Unaweza kujenga, ila tu inabidi ulaze tofari na hizo tofari unazolaza inabidi ziwe na compression strength ya 4.5 yaani (atleast mfuko mmoja wa cement 42.5 itoe tofari 25) ambapo tofari moja uwa ni Tsh 1800 ziwe cured na zimekaa siku 21 tokea kufyatuliwa, usitumie tofari ya Tsh 1000/1200. Pia hapo hapo partitions za vyumba vya chini visizidi span ya mita 4 bila kuwa na ukuta.
Kuongezea tu hapa, ghorofa bila nguzo zinaitwa kitaalamu (load bearing structures) na zile za nguzo zinaitwa (frame structures). Ni vizuri kujiridhisha kwa kusoma na kuwafata wataalaam na sio washinda katika mitandao