Mtu Mwenye fikra finyu pekee ndo anaweza kusema wakenya wanaharibu nchi yao

Mtu Mwenye fikra finyu pekee ndo anaweza kusema wakenya wanaharibu nchi yao

Kwa hiyo UK hakunaga uchaguzi wa vyama vya siasa?
Haujui UK inachagua PMs tu? Haujui the supreme Ruler wa UK anarithishwa??? You cant be seruous, Netherands? Spain? Hata hao Belgium, Sweden, Denmark, Norway n.k

Pamoja na kuwa hawa Monarchs wana limited political power lakini bado ndio supreme rulers, maana yake wameendelea na uzamani wao kwa kuounguza mdaraka tu lakini wafalme wapo na wanaishi kwa dedha za walipa kodi. democracy ni namna unavyoiishi kulingana na utamaduni wako tu... kina sisi sasa tukiletewa ni kupelekeana moto tu na kuharibu nchi zetu
 
Tz haikupigania uhuru kwa kuwa mwingereza hakuwa mkoloni, ndio maana tuliupata mezani, Kenya soma vita vya mau mau!
Na ndiyo maana hata multipatism hatukuipigania; maana yake kiutamaduni Tanganyika haiko embeded kwenye mapigano, ni ngumu kuiconvert leo; utamaduni utaendelea kubaki hivyo - kufikiri leo au kesho au keshokutwa watanzania wote wataingia barabarani dor whatever reason ni ndoto ngumu; mara zote ni ngumu kuukimbia utamaduni wako... ndiyo maana hata JPM alivyoondoka ghafla bado Nchi ilikabidhi kijiti kwa mtu mwingine, Nchi zingine zenye tqmaduni ya kupinduana pasingetosha...
 
Shida ni kuwa mnaanzisha mada na mnataka wote tufikilie sawa; njni maaana ya kutaka uhuru kama wewe ni dikteta na hauamini kwenye mitazamo tofauti??? Waafrika bado sana, kila mtu ni chawa wa mtazamo wake mwenyewe.... maana yake mtu wa aina yako ukipewa madaraka utakejeli, kufunga na kutukana wote wanaofikiri tofauti na wewe... utakuwa una tofauti gani na the current system.. ndio maana tunasema sisi bado sana
Kwahiyo wewe upo huru ama kweli jitu jeusi akili zero🤣🤣🤣
 
Haujui UK inachagua PMs tu? Haujui the supreme Ruler wa UK anarithishwa??? You cant be seruous, Netherands? Spain? Hata hao Belgium, Sweden, Denmark, Norway n.k

Pamoja na kuwa hawa Monarchs wana limited political power lakini bado ndio supreme rulers, maana yake wameendelea na uzamani wao kwa kuounguza mdaraka tu lakini wafalme wapo na wanaishi kwa dedha za walipa kodi. democracy ni namna unavyoiishi kulingana na utamaduni wako tu... kina sisi sasa tukiletewa ni kupelekeana moto tu na kuharibu nchi zetu
Wewe akili huna
 
Kuna mambo mnayatamani sana lakini bila kuangalia historia ya hizi nchi zetu na nini kinawasumbua Wakenya.

Kama Tanzania enzi za ukoloni - tulifanikiwa kupata uhuru kwa kupiga maneno tu, kama enzi za multipatism kuanzishwa nako ilikuwa ni baada ya kupewa tu na mamlaka kutokana na pressure za kipindi hicho, undhani itakuwa ni rahisi mtanzania kuingia barabarani kwa ajili ya uchaguzi???

Utamaduni wa Taifa ndiyo huamua nchi iendaje - ndiyo maana UK licha ya wao kututaka tufanye demokrasia lakini nchi yao inatawaliwa na familia moja in the name of King na maisha yanaendela.. huo ndio utamaduni wao.. kwa kuwa na sisi tumekuwa tunafanya mambo kwa utaratibu na utamaduni wetu kwa wakati sahihi, na kama upinzani utakuja kushika nchi basi Upinzani watashika madaraka bila hata vurugu na bila hata Chama tawala kushupaza shingo...

