Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Kwani ushauri hutolewa kwa namna gani mkuu?
Ndo kwanza naingia humu, bado nina maluweluwe. Ngoja nitulie kwanza, maanake naona kuna mengi ya kujadili kati yetu.
Nimeweka mstari wa nyongeza katika bandiko hilo ulilojibu sasa hivi. Tafadhali nenda kausome.
 
Ndo kwanza naingia humu, bado nina maluweluwe. Ngoja nitulie kwanza, maanake naona kuna mengi ya kujadili kati yetu.
Nimeweka mstari wa nyongeza katika bandiko hilo ulilojibu sasa hivi. Tafadhali nenda kausome.
Ok mkuu ubarikiwe sana kwa kujibu hoja kielimu zaidi tofauti na baadhi ya wachangiaji wengine wanaojibu hoja in somehow.
 
Crap
 
Kwani zito ni mpinzani?
Ni mpinzani wa makaratasi, ila kiroho ni miongoni mwa wapinzani butu waliotengenezwa na mfumo ili kuihadaa dunia kuwa Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi. Na matokeo yake misaada inayotumwa kwa ajili ya kukuuza na kuimarisha demokrasia hiyo inaliwa na wajanja wachache walio serikalini, CCM na Upinzani. Kama hautojali rudi juu kidogo kasome post namb #20 utaelewa nilichoandika hapa.
 
Ndo kwanza naingia humu, bado nina maluweluwe. Ngoja nitulie kwanza, maanake naona kuna mengi ya kujadili kati yetu.
Nimeweka mstari wa nyongeza katika bandiko hilo ulilojibu sasa hivi. Tafadhali nenda kausome.
Unaweza pia pitia post namb #20 kwa kaufafanuzi fulan. Just thinking tu maana moyo wa mtu msitu. Na ni Mungu pekee anaejua yaliopo mioyoni mwetu.
 
Ndiyo hii uliyonirejea (refer)?

Hapana, bado tunapishana sana.
Ila najuwa unastahili kupewa maelezo ya kina katika kupishana kwetu, na muda huo sasa hivi haupo. Nitaangalia njia ya kuja hapa tena kueleza tunavyopishana.
 
sisiemu kuanguka hilo swala litoe kichwani na wakianguka wametaka wao wenyewe hvi unaijua sisiemu ww sio watu wa nchezo kwenye swala a nani aiongize nchi
 
Ndiyo hii uliyonirejea (refer)?

Hapana, bado tunapishana sana.
Ila najuwa unastahili kupewa maelezo ya kina katika kupishana kwetu, na muda huo sasa hivi haupo. Nitaangalia njia ya kuja hapa tena kueleza tunavyopishana.
Ok mkuu, sisi wote tupo hapa kwa ajili ya kujadili namna ya kulijenga taifa lenye kesho nzuri kwa vizazi vyetu. Ni tofauti na wanasiasa ambao 98% wapo kwa ajili ya kuijenga kesho nzuri yao na ya vizazi vyao. Huku wakituhadaa sisi wafuasi wao wa vyama kuwa wanatusaidia kutujengea kesho yetu.
 
Hakuna lililo la maana zaidi kuliko kuiondoa CCM kwenye madaraka wakati huu. CCM kung'ang'ania kutawala kwa mabavu kwa kutumia vyombo vya dola haihitaji kuwepo na chama chenye sera bora zaidi kama uwezo wa kuondoa mkandamizaji inawezekana.

Kipaumbele kwa Tanzania sasa hivi ni kuiondoa CCM, mambo ya sera na mengine yatafuata baadae.
This is how serious it has become.
 
Mkuu kuiondoa CCM bila kujua huyo atakaeiondoa CCM atakuja na sera au mikakati gani ya kuijenga nchi, ni sawa na mtu anaeacha kazi bila ya kuwa na plan ya kazi nyingine.

Wakati nchi za magharibi zinaivamia Libya, kuna walibya wengi walifurahia uvamizi ule wakiamini kuwa ndio ilikuwa njia ya wao kuanza kuishi maisha kama wanayoishi wazungu huko ulaya na amerika.
Sasa hivi miaka 10 baada ya Gadafi kung'olewa na kuuwawa, walibya wale wale wanajuta na kutamani utawala ule wa Gadafi ungeendelea tu kulikoni huu uliopo sasa ambao kwao ni majanga makubwa. Hivyo hivyo kwa nchi nyingine kama Iraq, Sudan kusini, kaskazin nk.

Kwahiyo mkuu kusema tu CCM itoke bila kujua huyo atakaeingia baada ya kutoka atakuwa na mikakati gani ni kujivika kitanzi ambacho hapo baadae yakija kutukuta ya zaidi ya haya yanayofanywa na CCM tutashindwa kukitoa shingoni. Malawi kila siku wanabadili vyama lkn hali inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku, halikadhalika Zambia pia.

