Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 25,258
- 48,589
- Thread starter
- #41
Duh ase inasikitishaMkuu vijana wengi ndivyo walivyo. Kuna mdada fulani aliniomba nimuunge na watu wawili waliosoma au wenye experience ya prograamming na wanaweza kuonyesha hilo kwenye cv zao.
Nikatafuta vijana nikawambia waandae cv. Vijana wenyewe siwafahamu ila nawaonaga kwenye group fulani wakisema wao ni wahitimu wanapiga programming.
Wakanitumia cv hazionyeshi wao kama ni programmers. Nikawambia mdada anataka uonyeshe kwenye cv, lakini wakawa hawaelewi.
Mwisho nikawatumia wote cv yangu ambayo haihusiani na mambo hayo ila tu kuwaonyesha jinsi inavyoonyesha experience nliyo nayo.
Baada ya hapo hakuna aaliyeandika wakawa wanasema kuwa mdada anazingua kama ana kazi awaite otherwise mzinguaji tu.
Mwisho mdada nikamuunga na jamaa fulani mkenya na akaweza mpata programmer mwingine wakawa wawili akafanya nao kazi mpaka leo wanafanya wote kazi toka mwezi wa pili.