Nimewahi panga Nyumba fulani hivi kuna jamaa alikuwa anashinda chumbani asubuhi hadi jioni na anakula vzuri anapendeza na analipa bills zote bila usumbufu hadi majirani na wapangaji wenzie hususani wanawake walikuwa wakihisi labda anajihusisha na uuzaji madawa au ndo wale wa ile pesa tuma kwa namba hii..
Hii imekaaje wadau
Sikuhizi kuna njia nyingi sana za kupata fedha na kuinua uchumi wako, usikariri zile traditional ways kwamba lazima uingie mzigoni mzima mzima ndio upate pesa
1. Kuna Remote work. Mtu ana ofisi home ni Pc yake tu mchezo umeisha.
2. Freelancers, watu wanatafuta madili, yakitiki ndio wanaenda piga, unahisi wameenda kutembea kumbe mchongoni, na wengine wanapigia online, Upwork etc.
3. Passive investment, watu wengine walijiwekea plans za ku retire mapema, so wamejiwekeza, miradi,hisa, UTT, Hati fungani gawio wanalopata linawatosha.
Ukisoma kitabu cha Millionaire next door utaelewa, kuna watu mnaweza kuwa mnaishi nao kitaa ,but wana ukwasi na hawahtaj kukuonyesha au kukupa ishara.
4. Support, kutoka kwa ndugu, Mpenzi, wazazi etc. humu inahuisha wadangaji piaaa..
5. Matapeli, Kuna watu wanapiga madili ya ku scam watu mitandaon etc.
Maisha ni siri ,watu wana sirii sanaaaaa, siri maana yake ni fumbo huwezi kulijua.