Wanasiasa ni kama wacheza mpira. Anapokuwa nje ya uwanja atakwambia dah ingekuwa mimi ndo niko uwanjani mechi hii ningefunga hata magoli kumi.
Lakini ukimuingiza acheze hana la maana atalofanya mpaka mechi inaisha.
 
Mkuu kuiondoa CCM bila kujua huyo atakaeiondoa CCM atakuja na sera au mikakati gani ya kuijenga nchi, ni sawa na mtu anaeacha kazi bila ya kuwa na plan ya kazi nyingine.
Bado huelewi ninachosema.

Hakuna kipaumbele Tanzania kuliko kuondoka kwa CCM madarakani.
Hicho ndiyo kipaumbele zaidi vingine vyote sasa hivi.

Unapopata dharura na kutaka kuondoka kwenye dharura huna anasa ya kupanga hayo mengine yafuatayo. Hayo yatakuja baada ya kuondokana na dharura.

Sasa kama bado huelewi ninachosema hapa, hutaki kuelewa na hutaelewa kamwe hata nikiandika na wino wa dhahabu.
 
Nilijua toka mwanzo unapolalia na mada yako hii.
Unaleta mifano ya ajabu sana katika mjadala usiohusiana kabisa na hiyo mifano.

Ngoja nimalizane nawe kwa kukueleza kuwa haijalishi CCM iliyopo sasa inaondoka vipi, na haina maana kuwa mageuzi hayawezi kutokea huko huko ndani ya CCM.
 
Ni dhahiri toka mwanzo wewe ni mfaidika wa uozo huu wa CCM iliyopo sasa. Najaribu kujikumbusha michango yako ya huko nyuma. Nikikumbuka vizuri ni kama tuliwahi kujibizana kwa kiasi juu ya misimamo yako hapa hapa JF.
 
Nimekuelewa mkuu.
 
Nimekuelewa vizuri mkuu. Lakini hili ni wazo lako pengine na wenzako, sio wazo la watanzania wote including myself.

Nchi yoyote ikiwemo Tanzania huwa na makundi matatu ya kuamua mustakabali wa nchi kupitia demokrasia. Makundi hayo ni 👇
1) Kuna kundi ambalo huwa upande wa chama tawala. Lenyewe humpigia kura mtu aliepitishwa na chama chao ili agombee uraisi, ubunge, udiwani nk, haijalishi mgombea ana sifa nzuri au mbaya.
2) Kuna kundi ambalo huwa upande wa vyama vya upinzani. Kundi hili nalo pia huwapigia kura watu waliopitishwa na vyama vyao ili wagombee uraisi, ubunge, udiwani nk. Haijalishi wagombea hao wana sifa nzuri au mbaya.
3)Kundi la mwisho hili halina chama au linachama lkn huwa linamchagua mtu kwa kufuata tu sifa za mtu alie katika kinyang'anyiro cha uraisi, ubunge, udiwani nk.

Sasa unaposema kuwa CCM inahitajika kutoka hata sasa hivi bila kujali chama au mtu atakaeingia baada ya CCM kutoka madarakani, sikupingi maanake huo ni mtizamo wako wewe na wenzako. Ila kuna mtizamo wangu mimi na wenzangu ambao baada ya kuangalia aina ya upinzani uliopo nchini, na sifa, matendo au tabia za wagombea mbali mbali wa uraisi, ubunge na udiwani waliopitishwa na vyama vyao kugombea nafasi hizo nchini. Sisi kwa mtanzamo wetu tunaona ni afadhali mara 70 CCM iendelee kubaki kuliko wao kuingia ikulu. Maana tabia zao hazina tofauti na zile za CCM au pengine ni zaidi ya zile za CCM. So huwezi kusema kuwa mimi siipendi harufu ya mkojo nyumban kwang, lkn wakati huo huo unaona sawa tu kuishi katika nyumba ambayo nyuma ya dirisha kuna shimo la choo linalotema harufu ya kinyesi. So hapo ndio tunapopishana. Katika CCM kuna mafisadi, waongo, wachumia tumbo na wanafiki, na katika upinzani vyama vyote kuna mafisadi, waongo, wanafiki na wachumia tumbo.
 
Alphonce mawazo Yuko wapi??nani alimuua Mwangosi??Tume huru ya Uchaguzi Iko wapi??nani alizuia Mali za Lowasa na kuzitoza Kodi kubwa??nani Alivuruga Uchaguzi 2019/20??kwa nini wakiunga mkono juhudi,lazima wapewe vyeo??senseless person will not and never see oppression for opposition
 
Mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa watanzania walio wengi huko vijijini.huko Hadi mtendaji wa kata ni kama rais.wakipewa kofia na t-shirt wanaridhika.only that
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…