Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Hahaa...mtoto akiwa bright huhitaji kumpeleka mashule yenye majina makubwa sijui ada mil. 10. Mwache hapo hapo ila habari yake wataipata tu kwenye matokeo ya kitaifa. Mimi ilinigharimu niliposoma O-level private ambapo kila kipindi mwalimu anaingia, shida ikaja A-level mwalimu humwoni na material unajitafutia. Kwenye mazingira kama hayo ndo utamwona mwanafunzi ambaye ni kichwa.....
Mkuu, kama pesa ipo mpeleke mtoto shule nzuri
 
Si kweli. Tunaona changamoto sana kwa hawa waliosoma Kayumba na kubahatika kufika level za kimataifa kwenye kazi za kimataifa.
-
Wengine walifanikiwa kufika level hizo kwa Connection tu. Kwa mfano nafanya kazi na Mtanzania mwenzangu kwenye International Organizational nchini Nambia, huyu Mdada amepata kazi kwenye hiyo Organization kwa sababu tu Ndugu yake ni Balozi wa Namibia.
-
Imemlazimu kufanya short course kuanzia Lugha mpaka Communications Skills na nyinginezo kwa sababu yeye mwenyewe anajionea aibu.
-
Hizo International school zinawajenga watoto vizuri sana hata kwa KUFIKIRI na kujiamini na mzazi ukiwa msimamizi mzuri wa mtoto wako atafika mbali sana na atakuwa very presentable kwa fadhila za International Schools.
-
It is very serious issue sisi tulio kwenye International Organization tunaona mengi na tunaona changamoto ya Mfumo wetu wa elimu na Africa kwa Ujumla.
-
Ukiona Kayumba yupo kwenye hizi Organization na anafanya vyema ujue huyo kaji mix sana na anapenda kujifunza vitu mbalimbali au ana exposure ya maisha.
-
Kwanza sisi wabongo hata kuongea hatujui, sijui kwa nini ! Sio English wala Kiswahili, hatujui kuongea na wala hatufikirii tunachongea.
-
Ukitaka kuona hilo angalia wasanii wetu wanavyojibu maswali, angalia wachezaji mpira wakihojiwa akiwemo Samatha, zero kabisa, njoo kwenye ngazi za viongozi, zero kabisa, sio Kiswahili wala English.
-
Msanii anaejua kuongea vyema Kiswahili na English ni Sepetu na Vanesi na Kiongozi ni Mkapa na January tu.
-
Shida ipo sana eneo hili na ndio maana once it comes about International Interviews , yaani WATZD huwa ni wa mwisho na hapo unakuta mtu ana vyeti vizuri na pass Marks zake.
Mpaka inakatisha tamaa kabisa.

Kuna vituko vilitokea shirika la reli aisee..
 
Nadhani serikali ijaribu kubuni mfumo mzuri utakaojengea wanafunzi ufahamu na uelewa wa kusoma na kuweza kutatua changamoto za mazingira yetu. Sio kusoma ma theory tu yaliyo solve nchi za ulaya na kusahau mazingira yetu na changamoto zake.
Pia sikuhizi primary hesabu ni mutliple choice, huko si ndo kufanya watoto wawe wavivu.
cariha suala la elimu sio kazi ya serikali tu. Hapana unakosea. Mtoto na mzazi pia wana mchango mkubwa sana katika kutatua changamoto hii.

Siku hizi access ya internet ni kubwa kiasi kwamba mtoto anaweza akaongozwa vema na mzazi anayejitambua katika kujiongezea maarifa.
 
Umetoka nje ya Mada.

Talent ni natural born thing wala hufundishwi na hakihitaji shule. Ukianza kufundishwa hiyo sio Talent bali unaweza kugundua Talent yako kupitia elimu na shule.

it is something you have never been taught. It comes out of the blue na ukiulizwa how did you know that , the honesty answer would be I don’t Know.
Talent inakuzwa, na sehemu ya kukuza hio talent ni shule ndio maana wakaanzisha shule za vipaji ingawa lengo la hizo shule halikufikiwa.Wenzetu huko ulaya was Academy za soka.Marekani wana Jim club kukuza mabondia.Hakuna talent inayojikuza yenyewe ndi maana Diamond na wasafi yake huwachukua wasanii kuwakuza, kama kungekuwa na shule kulikuwa hakuna haja hizo lebo.
 
