OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,701
- 11,920
Utajiri ni hali ya kuwa na mali au pesa nyingi . Mara nyingi utajiri hupimwa kwa wingi wa pesa alizonazo mtu mfano , kiwango kikianzia milioni 100 mtu huyo huitwa milionea, kikianzia milioni 1000 mtu huyo huitwa bilionea, Mtu mwenye utajiri huitwa TAJIRI na mtu asiye na utajiri (mali au pesa nyingi) huitwa MASIKINI.
Unyonyaji ni kitendo cha kukamua pesa au mali za watu wengine. Kwa maana hiyo tunaweza kusema tajiri ni mtu anaye kamua pesa au mali za mtu mwingine kwa lengo la kujinufaisha, ukamuaji unaweza kuwa ni halali kisheria au unao vunja sheria, ktk maada hii nitazungumzia ukamuaji usiovunja sheria.
Mfano: Kijiji A kikiwa na upungufu wa chakula mfano mahindi, mimi nikaenda kijiji B ambacho kinamahindi mengi, nikanunua kwa shilingi 5 kila gunia, nikarudi kijiji A nikawauzia kwa shilingi 10 kila gunia, nitakua nimekamua shilingi 5 kwa kila gunia.
Mfano: Nikizalisha juisi moja kwa gharama ya shilingi 1, nikamuuzia mwenye kiu kwa shilingi 5, ninakua nimekamua shilingi 4. Kumbuka katika mifano yote miwili hakuna mahali ambapo sheria imevunjwa.
Ili nitengeneze Shilingi 100 inabidi niwauzie watu wasiopungua 20 ktk mfano namba moja, kiuhalisia kila mtu anakuwa amenipa shilingi 5 ni sawa na kusema amepoteza shilingi tano.

Ili mtu yeyote apate pesa ni lazima mtu mwingine apoteze pesa. Tajiri akipata juwa kuna masikini kapoteza, mtu yeyote akipata juwaa kuna mtu kapoteza.
Ni kama vile mzani jinsi unavyofanya kazi
Ukitengeneza bilionea mmoja unakuwa umetengeneza masikini elfu moja
Kanuni haidanganyi, inafanya kazi popote pale duniani, inaleta matokeo yale yale
Nawasilisha