Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Sifa hizo mimi ninazo.

Wana Jamii Forum kwa umoja wetu tuundeni chama chetu cha siasa kitachoongozwa na:
1) Mwenyekiti: Maxence Melo
2) M/mwenyekiti: Pascal Mayalla
3)Katibu mkuu: Mshana.

Kwa uongozi huu hapo juu CCM inaaga mchana kweupe
Mm nitakua mtinza hazina wenu
 
Acha uongo, hakuna uchaguzi ulivokua na wapiga kura wengi kama 2015 sasa wakina nani walikata tamaa kisa Lowassa?? Sema walikata tamaa ya kushinda milele maana chance ya 2015 ilikua realistic zaidi so walivunjika moyo kura zilipoibiwa.

2. Kuhusu nguvu ya umma iliwezekana sababu serikali haikuwa violent kama ya JPM. Enzi za Kikwete kina Mnyika na Dr Slaa walikua moto sana ila sikuwahi ona Slaa akimiminiwa SMG au Mnyika kutekwa!! Hivi unadhani baada ya tukio la Lissu na SaaNane kuna mwenye ujasiri aingie barabarani?

3. Hiyo CUF unayosifia hapa nayo ilipoa baada ya machafuko ya zenji walipomwagiwa risasi kama mvua. Ukiwa violent unadhani raia wasio penda vurugu watalipiza?? Unless kama unataka tuanzishe armed wings kama vyama vya huko uarabuni.

All in all vyama vilipoa sababu ya violent crackdown ya serikali huku napoishi kuna mdhamini wa kisiri wa CHADEMA ni tajiri wa hardware ila alisakwa mpaka akapotea mpaka Leo Hana hamu ya kusikia siasa. Sasa huyo utasema ni sababu ya Lowassa?
Mkuu hebu tuwe wakweli, bila muunganiko wa vyama ulioitwa UKAWA unafikiri Lowasa angepata kura nyingi kiasi kile? Kumbuka Lowasa aliungwa mkono na vyama vyote vikubwa vya upinzani Tanzania kama vile CUF ya Maalim iliyokuwa na mamilioni ya wapiga kura kule Zanzibar lakini pia ilikuwa na mtaji wa wapiga kura kadhaa huku bara.

CDM na NCCR MAGEUZI nao kwa umoja wao walikuwa na mamilioni ya wapiga kura bara, lkn pia walikuwa na mtaji wa wapiga kura kadhaa Zanzibar.
kwahiyo ni lazima angepata kura zile alizopata. Hata ingekuwa wewe ndio unagombea afu vyama hivyo nilivyotaja hapo juu vinakuunga mkono, amini ungepata kura nyingi ambazo wewe mwenyew hukutarajia.

Ndomaana baada ya uchaguzi ule kuisha na UKAWA kusambaratika kilichofuatia ilikuwa ni aibu.
Wapinzani walianza kuangukia pua hata katika chaguzi ndogo tu za kawaida hapo Kinondoni na kupelekea wapinzani kujifanya kuitisha maandamano na hatimae maandamano yale yakaondoka na roho ya Akwilini.

Kuhusu wapinzani kunywea hii haisababishwi na utawala wa Magufuli, bali watanzania wenyewe wamechoshwa na siasa uchwara za hawa wapinzani butu. Kina Mwangosi wameteswa na kuuwawa wakati wa utawala wa nani? Vipi vifo vya kule Zanzibar? vipi yale mabomu yaliouwa watu kule Soweto Arusha? Vipi kina Lipumba kujaribu kuandamana na kuambulia kipigo kilichosababisha avunjwe mkono wakati wa utawala wa Kikwete? I mean tawala zote wapinzani walichezea kichapo na wapo waliouwawa pia, ila kwa vile wanachama walikuwa na imani na upinzani basi walikuwa tayari kufa kuliko kuendelea kutawaliwa na CCM. Ila baada ya kile kilichofanyika 2015, wote waliokuwa tayar kuweka maisha yao hatarini waliamua kuanza kufikiria mara mbili mbili kuhusu upinzani waliokuwa wanaupigania na hapo wengi wakaamua kuachana na mambo ya kisiasa kwani waliona siasa za Tanzania ni za kinafiki tu.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu wana JF wenzangu na watanzania wenzangu, ili chama cha CCM kiweze kushindwa katika uchaguzi mkuu wa 2025 au 2030, yanahitajika mambo matatu.

