Mtu kauza kiwanja. baada ya kupokea hela kagoma kutransfer umiliki wa kiwanja chake kwenda kwa mnunuzi

Huyo mashtaka yote yanamuhusu.

Muhimu sana muwe na wakili.
 
Kesi ni jinai, huyo katenda wizi wa kuaminiwa
 
Sharia za Tanzania haziruhusu diwani kusimamia mauziano ya ardhi, huo mkataba ni batili
 
Nilipe milioni 5 nikupe majibu
Majibu yanapatikana kwenye Sheria ya Usajili wa ardhi, na Sheria ya ardhi, land survey act
-ukinunua ardhi jaribu kuonana na Wakili,au mpima ardhi,
  • hayo mauzo ni batili 100%, na anaweza kukosa haki yake
  • unajua utaratibu wa kugawanya ardhi?
 
Wakati mwingine mwambie Amina asinunue mali kienyeji. Aende kwa mwanasheria waandike mtakaba na kupewa taratibu zote muhimu
Aisee mwasibu, umeandika kitu cha maana Sana, hawa watu huwa hawataki kutushirikisha Land surveyors kwenye ununuzi wa ardhi, wakipata majanga ndio wanakumbuka umuhimu wa Land surveyors, na hapo unaweza kukuta diwani kamlipa 10% halafu mkataba wenyewe batili
 
Lipia pesa kwa mpima ardhi usaidiwe

Mpima ardhi anahusika vipi kwenye mambo ya kisheria.

Hakuna mgogoro wowote wa kuhusu upimaji wa ardhi.

Pia manispaa zote zina idara za wapimaji ardhi. Kama ni mgogoro unaohusu upimaji. Manispaa wanasolve wenyewe
 
Mpima ardhi anahusika vipi kwenye mambo ya kisheria.

Hakuna mgogoro wowote wa kuhusu upimaji wa ardhi.

Pia manispaa zote zina idara za wapimaji ardhi. Kama ni mgogoro unaohusu upimaji. Manispaa wanasolve wenyewe
Wapima ardhi tunasoma sheria za ardhi zote,
Kama ulikuwa unajua kuwa manispaa kuna idara ya upimaji ardhi kwa nini hamkwenda kwa wakati ili mfanye subdivision ya ardhi?
 
Wapima ardhi tunasoma sheria za ardhi zote,
Kama ulikuwa unajua kuwa manispaa kuna idara ya upimaji ardhi kwa nini hamkwenda kwa wakati ili mfanye subdivision ya ardhi?

Utafanya vipi subdivision ya ardhi bila ku surrender hati ya mwanzo ?

Soma hoja zilizowekwa kwenye thread kwanza..

Pia hili ni jukwaa la sheria

Mambo ya sheria yanaletwa humu kuwauliza mambo ya sheria.

Hili sio jukwaa la surveyors
 
Hivi diwani naye ni ofisa wa viapo?
Huo mkataba ulisajiliwa?
Huo mkataba mlilipa Stampy duty?
Kuna uwezekano mkubwa hicho kielelezo ambacho ni mkataba wa mauziano kisipokelewe mahakamani na kesi yako inakuwa imeishia hapo, i.e ukashindwa kesi. (Kielelezo hicho ambacho ni mkataba hakitapokelewa)
Tafuta wakili umlipe pesa akisaidie, ukienda mwenyewe utawekewa mapingamizi na kesi inafutwa unabaki na hasara juu ya hasara
 
Funzo

Usinunue kiwanja bila HATI

Usinunue kiwanja kwa malikauli.


Daaah unaweza UA mtu aisee

Watu wanaudhi sana sana aisee.

Siku hizi UAMINIFU UNAPATIKANA KWA TABU SANA.
 
Mmechemka sana mkuu
Aridhi iliopimwa haigawanywi kizembe namna hiyo

Hapo inabidi uongee vizuri na polisi apewe kesi ya UTAPELI
Junai ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu

Akikaa ndani wiki moja atatia akili tu
 
Hapo kikubwa cha kufanya ni Amina kuingia site na kuanza kuendeleza eneo lake......haya mambo ya sheria sijui transfer sijui nn yatampotezea muda, yaani afanye akalitwae eneo lake mazima mazima, then asikilizie huyo Juma anasemaje.....kama akienda mahakamani basi na huyo dada ataenda na makaratasi yake yaliyomfanya mpaka akalimiliki na kuliendeleza hilo eneo......N.B Huu ni ushauri wa kimtaa tu.
 
Na huo ushauri wa kimtaa ndiyo wenyewe huo, hukumu lazima iheshimiwe na kila mtu!!
 
Mkataba siyo null and void ila ni unenforceable.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…