Mtu kauza kiwanja. baada ya kupokea hela kagoma kutransfer umiliki wa kiwanja chake kwenda kwa mnunuzi

habari wadau.

wataalamu wa sheria naomba majibu yenu.

JUMA anamiliki kiwanja chenye sqm 1200.

amepatwa na shida ameamua kumuuzia AMINA sehemu ya kiwanja chake. kamuuzia sqm 400 na yeye JUMA amebaki na Sqm 800.

wameandikishana kwenye mkataba wao wa makubaliano. kuwa baada ya kupokea hela JUMA ata surrender hati yake ya mwanzo yenye sqm 1200 na atagawanya kiwanja chake ili AMINA apate hati yenye Sqm 400 alizouziwa na yeye JUMA apate hati mpya yenye sqm 800.

mauziano yakafanyika na JUMA akaenda kulipwa pesa zake na AMINA via BANK.

baada ya JUMA kupokea hela zake akamuahidi AMINA wataanza mchakato wa kugawanya hati wiki ijayo.

ghafla JUMA akasafiri kwenda kijijini kwao kwamba ana dharura ya kuuguza mgonjwa.

akakaa huko kijijini mwezi mzima na baada ya kurudi nyumbani kwake amegoma kutoa ushirikiano kwenye kugawanya hati hiyo.

AMINA akaamua kwenda kumfungulia shauri Baraza la Ardhi kata kwamba JUMA amegoma kukabidhi kiwanja alichokiuza na haeleweki sababu ni nini.

JUMA alivyoulizwa kwa nini hafanyi hivyo. anadai aliuza kwa bei ndogo na alikuwa na mapepo ndiyo yalimfanya auze. hivyo anatafuta hela kwa sasa akizipata atamrudishia AMINA hela zake.

baraza la ardhi kata limemuambia AMINA aende akadai haki yake mahakama za juu. Baraza limempa AMINA cheti cha kushindwa kusuluhisha mgogoro huo.

AMINA amechanganyikiwa akamfungulie kesi ya aina gani ? maana kila mtu anashauri kivyake

1. Je AMINA aende baraza la ardhi la wilaya ajkamfungulie kesi ya kudai ardhi aliyouziwa

2. Aende mahakama ya wilaya aende akamfungulie kesi ya madai kwa uvunjanji wa mkataba wa mauziano

3. Aende akamfungulie kesi ya jinai ?

ama aende mahakama gani na akamfungulie kesi ya aina gani ?

wanasheria ni vizuri mkatoa maoni yenu. mtu kama huyu kesi gani ni sahihi kumfungulia ?
Huyo mashtaka yote yanamuhusu.

Muhimu sana muwe na wakili.
 
Kesi ni jinai, huyo katenda wizi wa kuaminiwa
 
1.Mkataba wake ulisimamiwa na diwani wa kata ya eneo ambao kiwanja lilipo

2. Kiwanja chake waliuziana bila hizo requeast kufanyika. Maana huyo juma hizo sqm 1200 alizipata baada ya kurithi kiwanja kilichopimwa na serikali. Kipo kwenye ramani ya mipango miji ya mwaka 1988. Na kina hati ya serikali
Sharia za Tanzania haziruhusu diwani kusimamia mauziano ya ardhi, huo mkataba ni batili
 
Nilipe milioni 5 nikupe majibu
Majibu yanapatikana kwenye Sheria ya Usajili wa ardhi, na Sheria ya ardhi, land survey act
-ukinunua ardhi jaribu kuonana na Wakili,au mpima ardhi,
  • hayo mauzo ni batili 100%, na anaweza kukosa haki yake
  • unajua utaratibu wa kugawanya ardhi?
 
Wakati mwingine mwambie Amina asinunue mali kienyeji. Aende kwa mwanasheria waandike mtakaba na kupewa taratibu zote muhimu
Aisee mwasibu, umeandika kitu cha maana Sana, hawa watu huwa hawataki kutushirikisha Land surveyors kwenye ununuzi wa ardhi, wakipata majanga ndio wanakumbuka umuhimu wa Land surveyors, na hapo unaweza kukuta diwani kamlipa 10% halafu mkataba wenyewe batili
 
Lipia pesa kwa mpima ardhi usaidiwe

Mpima ardhi anahusika vipi kwenye mambo ya kisheria.