1) Kwanza: kinahitajika chama imara cha upinzani chenye sera nzuri, zinazoeleweka na kutekelezeka. Chama hicho kiwe na sura ya kitaifa, kiwe na viongozi wakweli, wenye maono na misimamo thabiti ya kuikomboa nchi.

Kiwe na mifano hai ya utekelezaji wa sera zake kupitia chama husika ili kiweze kuaminika machoni mwa watanzania wengi. a) sio mtu useme chama chetu kina misingi ya demokrasia wakati mwenyekiti wa chama ambacho kingekuwa mfano wa demokrasia hiyo ana miaka 20 madarakani.

b) Sio mtu useme chama chetu ni cha maendeleo, wakati wanaoendelea katika chama ni mwenyekiti wa chama taifa na genge lake, huku chama chenyewe kikiwa hakina hata ofisi ya kufanyika mkutano wa ndani.

c) Sio mtu useme chama chetu kitasimamia utawala bora na haki, huku ndani ya chama chenyewe hakuna anaeweza kuongelea lolote mbele ya mwenyekiti wa chama au makamu wake.

2) Pili: Anahitajika kuchaguliwa mgombea ambae hana makandokando ya uongo, uoga, unafiki na mwenye uwezo wa kweli wa kusimamia sera za chama chake bila kuyumbishwa na mtu yoyote iwe ndani ya chama au nje ya chama.

a) Sio kiongozi anakuwa na kauli za kilaghailaghai kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa, na kiuongozi (kama tunavyoona hapo chini pichani) bila kujali madhara yatokanayo na ulaghai huo. Mtu wa aina hii ni ngumu kuchaguliwa maana watanzania wa sasa sio wale wa 2001, kule Zanzibar ambapo watu walikufa, kujeruhiwa na kufungwa, huku muhusika aliepiganiwa (aliekuwa katibu mkuu wa chama, na mgombea wa upinzani) akiwa Saudia Arabia kula tende na maswaiba zake.

Mgombea akiwa hana msimamo thabiti wa kusimamia sera au hoja zake mwenye, basi hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Marekani ikija kusimamia uchaguzi bado ataangukia pua tu.

3) Tatu: Tume huru isiyoegemea upande wowote wa kisiasa. Tume iwe na viongozi kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa na kiraia ili kujenga sura ya utaifa katika tume hiyo.

Ni hayo tu ninayoyaona mimi, katika kuijenga Tanzania bora zaidi ya kesho.

Asanteni sana.

View attachment 2319901View attachment 2319903View attachment 2319904View attachment 2319911View attachment 2319912
Haya magaidi hayawezi ingia ikulu pale. Ikulu ni mahala patakatifu alisikika akisema mzee mmoja.
 
Kabisa, CCM watu hawaipendi, ila ukikaa vizuri ukifikiria kwa kina unaona bora niwape kura CCM au nisipigie kura chama chochote.
Upinzani upo katika hali mbaya sana, pamoja na kujaza chawa mitandaoni lkn bado haisaidii chama kusonga mbele.
 
Mbona hatuulizi juu Mzee Mrema kwani naye ana muda mrefu sana ktk harakati zake.
Kwanini iwe shida kwa huyu anayejenga Tasisi nakuonekana imara katka ushindani kwani tukumbuke ndo mshindani wa kweli na wa mfano wa kuigwa.
Tukumbuke sio mwepesi ndo maana hoja zinazomhusu haziishi kutoka kwetu.
Mfano ni madhila aliyoyapitia yy na wanaomzunguka.
Je ni nani mwingine aliyeyapitia aliyoyapitia?
Tuje na hoja dhabiti tutaeleweka vizuri sana.
Mleta mada angekuwa ni mtu makini angekusoma kwa uangalifu zaidi ya kukupa 'like' kama alivyofanya hapa.

Kama kuna mtu aliyejitoa kikwelikweli (hata kama hilo halikuwa lengo na tegemeo mwanzoni mwa harakati zake), mtu huyu anayesemwa hapa kajitoa hasa. Lakini pamoja na kujitoa huko, watu aliotegemea wataelewa maana ya kujitoa kwake ikawa kama hawana habari naye. Hili linakatisha tamaa mtu yeyote yule, hata kwenye siasa.

