Mtu mjinga sana anaweza kupata mafanikio makubwa katika maisha?

Kwa tafsiri hii,ina maana wale wote ambao hawajafanikiwa ni Wajinga?
Naomba ufafanuzi mkuu.
No - hiyo itakuwa ni Hasty Generalization.

Mtu unaweza ukawa very Intelligent na hujafanikiwa ila ukawa Mentality perfect, ukaweka malengo makubwa na kuongeza Nidhamu means siku1 utakuja kufanikiwa.

Mjinga anayezungumzwa hapa ni zwazwa, Mtu ambaye yuko Comfortable, Hana malengo, Anaishi ishi tu, Huyu kamwe haji kufanikiwa.

Mjinga anaweza kufanikiwa kupitia kujifunza ili kuuondoa huo ujinga.

cc: The ice breaker
 
Mtu mjinga sana anaweza kupata mafanikio makubwa katika jamii mfano kuwa tajiri au mtu mkubwa sana katika siasa, biashara na sanaa katika jamii?

msome mtu anayeitwa Timothy Dexter, the richest and most foolish person who ever lived. nahis hata youtube kuna video zimemuelezea. huyo deter alishaamua kuandika kitabu cha maisha yake. ni vituko vitupu

kufanikiwa ni fursa ambayo wakati mwingine inakuja kwa bahati with zero effort, alishawahi kupeleka vizalisha joto kwenye nchi yenye joto na akauza.... yaani ni sawa uanzishe biashara ya kupeleka mabarafu north pole mahalia mabapo 90% iko covered na barafu lakini wewe ugandishe ice blocks kwenye freezers unazisafirisha na meli hadi north pole na bado ufanikiwe kuyauza
 
tafsiri ya ujinga kwanza
Ujinga ni hali ya kutokujua, kutokuelewa, au kutojua mambo muhimu ambayo yanahitaji ufahamu.

Inahusisha kutokuwa na elimu, maarifa, au ufanisi katika kufanya maamuzi au kuchukua hatua kwa njia ya busara.

Ujinga unaweza pia kumaanisha kutokuwa na uwezo wa kujieleza au kutatua matatizo kwa njia ya akili.

Hata hivyo, ujinga si kitu cha kudumu; mtu anaweza kujifunza na kuboresha maarifa yake ili kuondokana na ujinga.
 
Kama una IQ chini ya wastani au ndogo sana sidhani hata kama ukijifunza unaweza kuondokana na ujinga.
 
No - hiyo itakuwa ni Hasty Generalization.

Mtu unaweza ukawa very Intelligent na hujafanikiwa ila ukawa Mentality perfect, ukaweka malengo makubwa na kuongeza Nidhamu means siku1 utakuja kufanikiwa.

Mjinga anayezungumzwa hapa ni zwazwa, Mtu ambaye yuko Comfortable, Hana malengo, Anaishi ishi tu, Huyu kamwe haji kufanikiwa.
Ujinga upo wa aina nyingi na kila mtu ana ujinga wake,binafsi sioni kama ni sawa kufanya kua kipimo cha kufanikiwa kimaisha ( Yani kutumia kipimo kimoja tu) ndio akili,

Unaweza ukawa umefanikiwa kimaisha ila ukawa unadhulumu mali za watu,unaua watu,unatapeli watu,hutendi haki na mengineyo,huu nao pia ni ujinga,

Mleta mada angetumia neno Mvivu badala ya Mjinga hapo ingeleta maana,

Kila Binadamu ana ujinga wake,nobody is perfect.
 
Ujinga upo wa aina nyingi na kila mtu ana ujinga wake,binafsi sioni kama ni sawa kufanya kua kipimoja cha kufanikiwa kimaisha ( Yani kutumia kipimo kimoja tu) ndio akili,

Unaweza ukawa umefanikiwa kimaisha ila ukawa unadhulumu mali za watu,unaua watu,unatapeli watu,hutendi haki na mengineyo,huu nao pia ni ujinga,

Mleta mada angetumia neno Mvivu badala ya Mjinga hapo ingeleta maana,

Kila Binadamu ana ujinga wake,nobody is perfect.
Kama ujinga uko wa aina nyingi basi mtu mmoja anaweza kuwa na ujinga wa aina nyingi pia au hata aina zote kabisa.
 
