Mtu mmoja akiwa bilionea, watu elfu moja huwa masikini

SI KWELI.

KABLA YA UWEPO WA FEDHA WALIKUWEPO MATAJIRI NA MASIKINI.
Sijajua kama umesoma kwa kutafakari nilichokiandika mkuu, maana nimeeleza wa wino mweusi kabisa kuwa utajili ni hali ya kuwa na mali au pesa nyingi. Au hujaelewa mkuu? Hujui kuwa kabla ya uwepo wa pesa dhahabu ilitumika kama pesa,
Tafsiri ya utajiri sio pesa bali ni uwezo wa akili wa kutawala rasilimali zinazokuzunguka kulinganisha na viumbe wengine.
Unachanganya mambo mkuu, hapa hujatoa maana ya utajiri umetoa maana ya UONGOZI, kama unabisha google maana ya uongozi kisha ulinganishe na ulichokiandika
Mtoto wa Masai anatawala watoto wa ng'ombe na baba zao si kwa sababu ni milionea ila uwezo wake wa akili upo juu kulinganisha na ng'ombe.
Hapa unaonyesha utofauti kati ya binadamu na ngo'mbe sioni uhusiano wa haya maelezo na hii thread
Utajiri ungekuwa ni pesa ungerithishwa daima,
Rejea maana ya utajiri niliyoiandika hii ni ya kwako
hakuna matajiri wangeibuka kutoka katika masikini.
Duh
Utajiri ni uwezo wa akili, Pesa ni matokeo ya kuwa tajiri au masikini. Kabla ya kuwa na pesa matajiri na masikini walikuwepo.
Yaani hata sijaelewa ulikusidia kufikisha ujumbe gani
 
mi nauliza hivi mimi forex trader, nikimula broker akaniingizia tsh kwenye account yangu ya bank, je nitakuwa nimewakamua watanzania au??? au nitakuwa nimewakamua watu wote wanaotumia USD?? hapa sijaelewa, maaana namkamua broker, dola zake then yeye ananiingia kama tsh kwenye account yangu bank


je masikini wataadhirika vipi na mtonyo wangu alionipa broker?

kingine naulizaa je, hizo pesa nitakazopata baaada ya kuzitoa bank na kupewa hardcopy, kwamba na mimi nakuwa nimenyakuwa pesa iliyokuwaa kwenye mzungukoo?? je serikari inaconsider na sisi maforex trader tunaweza affect mzunguko wa fedhaa kwa fedha zote zilizoingizwa na BOT kununua goods na services?

je mkopo tuliopewa trioni 1.3 na Bank kuu ya dunia, ni kwamba sisi hatuna pesa nchini hadi kufikia kupewa dolaa??
 
kama unachokisema mleta mada ni sahihi basi nchi kama USA yenye mabilionea wengi si ungekuta ina masikini wengi kuliko hata TZ[emoji23][emoji23]
USA wanakamua mataifa maskin.
Hata mabilionea wao wanakamua raia walioko mataifa maskin mf Zuckerburg watumiaji wengi wa FB wapo mataifa maskin kwasababu mda wote wenyewe ni kuchat hawafikilii kufanya kazi.
 
Bidhaa nyingi tunaagiza kaka,hivyo tunapoteza hela nyingi kwenda abroad,hela tunayopata tukiexport bidhaa ni ndogo sana.Ili kusawazisha mambo tunakopa,hatuwezi kuprint hela.

BALANCE OF PAYMENTS
Export=Import
Import>export=deficit-lazima ukope hapa.
Import<export=surplus-hapa maisha safi tu.
 
USA wanakamua mataifa maskin.
Hata mabilionea wao wanakamua raia walioko mataifa maskin mf Zuckerburg watumiaji wengi wa FB wapo mataifa maskin kwasababu mda wote wenyewe ni kuchat hawafikilii kufanya kazi.
Sisi ni miradi ya wazungu.Machinga ni Madalali wao,wana soko la uhakika afrika.Kila bidhaa wanatuuzia,Wao ni kuzalisha na kula bata kwani soko lao la mafukara lipo,wanaishi kwa migongo yetu.
 
Tajiri anacheza na market demand mkuu.Kwa hiyo hata hela za kina Mo au bakhresa unaweza ukazivuta mkuu,endapo utaanzisha profitable venture au business
Hiyo concept yako ina walakini kiuchumi mkuu.Hao matajiri nao wana expenses,wanalipa mishahara,wanafanya shopping,so hela lazima irudi kwenye mzunguko,so mtu yeyote ana probability ya kutajirika at any time.
 