Kushadadia haya ya Kenya na kudhani yakija huku kwetu ndiyo tutapiga hatua ni swala la kushangaza sana. Jana wamekufa watu 16, na serikali imelipongeza Jeshi la Polisi - na haya yanayoendelea ni karma kwa Rais Ruto (alimisbehave sana enzi za Uhuru na kuchochea unrest hasa kupitia vijana) sasa kwa miaka miwili toka yeye awe Rais - Kenya ni kama iko kwenye autopilot mode....

Yapo ya kujifunza kutoka Kenya lakini sio Maandamano...
Wachache watakuelewa, na mwisho wa siku hayo maandamano huishia kupelekea wanasiasa wachache kupewa nafasi ndani ya serikali huku asilimia kubwa ya wananchi wakibaki kwenye umasikini wao wa siku zote.

Mfano kabla ya Odinga kuingizwa kwenye serikali Luo Nyanza ilikua ndio kitovu cha maandamano, ila baada ya yeye na wanachama wake kupata nafasi za uwaziri, ukatibu, ukuu wa mashirika na nafasi za ubalozi watu wa Luo Nyanza wakaona wapo ndani ya Serikali ya Ruto na hata maandamano ya Kipindi hiki hawajashiriki ila ki uhalisia ukienda huko Luo Nyanza (Homa bay, Kisumu etc) hali ya umasikini ni ya kutisha na hakuna mabadiliko yoyote ila ukikutana na mjaluo anakuambia ‘Tuko ndani ya Serikali’, upuuzi mtupu
 
Kumbe na Mimi basi fikira zangu ni finyu mwaka wa 20 Sasa wakenya wanauana wenyewe Kwa wenyewe

Mimi naona wanaharibu nchi yao
 
Wachache watakuelewa, na mwisho wa siku hayo maandamano huishia kupelekea wanasiasa wachache kupewa nafasi ndani ya serikali huku asilimia kubwa ya wananchi wakibaki kwenye umasikini wao wa siku zote.

Mfano kabla ya Odinga kuingizwa kwenye serikali Luo Nyanza ilikua ndio kitovu cha maandamano, ila baada ya yeye na wanachama wake kupata nafasi za uwaziri, ukatibu, ukuu wa mashirika na nafasi za ubalozi watu wa Luo Nyanza wakaona wapo ndani ya Serikali ya Ruto na hata maandamano ya Kipindi hiki hawajashiriki ila ki uhalisia ukienda huko Luo Nyanza (Homa bay, Kisumu etc) hali ya umasikini ni ya kutisha na hakuna mabadiliko yoyote ila ukikutana na mjaluo anakuambia ‘Tuko ndani ya Serikali’, upuuzi mtupu
We ambaye huandamani unazidiwa uchumi na wanaoandamana Kila siku tafakari kichwa chako vizuri
 
GT
Katika ulimwengu wa harakati za mapinduzi ya kisiasa na kusukuma nchi iende mbele kile kinachotokea Kenya ni sahihi kabisa maana wanaijenga nchi yao.

Ndugu zangu hakuna taifa lolote tajiri ambalo halijapitia madhira kama ya Kenya. Wanachofanya wakenya ni kutafuta kuheshimiana ili serikali iwe inatimiza kile wananchi wanataka pia kuepusha ufujaji wa mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa hali ilivyo sasa hakuna mwanasiasa wa Kenya atakuwa anaingia madarakani kufanya ujinga ujinga huu ndo utakuwa mwanzo wa Taifa hili kusonga mbele zaidi. Umewahi kujiuliza toka wakenya waanze vurugu back 2007 uchumi wao umeshuka au umepanda? Automatically wako vizuri kuzidi Tanzania.

Pamoja na vurugu za wakenya kutaka katiba na haki lakini sisi watanzania hatujawakaribia hata kidogo kiuchumi Wakenya wanajenga nchi yao, hata sisi tutafika huko kwenye kushikana mashati endapo CCM hawatachukua hatua Mapema, Chadema wamekuja na reforms ambazo ni msaada mkubwa kwa taifa na hata kwa wana CCM wenyewe maana mizengwe ndani ya chama tawala ni mingi .

Naomba nikukumbushe America, Europe na Asia hizo nyakati walishapitia wamepigana sana ndo maana kwa sasa wanaheshimiana hakuna aliyejuu ya sheria na huo ndo huwa mwanzo wa maendeleo katika taifa lolote lile.