Mbona wengine tumesoma hizi hizi shule za sirikali, tena shule ya msingi kijijini kwa babu kuongea kilugha mwanzo mwisho lakini tumefanikiwa kupata scholorship kusoma Masters na PhD kwenye international universities ambazo zipo kwenye world ranking ya 10 bora, what happened?
Haijaishi umesoma Mpaka level gani foundation ndio kila kitu Nina uhakika reasoning yako and analytical skills zako ni tofauti kabisa na wale watoto wa Breibum na IST
 
Umeona sasa [emoji23][emoji23][emoji23] yale yale.
Ukisema yaleyale ndiyo unakuwa umeelewekaje/umesemaje au ndiyo unaongea kimataifa

Ulichoonge mwanzo hujaeleweka fafanua
Basi bado unaleta manyanga
 
Mkuu kwanza waliosoma International school 80 target yao ni kusoma International Universities na wakifaulu vizuri A-levels na kuwa assessed kwenye CIA wanaenda hizo Versitt za nje ....

hao wachache wanaobaki basi unakuta wamepoteza passion kutokana na kuhisi wameshuka standard hata masomo yatakuwa tofauti maana mfano kuna wanaosomea Art ya kuchora mavinyago na macartoon hao ukimleta atachagua masomo yasio preference yake...
Sasa mbona watu ninaowafahamu mimi ambao walisoma International asilimia kubwa wamesoma vyuo vyetu vya Kibongo,Wameajiriwa kwenye fani zile zile za sisi akina Yakhe,Sasa je,unataka kuniambia kuwa hao wote wameshuka kiwango?.
 
Ukisema yaleyale ndiyo unakuwa umeelewekaje/umesemaje au ndiyo unaongea kimataifa

Ulichoonge mwanzo hujaeleweka fafanua
Basi bado unaleta manyanga
Una IQ ya ngapi ndugu? Hadi unashindwa kuelewa vitu simple kama vile ?
 
Sasa mbona watu ninaowafahamu mimi ambao walisoma International asilimia kubwa wamesoma vyuo vyetu vya Kibongo,Wameajiriwa kwenye fani zile zile za sisi akina Yakhe,Sasa je,unataka kuniambia kuwa hao wote wameshuka kiwango?.
mkuu fatilia vizuri sababu za wao kusoma hapa....kumbuka ili kuweza kuwa qualified kusoma nje kutokea International schools lazima upitishwe na CIA (Cambridge International Assessment) tena hiyo ni hatua ya pili baada ya kupita AS inayofanywa sana na walimu wa hapohapo shuleni... So unaweza kuwa na expectation ya kusoma nje ila ukakosa vigezo ukaamua kusoma hapahapa..

Mimi kuna alumn wa miaka 2 iliyopita ninaowajua walisoma shuleni hapa 80 wote wameenda vyuo vya nje na waliofail wengine wanapiga kazi office za wazee wao wengine wanasoma hapa bongo....

Ila pia unaweza soma PYP, MYP kwa primary au ukafanikiwa vuka hadi olevel na alevel wanaotumia IGCSE ukamaliza alafu uchumi ukawa mbaya home, ukaenda shule za kawaida as long as unaufaulu mzuri.....

So ni kweli wanaosoma bongo wapo ila wachache sana na wanakuwaga na sababu 2 tu kukatwa na CIA au uchumi bro
 
Mtu ukiwa na hela ya kueleweka ama kama unataka kuwekeza kweli kwa watoto wako, wasomeshe international schools au shule zenye mitaala ya kimataifa.

Hizi shule zenye mitaala ya kimataifa zinawajenga watoto kwenye analytical skills, reasoning, logic, creativity, competence na mambo kama hayo.

Ukikutana na mtoto wa darasa la 6 wa hizi shule, reasoning yake ama analytical skills zake ni sawa na kijana wa form six wa necta schools.

Shule hizi hazilengi kuona mtoto anapata nini au maksi gani darasani bali kuibua talents nyingine alizonazo mtoto sio hizi za necta ambazo zimejikita kwenye ufaulu tu wa mwanafunzi.

Ukitaka kuwekeza kwenye elimu ya kweli kwa mwanao na kama uwezo upo peleka mwanao shule zenye mitaala ya kimataifa.
Wazo zuri
 
cariha suala la elimu sio kazi ya serikali tu. Hapana unakosea. Mtoto na mzazi pia wana mchango mkubwa sana katika kutatua changamoto hii.

Siku hizi access ya internet ni kubwa kiasi kwamba mtoto anaweza akaongozwa vema na mzazi anayejitambua katika kujiongezea maarifa.
Ndio swala la elimu ni la wote Ila think about mtaala Raia wakawaida huwezi kujibunia mtaala hapo lazima ushirikiane na serikali ili Mambo yaende vizuri. Pia kiongozi wa mwalimu unahitajika pia maana mzazi huwezi google Jambo lolote na ku mu feed mtoto tu bila kuchuja
 
Mtu ukiwa na hela ya kueleweka ama kama unataka kuwekeza kweli kwa watoto wako, wasomeshe international schools au shule zenye mitaala ya kimataifa.

Hizi shule zenye mitaala ya kimataifa zinawajenga watoto kwenye analytical skills, reasoning, logic, creativity, competence na mambo kama hayo.

Ukikutana na mtoto wa darasa la 6 wa hizi shule, reasoning yake ama analytical skills zake ni sawa na kijana wa form six wa necta schools.

Shule hizi hazilengi kuona mtoto anapata nini au maksi gani darasani bali kuibua talents nyingine alizonazo mtoto sio hizi za necta ambazo zimejikita kwenye ufaulu tu wa mwanafunzi.

Ukitaka kuwekeza kwenye elimu ya kweli kwa mwanao na kama uwezo upo peleka mwanao shule zenye mitaala ya kimataifa.
Tatizo ada zao hadi mil 45.
 
Hapa wengi wanawaza kama mkoloni alivyopanga iwe.Watu wanataka mtoto aongee kingereza kama vile hapa Uingereza.Hizo International organization zinatoa ajira ngapi mpaka tufate mtaala wao ? Mmesoma curriculum development au mnalopoka bila ufahamu.Yani tubadili mtaala uwe wa kimataifa nchi gani imewahi Fanya hivyo ? Hata Marekani hawawezi kufanya huo ujinga.
Hivi Tz unaweza ishi mahala mpaka ukajuta hicho kingereza ulijifunza cha nini maana Hana wa kuongea nae.
Huwa najiuliza watu waliopelekwa kusoma ulaya wameleta faida gani kwa nchi zaidi ya kuleta machotara wa kizungu. Ni bora anaesoma kayumba m,kama kuna teknolijia au jambo kubwa tujuzane.Wasomi wetu hao wanaojua kingereza wameshindwa hata kuandika vitabu ili tujitegemee tusiagize virabu vya wazungu.
 
Lakini mbona kibongo talent nyingi zinatoka kwa watu ambao ni masikini na wasio na elimu kubwa
Mbona hatuoni hao international wakiongoza kwenye fani nyingi zinazotumia vipaji sana
Tajiri namba moja wa Tanzania bwana Mo kasoma shule gani?? Mo amesoma International School of Tanganyika (IST)

Watu wote tunahangaika kutafuta hela/utajiri. Sasa kama tajiri namba moja kasoma IST unataka kutulinganishia na nani mwingine??
 
Kama uwezo wako sio wa kumpeleka mwanao hizo shule, mpeleke shule zetu hizi hizi kisha mtengenezee mazingira hayo ya ki international nyumbani.

Mfundishe kujiamini, ongea nae ktk mazingira ya kutaka ushauri wake utamjengea reasoning skills, usiwe unamfokea hovyo, tembea nae maeneo mbalimbali apate exposure, muache afanye anachokitaka ilimradi hakivuki mipaka ya kimaadili.
 
Back
Top Bottom