The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 9,205
- 22,219
GT
Katika ulimwengu wa harakati za mapinduzi ya kisiasa na kusukuma nchi iende mbele kile kinachotokea Kenya ni sahihi kabisa maana wanaijenga nchi yao.
Ndugu zangu hakuna taifa lolote tajiri ambalo halijapitia madhira kama ya Kenya. Wanachofanya wakenya ni kutafuta kuheshimiana ili serikali iwe inatimiza kile wananchi wanataka pia kuepusha ufujaji wa mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka.
Kwa hali ilivyo sasa hakuna mwanasiasa wa Kenya atakuwa anaingia madarakani kufanya ujinga ujinga huu ndo utakuwa mwanzo wa Taifa hili kusonga mbele zaidi. Umewahi kujiuliza toka wakenya waanze vurugu back 2007 uchumi wao umeshuka au umepanda? Automatically wako vizuri kuzidi Tanzania.
Pamoja na vurugu za wakenya kutaka katiba na haki lakini sisi watanzania hatujawakaribia hata kidogo kiuchumi Wakenya wanajenga nchi yao, hata sisi tutafika huko kwenye kushikana mashati endapo CCM hawatachukua hatua Mapema, Chadema wamekuja na reforms ambazo ni msaada mkubwa kwa taifa na hata kwa wana CCM wenyewe maana mizengwe ndani ya chama tawala ni mingi .
Naomba nikukumbushe America, Europe na Asia hizo nyakati walishapitia wamepigana sana ndo maana kwa sasa wanaheshimiana hakuna aliyejuu ya sheria na huo ndo huwa mwanzo wa maendeleo katika taifa lolote lile.
Nakumbuka pia Miaka ya 90 kuelekea 2000 nchi za misri, Algeria, Morocco, Tunisia na kadhalika palikuwa hapakaliki viongozi walitolewa sana madarakani hadi pale mambo yalvyokaa vizuri leo wanakula maisha.
Uharibifu unaotokea kenya ni mdogo sana tofauti na kama serikali ingeachwa iendelee na Ufisadi, Wazungu wanasema no pain no gain. Watanzania lazima tupitie maumivu ili kuweza kufikia uhuru.wa kweli katika kusimamia rasilimali zetu la sivyo wachache wataendelea kutuibia na taifa kubaki katika umasikini mkubwa
Ukitaka jambo lolote Zuri lazima ulipe gharama wakenya wanalipa gharama ya kutengeneza nchi yao kwa vizazi vijavyo. Nakumbuka enzi hizo niko chuo boom ilikuwa ni 5000 per day UDSM tulikinukisha sana shukuru kawamba waziri wa elimu enzi hizo alikuja pale jasho lilimtoka toka kipindi hiko boom likawa 7000 kwa sasa sijui vijana wanapata shilingi ngapi.
Pengie bila mgomo wa siku kadhaa pale UDSM enzi hizo huenda boom lisingepanda kirahisi na vijana waliopo chuo leo wanafurahia tu pengine hata hawajui boom Liianzaje kupanda.
Kwa hiyo serikali ya CCM isipochukua hatua mapema Tanzania tunaelekea njia za Kenya lazima tutakuja kushikana mashati huko mbele ya safari sisi tutagombana kwa itikadi za vyama na dini ni swala la mda tu nakihurumia sana kizazi kijacho..
Reforms zinazotakiwa sasa na CHADEMA ni kwa ajili ya kuleta uwajibikaji wa viongozi wetu na si umwinyi. Mtu unamchagua leo anapotea miaka mitano halafu kipindi cha uchaguzi anakuja na Tshirt na anaamini lazima achaguliwe maana tume ya uchguzi ipo mfukoni mwake tukienda kwa mtindo huu Tanzania maendeleo tutayasikia kwa majirani.
Asanteni kwa kusoma