Hakuna mgogoro wowote wa kuhusu upimaji wa ardhi.

Pia manispaa zote zina idara za wapimaji ardhi. Kama ni mgogoro unaohusu upimaji. Manispaa wanasolve wenyewe
 
Wapima ardhi tunasoma sheria za ardhi zote,
Kama ulikuwa unajua kuwa manispaa kuna idara ya upimaji ardhi kwa nini hamkwenda kwa wakati ili mfanye subdivision ya ardhi?
 
Aisee mwasibu, umeandika kitu cha maana Sana, hawa watu huwa hawataki kutushirikisha Land surveyors kwenye ununuzi wa ardhi, wakipata majanga ndio wanakumbuka umuhimu wa Land surveyors, na hapo unaweza kukuta diwani kamlipa 10% halafu mkataba wenyewe batili
Wapima ardhi tunasoma sheria za ardhi zote,
Kama ulikuwa unajua kuwa manispaa kuna idara ya upimaji ardhi kwa nini hamkwenda kwa wakati ili mfanye subdivision ya ardhi?

Utafanya vipi subdivision ya ardhi bila ku surrender hati ya mwanzo ?

Soma hoja zilizowekwa kwenye thread kwanza..

Pia hili ni jukwaa la sheria

Mambo ya sheria yanaletwa humu kuwauliza mambo ya sheria.

Hili sio jukwaa la surveyors
 
Hivi diwani naye ni ofisa wa viapo?
Huo mkataba ulisajiliwa?
Huo mkataba mlilipa Stampy duty?
Kuna uwezekano mkubwa hicho kielelezo ambacho ni mkataba wa mauziano kisipokelewe mahakamani na kesi yako inakuwa imeishia hapo, i.e ukashindwa kesi. (Kielelezo hicho ambacho ni mkataba hakitapokelewa)
Tafuta wakili umlipe pesa akisaidie, ukienda mwenyewe utawekewa mapingamizi na kesi inafutwa unabaki na hasara juu ya hasara
 
Funzo

Usinunue kiwanja bila HATI

Usinunue kiwanja kwa malikauli.

Daaah unaweza UA mtu aisee

Watu wanaudhi sana sana aisee.

Siku hizi UAMINIFU UNAPATIKANA KWA TABU SANA.
 
Mmechemka sana mkuu
Aridhi iliopimwa haigawanywi kizembe namna hiyo

Hapo inabidi uongee vizuri na polisi apewe kesi ya UTAPELI
Junai ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu

Akikaa ndani wiki moja atatia akili tu
 
Hapo kikubwa cha kufanya ni Amina kuingia site na kuanza kuendeleza eneo lake......haya mambo ya sheria sijui transfer sijui nn yatampotezea muda, yaani afanye akalitwae eneo lake mazima mazima, then asikilizie huyo Juma anasemaje.....kama akienda mahakamani basi na huyo dada ataenda na makaratasi yake yaliyomfanya mpaka akalimiliki na kuliendeleza hilo eneo......N.B Huu ni ushauri wa kimtaa tu.
 
Na huo ushauri wa kimtaa ndiyo wenyewe huo, hukumu lazima iheshimiwe na kila mtu!!
 
Huwezi kuiuza registered land bila muhuri wa kamishna wa viapo. So, lazima kuwe na drafting ya affidavit iambatane na sale agreement. Diwani yeye siyo kamishna wa viapo. Kwa hiyo, hiyo contract is null na haikufuata Sheria.
Pili, hiyo request ikikataliwa? Huko mkataba upo kinyume cha Sheria. Kwa sababu labda hilo eneo lilitakiwa liwe medium density, wewe unaligeuza low density bila approval ni kosa.
Halafu unahitaji hati ya nini? Yaani Amina apewe hati ya Sqm 1200 wakati kanunua Sqm 400? Sijapata mantiki yake.
All in all, Kuna makosa mengi upande wa mnunuzi.
Kwa hiyo atarudishiwa tu hela zake, hiyo contract is inoperable.
Mkataba siyo null and void ila ni unenforceable.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom