Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?
Bachelor of arts..na sasa anataka kufanya arts! Mbona yupo sahihi kabisa tatizo hapo ni kwenda kujifunza ujuzi kwa uyo ndugu unaesema darasa la Saba japo sipendi hii lugha. maana ata la Saba ni elimu pia ni nani ambaye alifika chuo pia bila kupita la Saba..?? Sasa cha kushauri ni vyuo vyetu kuwa na practical ya muda mrefu..mfano uyo binti mwaka wake wa mwisho angejikita kwenye eneo ambalo analipenda na huko ni full practical amna cha text wala Sapp apo akitoka awezi kwenda kuomba ujuzi Ni kumpa vitendea kazi na mtaji apo utaona tofauti yake na ambaye akwenda chuo kikuu..
 
Ila kiukweli kabisa cherehani inalipa sana,sasa ivi mjini wahindi wengi kwenye maduka yao kinachouzika sana ni Cherehani,Ila usishangae hajachelewa uyo baada ya miaka 1 mbele vyeti avichome
 
Hizi degree za "knowledge based education " ni shida sana.

Wenye elimu za "competence based education " hawapitii haya yote
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa kabisa mkuu,kuna RC wa moro alikua na PH.d in food security and Management Magu alivyoingia madarakani akamtumbua mapema tu,aisee yule mzee alikua analia huko magazetini anasema ooh mh.Rais nimekosa mimi nimekosa sana kama Petro alivyomezwa kwenye tumbo la samaki sijui nini.

Lkn wkt akiwa RC alikua akialikwa kwenye hafla mbalimbali alikua ndio bingwa wa kuwaambia vijana mjiajiri jamani eti Morogoro hii inakila aina ya utajiri hahah.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo alikuwa Dr. Rajab ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Ulanga.
 
Unamjua the speshoz?na mke wake? Ni mamilionea sasa kwa cherehani hiyo hiyo
 
Kwa wa kristo biblia inasema "watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa"

Biblia haijasema watu wana angamia kwa kukosa elimu imesema maarifa
Kumbe shule ni muhimu kwa sababu baadhi ya maarifa yanapatikana huko

Ila Kama shule/elimu unayosomea haikupi maarifa kwa hakika elimu hiyo ni bure kabisa na Haina maana kwa sababu hautakua na maarifa ya namna ya kukabiliana na maisha

Hoja ya pili mfumo wa nchi yetu kwa kiasi kikubwa bado unaandaa watu wakufanya kazi na sio wabunifu na ndo maana watu wengi wana shida ya pesa kwani hata wale wachache ambao wameamua kujiajiri utaona hao watu ni wazuri kufanya kazi ila pesa yao ni kiduchu Sana

Still mfumo wa elimu yetu ni tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili kama zako ndo inafanya watu wenye degree wasote wakitembea na bahasha wakati wasio na elimu wanalisha familia wakitembeza vifaa, so ipi bora kutembeza vifaa ili familia ile au kutembeza bahasha huku ukila hela za familia? Maji ukiyanywa kwa pupa lazima utapaliwa so alichofanya huyo ni kianzio tu hivyo usishangae miaka michache mbele akaanza kuajiri wenye degree

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom