Nationalism is an infantile disease. It is the measles of mankind
- Albert Einstein.
Siko hapa kwenye squabbles za Wakenya na Watanzania.
Najieleza tu.
Watanzania tuna lugha yetu tunaelewana wenyewe.
Hii inawezekana East Africa nzima ipo, lakini Tanzania nimeona sana. Labda kwa sababu ndipo nilipozaliwa na kuishi sana.
Haya ni baadhi ya matatizo, haijalishi mtu ana elimu vipi, mara nyingi sana yanajitokeza.
1. Kuongea bila kumaliza sentensi. Kuanzia mtoto mpaka rais, si ajabu kukuta mtu anaongea, halafu anaachia sentensi inaelea hewani bila kuimalizia. Sasa sijui ni aina mahsusi ya mawasiliano au ni mapungufu.
2. Kuongea katika namna ambayo mawazo hayana mpangilio. Mawasiliano bora yanajali mpangilio. Hoja inaanza kutambulishwa, maana za kiini cha hoja zinanyambulishwa, halafu maelezo mengine yanafuata. Tanzania si ajabu mtu akarukia mwisho wa hoja hata bila ya kuitambulisha.
3. Watu kuchukulia kirahisi tu kwamba mtu mwingine anajua wanachozungumzia kama wanavyojua wao. Hili linachangia sana tatizo namba 2 hapo juu.
4. Kujadili mambo kwa ushabiki, mahaba na hashuo badala ya kuangalia hoja. Watu wanachukua upande kama ushabiki wa timu za Simba na Yanga, halafu, baada ya hapo, watafanya kila hila upande wao uonekane ndio bora. Bila kujali hoja. Iwe kwenye siasa, dini, kujadili nchi, na kadhalika. Hapa utakutana na logical non sequitur zote, ad hominem attacks zote, deus ex machina zote, ili mradi mtu ashinde mjadala tu.
5. Non verbal communication. Hili ni janga la kitaifa. Unaweza kukuta rais anahutubia taifa, hapo hapa anajishika pua kama anataka kupenga makamasi.
6. Mikingamo katika dhana. Jana nilikuwa namsikiliza jamaa mmoja shabiki wa timu ya soka ya Yanga. Anasems anataka mambo yawe fair, Yanga ipewe nafasi ibebwe kwa sababu Yanga ilipigania uhuru wa nchi. Yani hapo hapo anasema anataka mambo yawe fair, hapo hapo anasema anataka Yanga ipendelewe. Haoni contradiction hapo. Kauli kama hizi kwa Watanzania si kitu cha ajabu. Hata siasa zetu za "Ujamaa na Kujitegemea" ni contradiction. Ujamaa maana yake ni kutegemeana, na kutegemeana ni kinyume cha kujitegemea, hivyo "Ujamaa" na "Kujitegemea" ni vitu vinavyopingana. Sisi tunaona sawa tu.
7. Kukosa uwazi. Mawasiliano ya Watanzania wengi yametawaliwa na hila na kukosa uwazi. Ama kwa sababu wengi hawana uwezo wa kuchambua hoja na kuiwakilisha vyema, ama kwa sababu hata wenye uwezo wa kukwambia kitu ambacho wanaona hutakipenda, huenda kujipendekeza, kutaka suluhu ya uongo, kueleza mambo yao kama utani na dhihaka, na kadhalika. Kwa Watanzania wengi ni bora akukubalie jambo bila ridhaa ya kweli, halafu akusengenye pembeni, kuliko akuambie ukweli na kukukatalia jambo mbele yako.
8. Kasumba/Generalization/Stereotyping.
Watanzania wakitaka kuoa wengi wanaanza kuuliza "kabila fulani tabia zao zipi?". Hili tatizo la ukabila hata Kenya lipo, tena zaidi.Bora yetu, huko hata kuoana makabila tofauti nafikiri bado ni mzozo. Ila Tanzania watu wanaishi kwa kukariri sana na labda kwa kiasi fulani kuna mantiki, lakini imezidi sana. Mpaka inaharibu mawasiliano. Kwa sababu mtu kabla hajawasiliana na kujua ukweli kashaweka dhana Wachaga wezi.
Kuna hotuba moja ya rais Magufuli aliletewa kesi ya Mchaga akasema nyie mlitegemea nini, huyo mtu ni Mchaga, akimaanisha kuwa walitakiwa wajue Wachaga ni wezi. Halafu nchi hiyo hiyo kuna watu wanajisifia kinafiki haina ukabila. Yani kwa watu wengine ukiwa unaishi nje wewe ni beberu tu. Cha ajabu, wewe beberu wakipata matatizo wanakufuata kukuomba msaada! Hapa tqtizo la kasumba limechanganyika na tatizo la namba 6 la contradiction. Wao wanaona sawa tu.
9.Kutotaka kujifunza. Watanzania wengi unaweza kuona mtu kakosea, ukamsahihisha. Tena kwa heshima tu, iki asikisee tena sehemu mbaya zaidi. Mwenzako anakwambia "Si umeelewa tu?". Yeye ukweli kwamba kakosea na anatakiwa kujifynza si kitu muhimu. Anakulazimisha wewe uwe umeelewa hata alipokosea.
10. Uzalendo wa kijinga. Watanzania wengi serikali inawapiga, inawatukana, inawanyanyasa. Lakini wanaitetea bado kwa "cognitive dissonance" ya " my country, wrong or right".
Si Watanzania wote walio hivyo. Tuna watu sharp wengi. Watu wanafunguka macho. Upinzani unakua.
Lakini naona kama majority ndiyo wako hivyo. Kibaya zaidi wengine wengi ni watoto wa mjini ambao walitakiwa kujua zaidi.
Before you gleefully gang on us with vitriolic schadenfreude, let it be known that I am a country agnostic equal opportunity offender and I can dish the same ten point harangue on Kenya.