Mtu mjinga sana anaweza kupata mafanikio makubwa katika jamii mfano kuwa tajiri au mtu mkubwa sana katika siasa, biashara na sanaa katika jamii?
Inawezekana, pia inategemea na wakati, utawala, technologia, vipaumbele vya kiongozi wakati huo.

Mwijaku wakati wa Nyerere angeonekana mjinga ila leo ni role model. Sababu ya Rais wa sasa, vipaumbele vyake ni machawa, technologia ya mitandao nk.
 
Kama una IQ chini ya wastani au ndogo sana sidhani hata kama ukijifunza unaweza kuondokana na ujinga.
Hapo sasa umechanganya vitu viwili na kutaka kuvifanya kiwe kiwe kitu kimoja.

Ujinga ni kutokujua au kutokuwa na maarifa katika maeneo fulani, Mfano mimi sijui kuendesha ndege ni Mjinga kwenye eneo hilo.

Low IQ (akili ya chini) ni kipimo cha uwezo wa akili, kinachohusiana na jinsi mtu anavyoweza kufikiri na kutatua matatizo, Hili ni tatizo la moja kwa moja la kiakili.

Ujinga unaweza kuboreshwa kwa kujifunza, lakini IQ ya mtu ni kipimo cha asili cha uwezo wa akili, haibadiliki.
 
Kama ujinga uko wa aina nyingi basi mtu mmoja anaweza kuwa na ujinga wa aina nyingi pia au hata aina zote kabisa.
Na ukubali pia kua hata kufanikiwa kimaisha sio kipimo cha kutokua mjinga pia,unaweza ukafanikiwa ila still na wewe ukawa una ujinga wako pia.
 
Hapo sasa umechanganya vitu viwili na kutaka kuvifanya kiwe kiwe kitu kimoja.

Ujinga ni kutokujua au kutokuwa na maarifa katika maeneo fulani, Mfano mimi sijui kuendesha ndege ni Mjinga kwenye eneo hilo.
Hapana, unachanganya mambo. Kotokujua jambo fulani hasa linalohusiana na taaluma sio ujinga au kuwa mjinga, ni kwamba hujui tu hilo jambo.
 
Ujinga upo wa aina nyingi na kila mtu ana ujinga wake,binafsi sioni kama ni sawa kufanya kua kipimo cha kufanikiwa kimaisha ( Yani kutumia kipimo kimoja tu) ndio akili,

Unaweza ukawa umefanikiwa kimaisha ila ukawa unadhulumu mali za watu,unaua watu,unatapeli watu,hutendi haki na mengineyo,huu nao pia ni ujinga,

Mleta mada angetumia neno Mvivu badala ya Mjinga hapo ingeleta maana,

Kila Binadamu ana ujinga wake,nobody is perfect.
Mtoa maada hajataja ujinga kwenye eneo Specific, Amejenga hoja kupitia neno ujinga kiujumla.

Ujinga ni kutokujua au kutokuwa na maarifa katika maeneo fulani.

Kama umefanikiwa katika eneo fulani inamaanisha ulipata maarifa kwenye eneo hilo ukaondoa ujinga then ukachukua hatua, ukafanikiwa.

Hayo matendo ya udhulumaji, uuaji na utapeli baada ya wewe kufanikiwa ni sahihi kabisa, si matendo ya kiungwana.

Mafanikio ya kweli ni kuuondoa ujinga huku ukitenda matendo ya busara katika jamii.
 
Mtoa maada hajataja ujinga kwenye eneo specific , Amejenga hoja kupitia neno ujinga kiujumla.

Ujinga ni kutokujua au kutokuwa na maarifa katika maeneo fulani.

Kama umefanikiwa katika eneo fulani inamaanisha ulipata maarifa kwenye eneo hilo ukaondoa ujinga then ukachukua hatua, ukafanikiwa.

Hayo matendo ya udhulumaji, uuaji na utapeli baada ya wewe kufanikiwa ni sahihi kabisa, si matendo ya kiungwana.

Mafanikio ya kweli ni kuuondoa ujinga huku ukitenda matendo ya busara katika jamii.
Kama unakubali kua mleta mada hajataja ujinga kwenye eneo specific basi unatakiwa ukubaliane na ujinga utakaotajwa kwenye maeneo mengine pia,
Ndio tunarudi kule kule kua kila mtu ana ujinga wake,nobody is perfect.
 
Back
Top Bottom