Nakumbuka pia Miaka ya 90 kuelekea 2000 nchi za misri, Algeria, Morocco, Tunisia na kadhalika palikuwa hapakaliki viongozi walitolewa sana madarakani hadi pale mambo yalvyokaa vizuri leo wanakula maisha.

Uharibifu unaotokea kenya ni mdogo sana tofauti na kama serikali ingeachwa iendelee na Ufisadi, Wazungu wanasema no pain no gain. Watanzania lazima tupitie maumivu ili kuweza kufikia uhuru.wa kweli katika kusimamia rasilimali zetu la sivyo wachache wataendelea kutuibia na taifa kubaki katika umasikini mkubwa

Ukitaka jambo lolote Zuri lazima ulipe gharama wakenya wanalipa gharama ya kutengeneza nchi yao kwa vizazi vijavyo. Nakumbuka enzi hizo niko chuo boom ilikuwa ni 5000 per day UDSM tulikinukisha sana shukuru kawamba waziri wa elimu enzi hizo alikuja pale jasho lilimtoka toka kipindi hiko boom likawa 7000 kwa sasa sijui vijana wanapata shilingi ngapi.

Pengie bila mgomo wa siku kadhaa pale UDSM enzi hizo huenda boom lisingepanda kirahisi na vijana waliopo chuo leo wanafurahia tu pengine hata hawajui boom Liianzaje kupanda.

Kwa hiyo serikali ya CCM isipochukua hatua mapema Tanzania tunaelekea njia za Kenya lazima tutakuja kushikana mashati huko mbele ya safari sisi tutagombana kwa itikadi za vyama na dini ni swala la mda tu nakihurumia sana kizazi kijacho..

Reforms zinazotakiwa sasa na CHADEMA ni kwa ajili ya kuleta uwajibikaji wa viongozi wetu na si umwinyi. Mtu unamchagua leo anapotea miaka mitano halafu kipindi cha uchaguzi anakuja na Tshirt na anaamini lazima achaguliwe maana tume ya uchguzi ipo mfukoni mwake tukienda kwa mtindo huu Tanzania maendeleo tutayasikia kwa majirani.

Asanteni kwa kusoma
Historia ni mwalimu asiekosea.
Kenya wamefanya uchaguzi majuzi tu, kikashinda chama cha upinzani. Aidha, tangu wadanganywe na kuamini tatizo ni KANU, waitoa KANU madarakani na kuwaweka wapinzani kupitia MWAI KIBAKI.

Tangu hapo wameendelea kubadilisha vyama kila uchaguzi na bado wanaona wanapaswa kubadilisha tena. Leo wanaimbishwa wimbo wa RUTO must go na wanauimba wakati hao hao wanaowaambia waimbe huo wimbo ndo waliwaaminisha RUTO ndo solution wakati wa kampeni za uchaguzi.

Kama kuwa na fikra sahihi ni kuona maandamano yanayoratibiwa wa wanaharakati wanaofadhiliwa na mataifa ya magharibi (rejea kauli ya RUTO kuwa nyuma ya maandamano wako Ford Foundation) ni kujenga nchi, ACHA niendelee kuwa na fikra finyu tu.
 
Niko pamoja na wewe kuwapa maflowers wakenya wetu,no blood no changes,ukondoo wetu waranzania ndio umetufikisha hapa tulipo ndio maana tunafanyiwa maovu ya kila namna na ccm
 
We ambaye huandamani unazidiwa uchumi na wanaoandamana Kila siku tafakari kichwa chako vizuri
Maandamano ndio yanaleta uchumi?? Ukitaka hali halisi ya uchumi ingia hapo Kenya ukaone hali ya mwananchi wa kawaida ilivyo ngumu usiishie kusoma mitandaoni na kufuata mkumbo.
 
Kuna mambo mnayatamani sana lakini bila kuangalia historia ya hizi nchi zetu na nini kinawasumbua Wakenya.

Kama Tanzania enzi za ukoloni - tulifanikiwa kupata uhuru kwa kupiga maneno tu, kama enzi za multipatism kuanzishwa nako ilikuwa ni baada ya kupewa tu na mamlaka kutokana na pressure za kipindi hicho, undhani itakuwa ni rahisi mtanzania kuingia barabarani kwa ajili ya uchaguzi???