Kuna kitu/jambo ambalo CHADEMA hawajalitambua vizuri kuhusu waTanzania, na kwa nini CCM inaonekana kuendelea kuwashikilia kama wapo jela.
CHADEMA inawapasa kudadisi na kuelewa ni jambo gani hilo.
Pamoja na ubovu wooote ilioufikia CCM, lakini waTanzania ni kama wameshikwa na sumaku wasiweze kujinasua. Jibu la CHADEMA na vyama vingine vya upinzani lipo hapo.
Wajiulize wenyewe, na wakilijua, CCM inakwisha.

Ukweli ni kwamba CCM imebaki kama mzoga tu, unaosubiri kufukiwa.
 
Ni hayo tu ninayoyaona mimi, katika kuijenga Tanzania bora zaidi ya kesho.
Upungufu wa mada yako ni kama ifuatavyo.

1. Kichwa cha mada hakiendani na yaliyomo ndani ya mada yenyewe. Kichwa kinasema "mtu" maelezo yanazungumzia chama.

2. Mada inajikita kushambulia chama kimoja cha upinzani, na kusahau kwamba kuna vyama vingi vya upinzani.
Kuelekeza nguvu zako zote kwenye hicho chama kimoja maana yake ni kwamba hicho ndiyo chama kinachokutia hofu zaidi ya kukiondoa chama unachokipigania wewe.

3. Kuondolewa kwa CCM sasa hivi hakuhitaji hayo yote uliyoyazungumzia ndani ya mada. Kule tu kukiondoa CCM kwa njia yoyote ile ni lengo linalojitosheleza kabisa kutokana na jinsi chama hicho kilivyogeuka kuwa adui wa waTanzania.

Haihitajiki hata kidogo chama kiwe na sera na mengi mengine unayolemba hapa.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu wana JF wenzangu na watanzania wenzangu, ili chama cha CCM kiweze kushindwa katika uchaguzi mkuu wa 2025 au 2030, yanahitajika mambo matatu.

1) Kwanza: kinahitajika chama imara cha upinzani chenye sera nzuri, zinazoeleweka na kutekelezeka. Chama hicho kiwe na sura ya kitaifa, kiwe na viongozi wakweli, wenye maono na misimamo thabiti ya kuikomboa nchi.

Kiwe na mifano hai ya utekelezaji wa sera zake kupitia chama husika ili kiweze kuaminika machoni mwa watanzania wengi. a) sio mtu useme chama chetu kina misingi ya demokrasia wakati mwenyekiti wa chama ambacho kingekuwa mfano wa demokrasia hiyo ana miaka 20 madarakani.

b) Sio mtu useme chama chetu ni cha maendeleo, wakati wanaoendelea katika chama ni mwenyekiti wa chama taifa na genge lake, huku chama chenyewe kikiwa hakina hata ofisi ya kufanyika mkutano wa ndani.

c) Sio mtu useme chama chetu kitasimamia utawala bora na haki, huku ndani ya chama chenyewe hakuna anaeweza kuongelea lolote mbele ya mwenyekiti wa chama au makamu wake.

2) Pili: Anahitajika kuchaguliwa mgombea ambae hana makandokando ya uongo, uoga, unafiki na mwenye uwezo wa kweli wa kusimamia sera za chama chake bila kuyumbishwa na mtu yoyote iwe ndani ya chama au nje ya chama.

a) Sio kiongozi anakuwa na kauli za kilaghailaghai kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa, na kiuongozi (kama tunavyoona hapo chini pichani) bila kujali madhara yatokanayo na ulaghai huo. Mtu wa aina hii ni ngumu kuchaguliwa maana watanzania wa sasa sio wale wa 2001, kule Zanzibar ambapo watu walikufa, kujeruhiwa na kufungwa, huku muhusika aliepiganiwa (aliekuwa katibu mkuu wa chama, na mgombea wa upinzani) akiwa Saudia Arabia kula tende na maswaiba zake.

Mgombea akiwa hana msimamo thabiti wa kusimamia sera au hoja zake mwenye, basi hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Marekani ikija kusimamia uchaguzi bado ataangukia pua tu.

3) Tatu: Tume huru isiyoegemea upande wowote wa kisiasa. Tume iwe na viongozi kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa na kiraia ili kujenga sura ya utaifa katika tume hiyo.

Ni hayo tu ninayoyaona mimi, katika kuijenga Tanzania bora zaidi ya kesho.

Asanteni sana.

View attachment 2319901View attachment 2319903View attachment 2319904View attachment 2319911View attachment 2319912
Uzi tayari kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom