Mtu anayejenga gorofa bila kusimamisha nguzo za zege (columns), ni imara kweli?

Mkuu ubarikiwe. Umenifungua sana macho
 
Ni kweli mkuu. Asante
 
Inawezekana kabisa... nimejenga gorofa 1 bila kutumia nondo, matofali ya chini ni ya inch 6 na yamelazwa.. nyumba ni imara haina nyufa zozote.. mwaka wa 15 sasa
 
Kuna Eng. Mkali humu.. hataki kabisa mambo ya kuhisi inawezekana.
 
Mim makubaliano na mapendekezo yako kwamba kila ujenzi lazima mtalaamu ahusishwe ktk hatua zote muhimu kutokana aina ya jengo na eneo linakojengwa .Ni kwel tofali zinaweza kujenga mpaka ghorofa 4 to maximum ili mradi tu wazingatie ubora wa materials na aina ya udongo .mfano mzuri ni ghorofa polisi ufundi kilwa road dsm na Jeshi pale mwenge.
 
Unaweza kujenga, ila tu inabidi ulaze tofari na hizo tofari unazolaza inabidi ziwe na compression strength ya 4.5 yaani (atleast mfuko mmoja wa cement 42.5 itoe tofari 25) ambapo tofari moja uwa ni Tsh 1800 ziwe cured na zimekaa siku 21 tokea kufyatuliwa, usitumie tofari ya Tsh 1000/1200. Pia hapo hapo partitions za vyumba vya chini visizidi span ya mita 4 bila kuwa na ukuta.
Kuongezea tu hapa, ghorofa bila nguzo zinaitwa kitaalamu (load bearing structures) na zile za nguzo zinaitwa (frame structures). Ni vizuri kujiridhisha kwa kusoma na kuwafata wataalaam na sio washinda katika mitandao
 
Tofautisha ghorofa na nyumba zilizobebana! Pale Goba walijenga nyumba zilizobebana wakadhani wanajenga ghorofa!

Hata mchwa wanaweka nguzo kwenye zile basement zao!
 
Cha kwanza ulicho feli ni kuamini katika degree hapo ndipo ulipo feli na nikaudharau uzi wako wote na ujuzi wako wa kwenye madaftari.
 
Wewe umejibu kitaalam kabisa 100%
 
Salaam

Naombeni msaada kuhusu hizo nguzo za geti.
Naambiwa na kijana wa zege kuwa wakati fundi anajenga hapo hizo nguzo kuwa hawakuchimba msingi mrefu kwenda chini na hana hakika kama waliweka kitako chini.

Bahati mbaya fundi alikimbia kabla ya kazi kukamilika na pia hapatikani kwa simu.
Sasa naombeni msaada wa kitaalamu hapo nifanye nini??
Je nivunje hizo nguzo zisukwe upya ama tufanyie ukarabati ili kuweza kuziimarisha hizo nguzo.

Mimi nipo mbali nashindwa kusimamia kwa ukaribu ujenzi.

Tafadhali naomba maoni yenu ya kitaalamu

Trendz
Upepo wa Pesa Equation x
 
Kwa jengo la gorofa moja hakuna tatizo. Isipokuwa uzingatie uimara wa tofali na msingi. Pia nguzo baadhi ya sehemu zenye uwazi mpana jengo la chini au ground floor zinatakiwa ili kuweka uimara wa jengo la juu.
 

Kazi ya nguzo (column) ni kusafirisha loads(mzigo) kwenda ktk ground na kazi ya kitako (Footing) ni kupunguza presha ya udongo inayotokana na mzigo uliobebwa juu.
1. Nguzo zako hazina mzigo wowote uliobebwa juu
2.Kuna aina tofauti za columns na sio kila column lazima iwe na footing.
3. Ukiangalia vizuri ktk picha umetuma kuna beam iliungwa na nguzo ya geti inamaana geti lako halitacheza.
4. Kwa rangi ya udongo wako ninaoona hapo yani wala usipate stress sana kuwa zitadondoka labda tu hiko kibonde kiwe kina erosion hapo utakuwa na tatizo.

Kwa ushauri soma Vizuri nilichoandika number 3
 
Kuna perception 2 hapa.
1. Kama hatumii nguzo (column) atalazimika kufanya Walls transformation kutoka non load bearing to load bearing walls kitu ambacho economically itakugharimu sana.
2. Kama atatumia nguzo (column) hapa load transformation itakuwa controled na column at the same place walls zitabaki kuwa material ya kawaida.
Ushauri: Ujenzi wowote wa holera huleta unafuu wa muda mfupi na hasara ya muda mrefu. You have to design the stated building and checked before implementations
Thanks
 
Ahsante mkuu Trendz
Hapo juu ya nguzo kuna slab nyembamba alafu na tofali zimelazwa 40.

Je kuna namna ya kuimarisha hizo nguzo ziwe imara mara dufu?
Mimi huwa sipendi vitu vya wasiwasi.
 
Ila hata hizo tofali za kuchoma dio hizi za USWAHILINI labda ziwe kana ziler ZA NYANKALI - DODOMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…