Hamna tabia inayokufanya kuwa tajri bali ni vyanzo vyako vya mapato

Mfano ukipewa laki ukiwekeza vzuri itaendelea kuwepo. Na ukienda kununua jens ndo itakuwa imeisha hyo
Hujaelewa
 
safi sanaa mkuu, ila nijibu haya maswali

1.umesema tumekopa kwasababu export ni ndogo kuliko import, sasa kumbe tulipopewa USD millioni 556 nazani, hizo pesa ndo tuseme kwamba tunaongeza foreign currency reserve ama??? na tsh yetu tunaizuia kutoka nje, so inakuwa bado inathamani, sasa kumbuka hapo tuna riba kwenye huo mkopo so tutarudishaa kiasi zaidi ya hicho tulichopewa, so tutakuwa tumekamuliwaa tsh kiasi flani, sasa najiulizaa nchi inatumia njia gani, kupata hizo fedhaa ili kulipa mkopo??? si unajua tena pesa zote zilizopo kwenye mzunguko zinatoka bank kuu, na hela kwenye mzunguko hazitaongezekaa kwa njia yoyote zaidi ya zile zilizoprintiwaa na kube assured na BOT, namanishaa BOT, haiwezi kurprint pesa, na kuzitiaa kwenye mzunguko halafu baadae ukasema zimeongezeka zaidi ya zile zilizoprintiwaa, sasa hawa BOT watarudisha vipi hela ya riba ya mkopo tuliopata kutoka bank kuu.???

2.nauliza tena hivi pesa zote kwenye mzunguko si zinatoka BOT, sasa BOT wanatumia formula gani kucalculate total goods na services zilizopo ndani ya nchi, ili kuhakikisha kwamba pesa inayoprintiwaa haizidi goods and services zilizopoto nchini??? hapo kumbuka kuna services kila siku zinaanzishwaa pasipo BOT kufahamu, mfano mamalishe vijijini wanatoa huduma ya chakula ila BOT hawafahamu, sasa huoni hesabu wanakosea wanaweza sababisha pesa kuwa kidogo sanaa zaidi ya huduma zilizopokwenye mzunguko, na kupelekea maisha kuwaa magumu kwa wananchi?? kwani mama lishe watakuwa wanakosaa wateja kwa sababu na wao wateja hela wanakosa hivyo kupelekea chakula kushuka bei, na watoa huduma kupata hasara

3.narudia tena sisi speculator wa currency ama forex traders tukimula broker na akatuiingizia tsh kwenye account zetu za bank, je nitakuwa nimewakamua watanzania au??? au nitakuwa nimewakamua watu wote wanaotumia USD?? hapa sijaelewa, maaana namkamua broker, dola zake then yeye ananiingia kama tsh kwenye account yangu bank


hesabu za uchumi bado zinanisumbuaa sanaa, sijui kwa nini nisingesomaga uchumi.
 
USA wanakamua mataifa maskin.
Hata mabilionea wao wanakamua raia walioko mataifa maskin mf Zuckerburg watumiaji wengi wa FB wapo mataifa maskin kwasababu mda wote wenyewe ni kuchat hawafikilii kufanya kazi.
wanakamua vipi, wanachukua hela ya nchi hizo ama???
 
So umasikini ni uwezo mdomo wa kuchukua pesa toka kwa mwingine
 
True thus ni nadra Sana kukuta mtoto wa tajiri anakuwa tajiri.
 
Utajiri ni uwezo binafsi wa kutumia fursa zinazowazunguka
 
well said

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
yes

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni mbumbumbu anayejua kutype,ngoja nikuelezee,bilionea moja anapotokea au kupatikana katika jamii,anakuwa amesababisha mamilionea wengi kutokea,na watu wanaomiliki Malaki ya pesa wasiohesabika,hebu angalia mfano wa bilionea Bakhresa amesababisha mawakala wangapi wanaouza bidhaa zake tena kwa mafanikio makubwa,wakati yeye anaingiza mabilioni,mawakala wanaingiza mamilioni,wale wachini wanaingiza Malaki,kinachoonekana katika uzi wako una mtizamo hasi dhidi ya mtu kuwa tajiri,mpaka umefika point ya kutumia neno "kukamua" wakati hata vitabu vya dini vinaruhusu mtu kununua kitu na kukiongeza thamani ili kupata faida,na ndiyo mwendo wa maisha,matokeo yake huo mfumo umerahisisha maisha kiasi kwamba mtu aliyeko Sumbawanga anaweza akatia Nazi kwenye wali wake wakati ambapo Rukwa hazistawi Nazi,au mtu wa Dar anaweza kula pitches toka Iringa wakati inawezekana hata haujui mti wa pitches ulivyo.
Kwa hiyo mtoa uzi kukusaidia tu ni kukuambia kwamba usiogope kuwa tajiri si dhambi,na mzunguko wa pesa upo ila tu kinachotakiwa ni wewe mwenyewe kujiposition ili huo mzunguko wa pesa upitie na kwako. Wewe
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hapo 1
Ili turudishe mkopo kwa riba,kuna matumizi lazima tujibane,ndo mana Kuna barabara nyingi hazijengwi.
Ni kujibana afu watanzania wanapambana.Hapa ndipo unyonyaji wa mzungu ulipo sasa,bado hajakuuzia bidhaa zake nk.Bado hajaiba madini,wanyama[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…