Utamaduni wa Taifa ndiyo huamua nchi iendaje - ndiyo maana UK licha ya wao kututaka tufanye demokrasia lakini nchi yao inatawaliwa na familia moja in the name of King na maisha yanaendela.. huo ndio utamaduni wao.. kwa kuwa na sisi tumekuwa tunafanya mambo kwa utaratibu na utamaduni wetu kwa wakati sahihi, na kama upinzani utakuja kushika nchi basi Upinzani watashika madaraka bila hata vurugu na bila hata Chama tawala kushupaza shingo...

Kushadadia haya ya Kenya na kudhani yakija huku kwetu ndiyo tutapiga hatua ni swala la kushangaza sana. Jana wamekufa watu 16, na serikali imelipongeza Jeshi la Polisi - na haya yanayoendelea ni karma kwa Rais Ruto (alimisbehave sana enzi za Uhuru na kuchochea unrest hasa kupitia vijana) sasa kwa miaka miwili toka yeye awe Rais - Kenya ni kama iko kwenye autopilot mode....

Yapo ya kujifunza kutoka Kenya lakini sio Maandamano...
Marehemu 16 walitokana na hayo maandamano. Siku ikifika muache keyboards mkapambane katika field.
 
1

Wewe ni kati ya watu wa hovyo wachache wanaoamini kuna amani Tanzania. Huwezi amini hadi leo TZ tunatumia katiba ya mwaka 77 kabla ya vyama vingi.
Mpaka leo more than 60 years tuna tume ya uchaguzi ya chama kimoja halafu unasema tuendelee kupiga piga maneno CCM itaachia aha ha ha 😂 kwa kweli unashangaza.
Acha kujiandikia ujinga.Tanzania bado iko vizuri.Usitake kutuaminisha nchi iko kwenye hali mbaya wakati watu wako busy na maisha yao ya kila siku.Matatizo yaliyopo niyakawaida na hayajafika kiwango unachotaka kutuaminisha.Kenya wanachofanya ni uharibifu wala sio kujenga.Utawaona wanajenga kama utatumia akili ndogo ila kiuhalisia hawana hoja zakujenga zaidi ya mihemko ya vijana ambayo unayo ata wewe bila kujua nchi haiendeshwi hivyo.wewe ungekua kiongozi wa nchi hiyo nchi ingeharibika siku hiyo hiyo.
 
Wachache watakuelewa, na mwisho wa siku hayo maandamano huishia kupelekea wanasiasa wachache kupewa nafasi ndani ya serikali huku asilimia kubwa ya wananchi wakibaki kwenye umasikini wao wa siku zote.

Mfano kabla ya Odinga kuingizwa kwenye serikali Luo Nyanza ilikua ndio kitovu cha maandamano, ila baada ya yeye na wanachama wake kupata nafasi za uwaziri, ukatibu, ukuu wa mashirika na nafasi za ubalozi watu wa Luo Nyanza wakaona wapo ndani ya Serikali ya Ruto na hata maandamano ya Kipindi hiki hawajashiriki ila ki uhalisia ukienda huko Luo Nyanza (Homa bay, Kisumu etc) hali ya umasikini ni ya kutisha na hakuna mabadiliko yoyote ila ukikutana na mjaluo anakuambia ‘Tuko ndani ya Serikali’, upuuzi mtupu
Sahihi kabisa Mkuu;

Ukisikiliza speech ya leo ya Rais Ruto, utaona hata yeye anakerwa sana na maandamano hayo....
 
Keyboard warriors kwa nini huwa hamjitokezi CHADEMA wakiitisha maandamano yao? Au mnataka watu wengine wajitolee kuandamana kwa niaba yenu? Kenya haina cha kuifundisha Tanzania kuanzia demokrasia hadi uchumi. Huo uchumi unaotajwa kuwa mkubwa unawanufaisha kundi dogo sana la wakenya ila wengi wana hali ngumu mno. Hayo maandamano yanazidi kuiharibu Kenya badala ya kuijenga. Mwisho wa hayo maandamano ni serikali ya wahuni wengine ambao nao watahujumiwa pia.
 
Back
Top Bottom