ni za michongo
 
Sijatumia formula ya darasani,ila kwa uzoefu gorofa moja itashikiliwa na kuta imara za chini; utakapoenda gorofa ya pili, itategemea muendelezo wa gorofa ya kwanza kutokea kwenye msingi, ambapo kiunganishi ni nguzo kutoka chini



Unasema uzoezi je ni uzoefu gani na wa nani?

Na huo uimara wa kuta ya chini unaupimaje ili kukiridhisha ni imara? Unaweza kutupa kipimo chake ili na sisi tujue ni imara?

Je hiyo nguzo kutoka chini inatofauti gani na ujenzi kwa kutumia columns?

Ujue unapojenga nyumba ya kuishi watu unaongelea uhai wa watu mkuu!!
 
Ni kweli, kila kitu lazima kiwe na standard ila changamoto ni rasilimali fedha; kwa ushauri, kama ni gorofa moja ni bora ground floor iwe na nguzo na bimu ili kubeba uzito wa juu
 

Bwana mhandisi kwanza nikupe pole maana umedandia treni kwa mbele! Ilibidi uelewe mada imeanzia wapi kwanza kabla ya kukimbilia kujibu.

Nilicho andika sio kwamba mimi nataka hizo designs kiasi kwamba uniambie nitoe ela. Hoja iliyo kuwepo ni kwamba tulimshauri mleta mada aombe hivyo vitu kutoka kwa injinia wake. Na sio mimi nilikua naomba. Umeelewa?

Pia umetoa jibu ya kwamba inawezekana kujenga hata ghorofa tatu.

Hili ni jibu ambalo siwezi siwezi lisemea chochote au nikalikubali maana halina any logic ya kuniwezesha mimi kuli prove!

Na ndio maana nikamshauri mleta mada kabla hajachukua ushauri wa injinia wake amuulize kama ana structural design and analysis inayo support jibu alilo pewa!

Then kutokea hapo anaweza fanya maamuzi!

Nadhani umeelewa mkuu!
 
Ni kweli, kila kitu lazima kiwe na standard ila changamoto ni rasilimali fedha; kwa ushauri, kama ni gorofa moja ni bora ground floor iwe na nguzo na bimu ili kubeba uzito wa juu
Ukisema changamoto ni rasilimali fedha nakataa!

Kama mtu ana jenga ghorofa jua ana bajeti si chini ya 100mil! Sasa kama uko tayari kutumia 100mil kujenga kweli anakosa hata 5mil za kumpa injinia kishkaji asimamie kazi yako?
 
Kuna pahala umeona nikitanabaisha linaweza jengwa sehemu yoyote ile duniani?
 
Hata ghorofa tatu inawezekana sana tu
Shida sio ghorofa tatu hata 10 wenda ukajenga! Swali ni je kuna scientific/engineering logic behind hilo jibu?

Na ndio mana kwenye posti yangu ya awali nilimshauri ajiridhishe hilo kutoka kwa injinia!

Maana siku hilo ghorofa likianguka tujue tunaanzia wapi sio aje atuambie aliambiwa ajenge tu bila colums!
 
Tuangalie kwanza kilichosababisha jengo la Goba kuanguka.
 
Ndo hilo lililoanguka goba?
 
Kuna pahala umeona nikitanabaisha linaweza jengwa sehemu yoyote ile duniani?
Kuna sehemu yeyote kwenye posti nimeandika kwamba umesema linaweza jengwa sehemu yeyote duniani!?

(Kabla hujajibu rudia kusoma uelewe nilicho andika kwenye comment niliyo ku quote).
 
Tuangalie kwanza kilichosababisha jengo la Goba kuanguka.
Kwa wenzetu nje huwa jengo likianguka ni kampuni yenye uzoefu wa maswala ya majengo wanapewa tenda kutafuta chanzo!

Moja kati ya vitu wanavyo angalia ni report ya usanifu ya injinia, na ndio nikamshauri mleta mada awe na hii report!
 
1. Ni Engineer mwenye mhuru na amesajiliwa na board
2. Gorofa moja tu mkuu
3. Yes ameprovide structural drawings
4. hatujafanya soil analysis
Asante mkuu for your concern.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…