Mtu mweusi[ Mwaafrika ] ni uzao wa Adamu na Hawa.Adamu na Hawa hawakuwa wazungu, la hasha. Walikuwa watu weusi.
Kwa mujibu wa biblia, soma kitabu cha Mwanzo; 25: 24-26.
Ukitafakari kwa makini maandishi ya biblia, utajua ya kwamba wazungu walitokana na uzao wa Esau, mtoto wa Isaka na mkewe Rebeka.
Rebeka alizaa watoto mapacha; Esau na Yakobo. Biblia inatuambia Esau alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Yamkini alikuwa tofauti na rangi ya wazazi wake ndiyo maana ya kutoa maelezo juu ya mtoto wao. Lakini maelezo ya rangi ya Yakobo hayapo. Hivyo pasiposhaka Yskobo alikuwa na rangi asilia ya wazazi wake kutoka kwa Adamu na hawa.
Kwa hiyo wazungu ni kizazi cha Esau na weusi ni kizazi cha Yakobo. Hayo ni mawazo yangu. Hebu nawe tafakari kwa kusoma kitabu cha Mwanzo:
25:24 Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake.
25:25 Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.
25:26 Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo.